Waziri wa Mambo ya Nje wa Finland, Timo Soini ameipongeza serikali ya Tanzania

britanicca

JF-Expert Member
May 20, 2015
15,636
30,004
FINLAND WAIPONGEZA TANZANIA KUFANIKISHA VITA DHIDI YA RUSHWA: Waziri wa Mambo ya Nje wa Finland, Timo Soini ameipongeza serikali ya Tanzania kwa kuendeleza na kufanikisha mapambano dhidi ya rushwa.

Balozi huyo ametoa kauli hiyo alipokutana na kumkaribisha ofisini kwake Waziri mwenza wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki nchini Tanzania, Dkt. Augustine Mahiga pamoja na ujumbe wake ambao wako nchini humo kwa ziara ya kikazi ya siku mbili.

FB_IMG_1551198691040.jpg
FB_IMG_1551198687209.jpg

Source:Azam media
 
Vizuri sana, hapa CHADEMA wanaumia
Kama mambo ni shwari kwa nini misaada imekatwa. Hiyo ni diplomacy ya kumkaribisha mgeni akija kwako. Yanayoendelea ndani ni mnyukano wa kidiplomasia, fanyeni hivi hapa ,fanyeni hivi pale. Wabongo wakikubali misaada inarudi. Vinginevyo hapa ni kujifurahisha tu, lakini wenye akili hawadanganyiki na hizo sifa huku unaminywa misaada. Una habari Tz inakaribia kusaini mkataba wa umoja wa ulaya ili bidhaa zao ziingie bila kodi. Wazungu ni mashetani wakitaka kitu kwako watakipata na ukiwanyima watachukua kwa nguvu. Hatuna misuli ya kupambana nao kiuchumi wewe tulia ndani ya mwaka utaona ulichopinga leo utakishangilia, bila aibu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Serikali hii imejaa rushwa tupu kuanzia vituo vya police na sehemu nyingine za Dola huyo yupo ulaya hajui kinachoendelea aache ushoga wake

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuki kwa nguruwe kwa binadamu mchungu; yale anayosemaga lissu ulaya tumasemaga anapaka rangi na hao wazungu wasimuamini maana hawapo huku ila mnakomaaga kuwa wanajua kila kitu licha ya wako huko, kulikoni leo mwataka kuamisha magoli?
 
Kama mambo ni shwari kwa nini misaada imekatwa. Hiyo ni diplomacy ya kumkaribisha mgeni akija kwako. Yanayoendelea ndani ni mnyukano wa kidiplomasia, fanyeni hivi hapa ,fanyeni hivi pale. Wabongo wakikubali misaada inarudi. Vinginevyo hapa ni kujifurahisha tu, lakini wenye akili hawadanganyiki na hizo sifa huku unaminywa misaada. Una habari Tz inakaribia kusaini mkataba wa umoja wa ulaya ili bidhaa zao ziingie bila kodi. Wazungu ni mashetani wakitaka kitu kwako watakipata na ukiwanyima watachukua kwa nguvu. Hatuna misuli ya kupambana nao kiuchumi wewe tulia ndani ya mwaka utaona ulichopinga leo utakishangilia, bila aibu

Sent using Jamii Forums mobile app
Misaada umeikata wewe au nani kaikata?
 
Huko lumumba mtaendelea jazana ujinga...

Ila ukweli utaendelea kusemwa, awamu hii kuna rushwa za kutosha nahisi ndio awamu iliyovunja rekodi kwa utoaji rushwa...

Sio walinzi sio migambo rushwa njenje...
 
FINLAND WAIPONGEZA TANZANIA KUFANIKISHA VITA DHIDI YA RUSHWA: Waziri wa Mambo ya Nje wa Finland, Timo Soini ameipongeza serikali ya Tanzania kwa kuendeleza na kufanikisha mapambano dhidi ya rushwa.

Balozi huyo ametoa kauli hiyo alipokutana na kumkaribisha ofisini kwake Waziri mwenza wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki nchini Tanzania, Dkt. Augustine Mahiga pamoja na ujumbe wake ambao wako nchini humo kwa ziara ya kikazi ya siku mbili.

View attachment 1032780View attachment 1032781

Source:Azam media
Tundu lissu akiongea nao, anasupport ushoga. Ila mahiga akiongea nao ni wadau wa maendeleo
 
Misaada umeikata wewe au nani kaikata?
Unataka kumbishia waziri wa fedha mwezijana alikri kuwa wahisani wamepunguza misaada ya maendeleo. Umependa chongo unaita kengeza. Mimi naomba MUNGU atupe uhai tuone jinsi SGR train na STIEGLER'S GORGE umeme itakayokamilika.Leo mwaka wa tatu hata kilomita 200 haijafika je km 1250 hadi Mwanza tutaweza kweli.? Na Kule Stiegler hata misitu haijafyekwa. Au unadhani kusaini mkataba ndio umetekeleza mradi. Kwa kweli kabisa hamna MTU rohoni mwake anapenda serikali yake ishindwe jambo jema LA mendeleo . lakini baba akisema wanangu nitawanunulia gari na wewe ni MTU mzima unajua pato LA familia ni dogo. Ukimwambia mzee ahirisha hill ili wadogo wasome na kupata tiba wakugua, utakuwa umemkosea adabu. Au siku hizi tunaongizwa na malaika wanaotoa maelekezo mbinguni na hawawezi kukosea . Namheshimu Rais kwa maamuzi ya uthubutu lakini nisingependa tuishi maisha ya kipindi cha baba wa taifa maana ndege zilikuwepo na viwanda vilikuwepo lakini shida za mifuko kutoboka hazikupendeza RAIA. Nia njema haileti matokeo chanya bila umakini katika kutekeleza. Mipango si matumizi na waingereza wana msemo kuwa If wishes were horses fools could ride. Tupange yanayotekelezeka vinginevyo tutaishia kupeana kashfa , Mara huyu si mzalendo, mara huyu si RAIA . Lakini mwenydzi MUNGU katupa vichwa kila MTU na chake kwa hiyo kutofautiana kifikra ni jambo LA kiafya .. Hatujaambiwa kuwa simameni kufikiri na Fulani au kundi Fulani watafikiri kwa niaba yenu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huwa sielewi wanaposema mafanikio dhidi ya rushwa, labda kwa sababu neno rushwa lina pana, mie naona mafanikio kama yapo ni madogo sana
 
Back
Top Bottom