Waziri wa Nishati aagiza wakuu wa wilaya kukamata na kuwaweka mahabusu wananchi watakaoshindwa kuunganisha umeme kwenye nyumba zao baada ya miezi sita

Cannabis

JF-Expert Member
Jan 20, 2014
8,938
25,281
IMG_20210219_091420.jpg

Waziri wa Nishati Dkt.Medard Kalemani amewaagiza wakuu wa wilaya nchini wawakamate na kuwaweka mahabusu wananchi wanaoshindwa kuunganisha umeme katika nyumba zao baada ya miezi sita kwa kuwa serkali inatumia gharama kubwa kupeleka umeme katika vijiji na vitongoji vyao.
 
View attachment 1706048

Hivi huko mahabusu na magereza kuna ajuaye kama wanapigishwa japo nyungu? Vipi yale mambo yetu ya nimcaf, bupeji, covido au chanjo ya Madagascar wanapatiwa?

Au ni ule mwendo wa kuuwana kibudu tu?
 
Kama serikali inatumia gharama kubwa kupeleka umeme katika vijiji na vitongoji vyake kwanini isimalizie tu hizo gharama kidogo zinawashinda hao wanyonge huko vijijini.

Yote kwa yote umeme kila mtu kijijini anapenda awe nao nyumbani ila ndio hivyo uchumi hauruhu pia nyumba unakuta ya tope Sasa mtu ataweka umeme?
Hawa viongozi nahisi kuna shida au Kama sivyo huwa wanaonge TU bila kuangalia uhalisia wa kitu husika
 
View attachment 1706048
Waziri wa Nishati Dkt.Medard Kalemani amewaagiza wakuu wa wilaya nchini wawakamate na kuwaweka mahabusu wananchi wanaoshindwa kuunganisha umeme katika nyumba zao baada ya miezi sita kwa kuwa serkali inatumia gharama kubwa kupeleka umeme katika vijiji na vitongoji vyao.
Wananchi wamepelekewa umeme mpaka uwanjani, shida ni kwamba hawana uwezo wa kufanya wiring ndani ya nyumba zao. Shida iko hapo tu. Wengine hata ile 27,000/- ya kuunganisha umeme hawana. Umasikini umetamalaki sana. Watawafunga wengi mno, kama mkakati hautabadilishwa
 
Ameagiza akiwa wapi.Kuna maeneo umeme umefika toka 2017 hadi leo hawajawekewa transformer ili wananchi waweze kuutumia hilo halioni?
 
View attachment 1706048
Waziri wa Nishati Dkt.Medard Kalemani amewaagiza wakuu wa wilaya nchini wawakamate na kuwaweka mahabusu wananchi wanaoshindwa kuunganisha umeme katika nyumba zao baada ya miezi sita kwa kuwa serkali inatumia gharama kubwa kupeleka umeme katika vijiji na vitongoji vyao.
Weka link ,, la sivyo ni uzushi.
 
Inatakiwa kutengeneza mazingira mazuri ya Uchumi wa watu ili waendane na hivyo vitu mtatengeneza bara bara Kama Kodi ya kuingiza magari itakua juu mtakamata wananchi kwa kutokununua magari pia mimi nadhani tatizo mnalijua ila mnazunguka tuu mnapoambiwa watu vyuma vimekaza sio kwamba wanaigiza ni kweli watu pesa hawana ila kwa kuwa mnakuwa kwenye mavieiti na vikao hakuwezi kujua kuwa ndugu zako kijijini wanakosa pesa hata kidogo watu wapo wanaokosa pesa ya kula unazungumzia umeme???
 
Back
Top Bottom