WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amepiga marufuku tabia ya baadhi ya askari Polisi nchini kukamata waendesha pikipiki (bodaboda) wakiwa

esther mashiker

JF-Expert Member
May 29, 2018
616
552
lugola+pic.jpg



WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amepiga marufuku tabia ya baadhi ya askari Polisi nchini kukamata waendesha pikipiki (bodaboda) wakiwa hawana sare za jeshi.

Akizungumza na mamia ya wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Uwanja wa Uhuru maarufu Mayunga mjini Bukoba mkoani Kagera jana, Lugola alisema polisi wanapaswa kufuata utaratibu wa kijeshi hasa wanapokamata vyombo vya moto na siyo kuvunja utaratibu.

Lugola aliongeza kuwa bodaboda zinazovunja sheria za usalama barabarani zinapaswa kukamatwa bila kuwaonea huruma, ila ni kosa Polisi kuwanyanyasa vijana hao ambao wanapata riziki kupitia biashara hiyo. “Mnapaswa kukamata hizi bodaboda zinapofanya makosa, tabia ya kukurupuka huku mkitafuta fedha zisizo halali, huko ni kuwaonea waendesha bodaboda,” alisema Lugola.

Pia aliwataka waendesha bodaboda mjini Bukoba na Tanzania kwa ujumla wafuate sheria za usalama barabarani zikiwemo kuvaa koa ngumu, kutokubeba abiria zaidi ya mmoja na pia wakiendesha wanapaswa kuwasha taa. Lugola ameanza ziara ya siku nane mkoani humo akitembelea wilaya zote, akisikiliza kero za wananchi pamoja na kufuatilia maagizo yake aliyoyatoa kwa vyombo vya ulinzi na usalama vilivyopo ndani ya wizara yake.

Mwaka jana, alitoa maagizo kwa makamanda wa mikoa nchini kuwa dhamana zitolewe saa 24 katika vituo vyote vya polisi nchini, na pia kupiga marufuku tabia ya baadhi ya Polisi kubambikizia kesi wananchi, na pamoja na agizo la pikipiki zote zilizopo vituoni ziondolewe. Lugola tayari amemaliza ziara yake kwa Wilaya ya Bukoba na leo ataanza ziara Wilaya za Missenyi baadaye Karagwe, Kyerwa, Ngara, Biharamulo na Januari 8, mwaka huu atamalizia ziara yake Wilaya ya Muleba.

Katika wilaya hizo, pia atazungumza na wananchi pamoja na watumishi waliopo ndani ya wizara yake ambao ni Jeshi la Polisi, Idara ya Uhamiaji, Jeshi la Magereza, Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, pamoja na Idara ya Probesheni. Idara ya Probesheni jukumu lake kuu ni kupunguza msongamano gerezani na kusimamia wafungwa waliopewa adhabu mbadala na mahakama au wafungwa waliopata msamaha kupitia sheria ya huduma kwa jamii na kutumikia kifungo chao nje ya gereza
 
Huyu sasa ndo yule Kangi tuliyemkubali enzi zile akiwa ninja bungeni.
 
Back
Top Bottom