Waziri wa Miundombinu (Zanzibar) ajiuzulu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waziri wa Miundombinu (Zanzibar) ajiuzulu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by norbit, Jul 23, 2012.

 1. norbit

  norbit JF-Expert Member

  #1
  Jul 23, 2012
  Joined: Jul 30, 2007
  Messages: 496
  Likes Received: 212
  Trophy Points: 60
  Waziri wa miundombinu na mawasiliano (Zanzibar) Hamad Masoud Hamad (CUF) amejiuzulu kufuatia ajali ya boti ya Mv Skagit.

  Nafasi yake imerithiwa Mhe. Rashid Seif Suleiman (Ziwani, CUF)


  Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano wa Zanzibar, Hamad Masoud Hamad amejiuzulu wadhifa wake leo jioni imeelezwa.

  Kwa mujibu wa taarifa ya Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Dk. Abdulhamid Yahya Mzee ilisema tayari Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk. Ali Mohammed Shein amekubali ombi la Waziri Hamad Masoud kujiuzulu.

  "Tarehe 20 Julai, 2012 Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano Mheshimiwa Hamad Masoud Hamad alimuandikia barua Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk Ali Mohammed Shein ya kumuomba ajiuzulu kufuatia ajali ya kuzama kwa meli ya Mv. Skagit iliyotokea Julai 18,2012" Ilisema taarifa ya Dk. Mzee.

  Kufuatia kujiuzulu kwa waziri huyo, Rais Dk Shein amemteua Mwakilishi wa
  Jimbo la Ziwani(CUF) Rashid Seif Suleiman kuwa Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano.

  "Kufuatia kujiuzulu kwa aliyekuwa Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano,Rais amemteua Rashid Seif Suleiman kuwa Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano" Taarifa ya Ikulu ilisema.

  Uteuzi wa Waziri mpya wa Miundombinu na Mawasiliano umeanza Julai 23 mwaka huu.

  Wakati huo huo, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk. Ali Mohammed Shein ameunda Tume ya kuchunguza ajali ya kuzama kwa meli ya Mv. Skagit.

  Mwenyekiti wa Tume hiyo ni Jaji Abdulhakim Ameir Issa, wajumbe ni Meja Jenerali S.S. Omar, COMDR. Hassan Mussa Mzee, Kapteni Abdulla Yussuf Jumbe, Kaptein Abdulla Juma Abdulla, Salum Taoufiq,Kaptein Hatibu Katandula, Bi. Mkali Fauster Ngowo, Ali Omar Chengo na Shaaban Ramadhan Abdalla Katibu wa Tume.
   

  Attached Files:

 2. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #2
  Jul 23, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,522
  Likes Received: 19,945
  Trophy Points: 280
  huo ndio ubinadamu...watanganyika igeni mfano..
   
 3. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #3
  Jul 23, 2012
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,962
  Likes Received: 1,284
  Trophy Points: 280
  haswaaaaa!
   
 4. mndwadage

  mndwadage JF-Expert Member

  #4
  Jul 23, 2012
  Joined: Jul 15, 2012
  Messages: 345
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  safi sana huo ndio uzalendo.!
   
 5. Omutwale

  Omutwale JF-Expert Member

  #5
  Jul 23, 2012
  Joined: Feb 4, 2008
  Messages: 1,429
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  That was obvious kwa mtu aliyemuelewa vema Prof. Lipumba alichosema siku alipokutana na waandishi wa habari. Kudoz kwa CUF...mmeonyesha uwajibikaji
   
 6. Puppy

  Puppy JF-Expert Member

  #6
  Jul 23, 2012
  Joined: Oct 6, 2011
  Messages: 2,280
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  huo ndo uongozi
   
 7. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #7
  Jul 23, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  hahahahaha....jiulize huyu kwanini hakufanya hivyo awali yaani ajari ya mwezi wa 9.
   
 8. Jungumawe

  Jungumawe JF-Expert Member

  #8
  Jul 23, 2012
  Joined: May 2, 2009
  Messages: 246
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Inaonekana kweli ameumia sana kwa kuwajibika labda yeye siyo gamba hebu fuatilieni zaidi
   
 9. S

  Sessy Senior Member

  #9
  Jul 23, 2012
  Joined: Jun 16, 2012
  Messages: 118
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  huo ndio uwajibikaji hongera sana kwa mauzi haya
   
 10. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #10
  Jul 23, 2012
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Mh ......mie hapa sitii neno manake hawa bana !.....mbona hakujiuzulu kwenye ile ajali ya mwanzo?
   
 11. gody

  gody JF-Expert Member

  #11
  Jul 23, 2012
  Joined: Apr 16, 2010
  Messages: 1,227
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145


  hakiyanan naagiza kuku ngoja nifuatlie vizur
   
 12. r

  raymg JF-Expert Member

  #12
  Jul 23, 2012
  Joined: Jun 30, 2012
  Messages: 845
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  source
   
 13. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #13
  Jul 23, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Hussein Mwinyi una masikio? Roho za Wanambagala na WanagongolaMboto zinakulilia.
  Nampongeza sana huyu Waziri. Wazanzibari sometimes ni waungwana!
   
 14. a

  andrews JF-Expert Member

  #14
  Jul 23, 2012
  Joined: Mar 28, 2012
  Messages: 1,680
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  ​hatuna shida na wazanzibari tatizi ni mifisadi yetu ya bara hii ina roho za kishetani
   
 15. KALYOVATIPI

  KALYOVATIPI JF-Expert Member

  #15
  Jul 23, 2012
  Joined: Aug 11, 2011
  Messages: 1,419
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 0
  Alikuwa anasubiri uongo wao utimizwe
   
 16. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #16
  Jul 23, 2012
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  lakini sio yeye ndiye aliyesababisha ajari iweje aondoke?
   
 17. k

  kimeloki JF-Expert Member

  #17
  Jul 23, 2012
  Joined: Jul 9, 2012
  Messages: 1,932
  Likes Received: 957
  Trophy Points: 280
  ameonesha kuguswa ingawaje kachelewa
   
 18. Nyetk

  Nyetk JF-Expert Member

  #18
  Jul 23, 2012
  Joined: Feb 28, 2012
  Messages: 1,624
  Likes Received: 819
  Trophy Points: 280
  Bi kiroboto anasubiri nini? Maana meli yake ishazama siku nyingi.
   
 19. a

  abu alfauzaan Member

  #19
  Jul 23, 2012
  Joined: May 19, 2012
  Messages: 61
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kufuatia ajal ya meli,mv skagt
  waziri mwenye dhamana ya uchukuzi na miundombinu mh Hamad masoud ajiuzulu wadhifa wake wa uwaziri
   
 20. simplemind

  simplemind JF-Expert Member

  #20
  Jul 23, 2012
  Joined: Apr 10, 2009
  Messages: 11,813
  Likes Received: 2,586
  Trophy Points: 280
  Better late than never.
   
Loading...