Waziri wa Nchi Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar akutana na Ujumbe wa umoja wa Makanisa Tanza | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waziri wa Nchi Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar akutana na Ujumbe wa umoja wa Makanisa Tanza

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by nngu007, May 30, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  May 30, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  [h=2]Wednesday, May 30, 2012[/h]
  [h=3][/h]  [​IMG]
  Na Miza Chande-Maelezo Zanzibar  Waziri wa Nchi Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Mohammed Aboud Mohammed ameuhakikishia umoja wa Mapadri nchini kuwa malamiko ambayo wameyatoa kwa Serikali atayawasilisha kwa maandiko kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Kikwete na Rais wa Zanzibar Dk.Ali Mohammed Shein.


  Malalamiko hayo yanatokana na vurugu ambazo zilitokea mwishoni mwa wiki katika maeneo ya mji wa Zanzibar ambapo Makanisa matatu yalichomwa moto na kusababisha uharibifu wa mali mbali mbali za Makanisa.


  Waziri Aboud ameyasema hayo alipokutana na Ujumbe wa umoja wa Makanisa Tanzania ulioongozwa na Askofu Mkuu wa Kanisa Anglikana Dk. Valontine Mokiwa katika Afisi ya Waziri huyo Mjini Zanzibar.


  Amesema Serikali na kila mwananchi mpenda amani amehuzunishwa sana na fujo zilizotokea na kuahidi kuwa Jeshi la Polisi linaendelea kufanya kazi yake ya kuwatafuta wale wote waliohusika na kuchukuliwa hatua za kisheria.


  Waziri Aboud amesema amefurahishwa na subra ambayo Wakristo hao wameichukua bila ya kulipiza kisasi jambo ambalo linawajengea heshima kubwa kwa jamii.


  Amezisisitiza Taasisi za dini kuendelea kuhubiri amani kama lengo la taasisi hizo linavyosema na kuongeza kuwa kama kuna mambo ambayo yanafaa kuzungumzwa ni suala la ukosefu wa ajira na umasikini nchini.


  Amesema Viongozi wa Dini wanapaswa kuwa na mipaka,busara na elimu wa yale wanayoyahubiri na kuwataka wananchi kuweza kuchambua juu ya viongozi ambao wanafaa kusikilizwa na wale ambao hawafai kusikilizwa.


  Aidha amewahakikishia Viongozi hao wa dini kuwa na amani na kwamba ulinzi umeimarishwa katika Sehemu zao za ibada ili kuweza kuzuia watu ambao hawaitakii mema Zanzibar.


  Kwa upande wake Askofu Mkuu wa Kanisa Anglikana Dk. Valontine Mokiwa amesema kuwa matukio ambayo yamekuwa yakifanyika yamepindukia mpaka Zanzibar lakini Serikali ya Mapinduzi imekuwa imeonekana kuwa na imani kubwa wakati hali inakuwa mbaya.


  Amdai kuwa Makanisa 25 katika Visiwa vya Unguja na Pemba tokea mwaka 2001 yameshambuliwa lakini hakuna hatua yoyote ambayo imechukuliwa kwa wahalifu hao jambo ambalo linawapa shaka.


  Mokiwa amesema Jamii ya Wakristo nchini ina hamu ya kujua nani kahusika na kuchukuliwa hatua za kisheria na siyo tu kuishia kuambiwa Jeshi la Polisi linaendelea kuwatafuta wahalifu hao.   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  May 30, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  "Mokiwa amesema Jamii ya Wakristo nchini ina hamu ya kujua nani kahusika na kuchukuliwa hatua za kisheria na siyo tu kuishia kuambiwa Jeshi la Polisi linaendelea kuwatafuta."

  Good Start... We can Talk... Is it? Hate is not PEACE!!!
   
 3. Tume ya Katiba

  Tume ya Katiba JF-Expert Member

  #3
  May 30, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,892
  Likes Received: 732
  Trophy Points: 280
  Mh hii kama tamthiria!

  Kamwandikia barua shein na JK!
   
 4. t

  tpmazembe JF-Expert Member

  #4
  May 30, 2012
  Joined: Jan 5, 2012
  Messages: 2,474
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  na kweli ni tamthilia kati yao kuna wakumkamata kiongozi wake wa dini?
   
 5. Prophet

  Prophet JF-Expert Member

  #5
  May 30, 2012
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 272
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 45
  Sitegemei kusikia hatua stahiki zimechukuliwa kwa wahuni hawa
   
 6. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #6
  May 30, 2012
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  wapendwa,

  hebu wanasiasa wetu waache kutoa "maagizo" au "kukutana" na somebodies, bali watuambie; wanafanya juhudi gani kuudumisha muungano zaidi ya sherehe za kila mwaka na kugawana vyeo na "bahasha za posho" kati yao wenyewe wanasiasa wa bara na visiwani?

  kama muungano hauko mioyoni mwa wananchi na umesalia kwenye denda za wanasiasa pekee, tena zitokanazo na posho haramu za kujitwalia kwa mabavu kutoka katika kodi za wananchi masikini wa taifa hili, nani ataunusuru huu muungano kwa wakati huu?

  vijana masikini wanaohadaiwa kwa "vijineno' vya wafadhili wa OIC watawezaje kuzinduka katika utusitusi wa akili wa namna hii?

  mbarikiwe sana

  Glory to God!
   
 7. miftaah

  miftaah Member

  #7
  May 31, 2012
  Joined: May 31, 2012
  Messages: 30
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mwacheni ayawasilishe ila ukweli utajulikana ni nani aliechoma moto kanisa na Inshaallah Mwenyezi Mungu atamdhihirisha hapa hapa duniani na wanafiki wote watajulikanwa, ila ukweli ni kua wazanzibari haturudi nyuma hadi tupate muungano wenye maslahi kwa pande zote mbili na kama kuvunjika tupo tayari mna sio faradhi huo muungano.
   
Loading...