Waziri wa Mifugo na Uvuvi, unakubali vipi nchi kuingiza pesa kidogo hivi na kisha kujisifia?

Koryo2

JF-Expert Member
Nov 28, 2016
2,056
2,515
Katika taarifa ya jana ya saa mbili kupitia runinga nilimshuhudia Mhe. Waziri wa Mifugo na Uvuvi akihabarisha umma kuwa tumepata meli itakayopeperusha bendera ya Tanzania na akatamba kuwa kwa mwaka tutakuwa tukipata $400,000 na samaki tani 500 na mengineyo mengi.

Binafsi ninamshangaa sana Mhe. Waziri. Tanzania ni nchi kubwa yenye sqm 943,000. Naona nchi kama Tanzania kupata Tshs.900,000,000 kwa mwaka naona ni kiasi kidogo sana (kwa kiingereza ni peanuts).

Huo mkataba ulifanyiwa utafiti gani na nchi kuja kuambulia fedha kidogo kama ilivyotamka na Mhe. Waziri? Afadhali angetamka kuwa nchi ingepata $5millioni hapo ningemuelewa.

Nimesikitika sana kwa tamko la Mhe. Waziri wakati samaki wanaoitwa jodari watavuliwa mwaka mzima na thamani yao ni kubwa sana.
 
Back
Top Bottom