Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba: Naagiza aliyemtolea bastola Nape Nnauye, achukuliwe hatua

Feb 25, 2012
419
2,168
IMG_4534.JPG

Mwigulu Nchemba(Kushoto) akizungumza na Nape Nnauye katika ukumbi wa NEC kabla ya kuanza kwa kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM mjini Dodoma 10/15/2014(Maktaba)

Mh. Nape Moses Nnauye sio jambazi, ni mtanzania, ni mbunge, mjumbe wa NEC wa CCM, hana record ya uhalifu. Kitendo cha mtu kumtolea Bastola, Sio cha kiasikari, sio cha kitanzania na sio cha ki Mungu, kama mtu ameweza kutoa Bastola mbele ya Kamera nawaza mbali ingekuwa kwenye uchochoro angefanya nini.

Nahusika na Usalama wa Raia wote wa Tanzania, nimemwelekeza IGP atumie picha kumsaka mtu yule aliyeinua kufanya kitu cha kihalifu kwa kofia ya uaskari. Na kama ni Askari basi sheria zinazoongoza taasisi husika zichukue mkondo wake.
======

Mwigulu.PNG
 
Hujui Mtoto wa Baba katoa instruction,na yeye anafuata Mkondo wa Maji sasa hivi.Alichelewa kwenye Clouds,hakuwaona kama Clouds ni Watanzania??Je hakuwaona kama Lissu,Lema na wapinzani wengine wakishikiwa Bunduki na Polisi kama kumi hivi,duh,Mwigulu acha double standard anza upya
 
Mwigulu kama mzalendo awe committed katika hili, akisakwa so what? ni lazima abanwe aseme nani alimtuma na kwa sababu gani. Huyo aliyemtuma naye awekwe wazi wananchi tumjue. Kama atafanikiwa hivi nina uhakika nae siku zake zitakua zinahesabika maana Mtukufu hataki kupingwa
 
Kwanza mh Nchemba uwe tayari kutumbuliwa maana umebaki wewe na January.Vile vile lazima ujue kua askari wanafanya kazi kibashitebashite hakuna weledi hapo.Huyo askari ametumwa na Daud usimuonee na kama una uchungu sana na upo tayari kutumbuliwa mshughulikie aliyemtuma ndg Daud
 
Back
Top Bottom