Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Ndugulile afungua mkutano wa 41 wa Sourthern Africa Telecom Association(SATA) wa nchi za SADC

JUMA JUMA

JF-Expert Member
Jan 5, 2013
658
821
Waziri wa Mawasiliano Teknolojia na habari Dkt. Faustine Ndugulile amefungua Mkutano wa 41 wa mashirika na makampuni ya mawasiliano katika nchi za Ukanda wa Kusini mwa Afrika (SADC) unaojulikana kama Sourthern Africa Telecom Association (SATA) ambapo nchi ya Tanzania kupitia Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) imekuwa mwenyekiti wa Umoja huo.

Akifungua kikao hicho kilichofanyika kwa njia ya mtandao jijini Dodoma ambapo nchi 23 za umoja huo zimeshiriki Dkt. Ndugulile amezungumzia fursa mbalimbali zinazopatikana kutokana na kukua kwa teknolojia ya habari na mawasiliano hasa matumizi ya intaneti kuwa yanawezesha kufanyika kwa shughuli za biashara, uchumi na maendeleo kwa ujumla.

Aidha, amesema kuwa ni vema elimu ya matumizi sahihi ya mtandao iendelee kutolewa ili kupunguza uhalifu wa mitandaoni na mmomonyoko wa maadili kulingana na tamaduni zetu za kiafrika ambao kwa namna moja ama nyingine unasababishwa na kukua kwa matumizi ya intaneti.



IMG-20210427-WA0085.jpg




IMG-20210427-WA0089.jpg
 
Bichwa pembenne kiboko yake Vodacom, wamegoma kushusha bei ya vifurushi
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom