Ndebile
JF-Expert Member
- Sep 14, 2011
- 7,237
- 9,871
Nipo hapa Igombe wilaya ya Ilemela jijini Mwanza kwa mwenyeji wangu ambapo nimekaa siku tatu sasa. Nimeshuhudia uvuvi haramu wa kutumia kokolo kwa kasi ya kutisha, yaani juhudi zote zilizokuwa zimefanyika kutokomeza hii hali na hali ya upatikanaji wa samaki kuwa wa kulidhisha sasa zimepotea.
Maeneo vinala wa uvuvi huu ni fukwe za Mhonze, Kayenze Ndogo hadi na maeneo yote jirani. Huitaji kuwa mtaalam sana ili kuona hali hii, pikipiki maarufu kama bodaboda zinaanza kupakia samaki magunia kwa magunia kuanzia saa kumi alfajiri kuelekea mjini kati hadi saa mbili asubuhi jambo ambalo linatufanya tujiulize kama hao watu hawaonwi na maafisa mali asili au ndio kufa kufaana.
Hapa sio lazima Rais akemee, Waziri na watu wako njoo muone kwa macho yenu huu uharibifu wa mali asili ya Watanzania.
Nipo njiani kulekea kwangu N'gwashilalage, Kwimba- MWANZA.