Waziri wa Mawasiliano tunaibiwa na kampuni za simu za mkononi!!

mmaroroi

JF-Expert Member
May 8, 2008
2,960
544
Jamani mimi binafsi kuna wizi ninafanyiwa na kampuni za simu za mkononi ambalo nimeona nikilileta JF litawafikia wahusika. Hili tatizo wenzangu mtasema kama na nyie linawapata. Ni hivi kati line ya VODA mara unatumiwa kuwa umekatwa sh: 300 kwa ajili ya wimbo wa swagga wakati hujawahi kuomba nyimbo hizo au kubonyeza nyota kama wanavyoelekeza kama unahitaji nyimbo. Mimi naweka credit kwenye simu ili niwasiliane sasa inapokatwa kwa ajili ya nyimbo ni wizi kwani zijaziomba. Ukiwafuta VODA wanaiondoa halafu wanakuambia ni system yenyewe ndio inakuunganisha, sasa huu wizi hadi lini?

Katika line ya TIGO wanakuambia umetozwa sh: 300 kwa huduma ya TIGO beatz, kwa ajili ya mwito wako wa akupigiae wakati hujaomba kwani bila nyimbo hizo naweza kuwasiliana kama kawaida, kama nataka nyimbo nitanunua CD zake au kuzirekodi nyimbo ninazoziitaji na kwa kukatwa credit niliyoiweka ili niwasiliane.

Jamani mimi naomba msaada wenu maana nimechoka kuibiwa hadi naogopa kuweka fedha kwenye simu maana nikeweka ninataka kuwasiliana imekatwa kwa nyimbo au huduma ambayo sijaiomba. Nawasilisha, asanteni kwa kunisikiliza.
 
pole, unachosema ni kweli hawa ni wezi hata TCRA mara nyingi wanawalinda kwani hakuna wasichokijua maana hata wao ni watumiaji wa mitandao hiyo

kama unakumbukumbu za fedha zote ulizokatwa kwa huduma ambazo hukumba nenda na simu yake kwenye ofisi za VODA na TIGO pale mlimani city uwaeleze kuwa wakurudishie fedha yako waliyokukata kawani hukuomba huduma hizo. pili omba waondoe huduma zote za TIGO/VODA katika laini zako(wakutoe katika huduma zao). baada ya hapo usumbufu utapungua

mbona hujaongelea kutumiwa simu kadi yako kama billboard/ubao wa matangazo kwa wanaokupigia. waambie wakutoe unachotaka kusikia kama namba unayoipiga haipo hewani wakuambie namba hiyo haipatikani sio kukuletea miziki na matangazo ambayo ww hukuiomba

nakutakia mafanikio
 
Back
Top Bottom