Waziri wa Mawasiliano, Dkt. Faustine Ndugulile atembelea Maonesho ya Kitaifa ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu

PendoLyimo

JF-Expert Member
Sep 30, 2014
878
955
DKT. NDUGULILE ATEMBELEA MAONESHO YA MAKISATU.

Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt. Faustine Ndugulile ametembelea mabanda ya wabunifu mbalimbali kwenye Mashindano ya Kitaifa ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu (MAKISATU) yanayoendelea kufanyika katika viwanja vya Jamhuri jijini Dodoma yaliyoandaliwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.

Akizungumza mara baada ya kutembelea mabanda ya wabunifu hao Dkt. Ndugulile ameipongeza Wizara ya elimu, sayansi na teknolojia kwa kubuni mashindano ya MAKISATU ambayo yanasaidia kuvumbua vipaji na ubunifu uliopo ndani ya nchi

"Nimeona ubunifu mwingi katika maonesho haya na nimefurahishwa na ubunifu wa vijana wadogo, wengine wapo shule za msingi ambao wamekuja na majibu ya changamoto ambazo tunazo kwenye jamii", alisema Dkt. Ndugulile

Aliongeza kuwa Wizara yake inafanya kazi kwa karibu sana na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na lengo la kwenda katika maonesho hayo ni kuangalia ubunifu uliopo ili kujipanga katika maonesho ya mwakani Wizara yake wasishiriki kama waalikwa bali Wizara hizo mbili zishirikiane kufanya maandalizi pamoja na ushiriki yakinifu.

Dkt. Ndugulile amezungumzia masuala ya ubunifu kama kipengele ambacho Wizara anayoisimamia inahusika moja kwa moja hasa kipengele cha ubunifu katika TEHAMA, na kuahidi kushirikiana na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ili katika maeneo ambayo Wizara yake ina ushiriki waweze kuyatafutia ufumbuzi.

Aidha, Dkt. Ndugulile amesema kuwa ni muda muafaka wa kuangalia suala la ubunifu katika mtazamo mpya kama nchi kwa kuwajengea uwezo vijana wabunifu waweze kutengeneza bidhaa na kuwatafutia masoko ili wauze bidhaa au kampuni walizozitengeneza na kwenda kufanya ubunifu mwingine mpya ili kuendelea kupiga hatua kama Taifa
 
Hongera zake huyu kajitengeneza trekta lake hakusubiri cha TBS wala TRA analitumia kwa shughuli zake kijijini

TBC acheni porojo kiongozi anapotembea mabanda kamera elekezeni hapo ili na sisi watazamaji tuone hicho kilichogunduliwa na tusikie maelezo ya wagunduzi

Waziri mkuu akiwa anatembelea mabanda kamera zenu hazikuwa pale anapotembelea mkabaki mnatupigia porojo tu kuwa ohh sasa anatoka banda hili kwenda lile .Maana ya mbashara ni nini? kuwasilikilizeni nyie au kutuonyesha matukio yenyewe husika?
 
NDUGULILE AMEJIFUNZA :-
1. Kufungia tweeter.
2.Kufungia fb.
3. Kuufungia insta na magazet.

Mtaniambia.
 
TBC acheni porojo kiongozi anapotembea mabanda kamera elekezeni hapo ili na sisi watazamaji tuone hicho kilichogunduliwa na tusikie maelezo ya wagunduzi

Waziri mkuu akiwa anatembelea mabanda kamera zenu hazikuwa pale anapotembelea mkabaki mnatupigia porojo tu kuwa ohh sasa anatoka banda hili kwenda lile .Maana ya mbashara ni nini? kuwasilikilizeni nyie au kutuonyesha matukio yenyewe husika?
MEDIA nyingi tanzania hawajikiti kwenye kuwafatilia watu wanaounda vifaa au kufa gunduzi,wao wame base kwenye kufatilia
Ujinga ujinga tu

Ova
 
TBC acheni porojo kiongozi anapotembea mabanda kamera elekezeni hapo ili na sisi watazamaji tuone hicho kilichogunduliwa na tusikie maelezo ya wagunduzi

Waziri mkuu akiwa anatembelea mabanda kamera zenu hazikuwa pale anapotembelea mkabaki mnatupigia porojo tu kuwa ohh sasa anatoka banda hili kwenda lile .Maana ya mbashara ni nini? kuwasilikilizeni nyie au kutuonyesha matukio yenyewe husika?
Ndicho kilichokuwa kinatokea Dodoma, media zinafuata wanasiasa badala ya ugunduzi husika.
 
Back
Top Bottom