Waziri wa Mambo ya Ndani Dk Nchimbi Atua Zenj, Akemea Vitendo vya Vurugu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waziri wa Mambo ya Ndani Dk Nchimbi Atua Zenj, Akemea Vitendo vya Vurugu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kakke, May 28, 2012.

 1. Kakke

  Kakke JF-Expert Member

  #1
  May 28, 2012
  Joined: Dec 4, 2010
  Messages: 1,797
  Likes Received: 389
  Trophy Points: 180
  [h=3]Waziri wa Mambo ya Ndani Dk Nchimbi Atua Zenj, Akemea Vitendo vya Vurugu[/h]

  [​IMG]
  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi


  [h=2][/h][h=3][/h]
  Na Juma Mohammed,MAELEZO Zanzibar


  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi ametua Visiwani Zanzibar leo ambapo amekemea vitendo vya vurugu,akiahidi Serikali kuwachukulia hatua ikibidi hata kuwavizia nje ya misikiti kwa wale watakaohusika na uvunjifu wa amani .


  Waziri Nchi aliwasili Mjini Zanzibar akiwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi,Inspekta Jenerali Said Mwema kwa pamoja waliitisha mkutano uliowakutanisha viongozi wa Jumuiya ya Maimamu Zanzibar(JUMAZA),Mabalozi,Kamisheni ya Utalii, Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislam Zanzibar(JUMIKI).


  “Suala la kufuata sheria halina mjadala,lazima kila mmoja wetu afuate na kutii sheria hatutawavumilia watakaovuruga amani ya nchi…maandamano yoyote lazima yapate kibali” Aliwaambia wadau katika mkutano huo uliofanyika Makao Makuu ya Polisi Zanzibar,Ziwani.


  Waziri Nchi alisema busara ya Polisi imefikia kikomo na kwamba atashangaa sana akiona busara hiyo ikiendelea wakati kuna watu au kikundi kinavunja amani ya nchi.


  “Tutashangaa busara ya Polisi ikiendelea wakati watu wanaumia kwa watu wengine kuvunja amani…hatutakubali, tutaendelea kuviziana hata nje ya misikiti tutawakamata” Alisisitiza Waziri Nchi.


  Waziri huyo alisema kila mtu anawajibika kitunza amani iliyopo ambapo pia alisema Serikali ya Mapinduzi Zanzibar yenye mfumo wa Umoja wa Kitaifa imefanyakazi nzuri katika kipindi kifupi na kuwapongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk. Ali Mohammed Shein, Makamu wa Kwanza wa Rais Maalim Seif Shariff Hamad na Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Idd.


  “Jamani Serikali ya Umoja wa Kitaifa inatufanyia kazi nzuri kwanini mnataka kuwachafua viongozi wetu,lazima mfuate sheria hakuna mbadala wa hilo kwani dini zote zinahimiza amani,umoja na mshikamano.


  Alisema Serikali inataka utulivu ndani ya mioyo ya watu na sio utulivu huo usiishie kuonekana barabarani tu, “watu waishi bila hofu kwa utulivu kabisa huku mioyo yao ikiwa imetulia” Aliongeza Dk. Nchimbi.


  Alitoa wito kwa viongozi wa dini, vyama vya siasa na wananchi kwa ujumla kuwafichua wahalifu wote waliohusika na matukio ya wizi,uporaji wa mali na uharibifu wa vitu na mali mbalimbali wakati wa matukio ya wiki iliyopita.


  “Wananchi wafichueni wahalifu ,tusichanganye uislamu na uhalifu” alisisitiza Waziri Nchi katika mkutano huo ambapo viongozi wa dini waliahidi kuchukua hatua kusambaza ujumbe wa Waziri huyo kwa waumini na wananchi wengine kutunza amani na kujieepusha na vurugu.


  Katibu wa JUMAZA,Sheikh Muhidin Zubeir Muhidin alisema Jumuiya yake ni tofauti na Jumuiya ya Uamsho hivyo watu wasizichanganye. Alisema Maimamu wataelezana ulazima wa kuwaeleza waumini kufuata na kuzitii sheria sio tu za Mwenyezimungu bali hata za Serikali.

  Katika mkutano huo kulikuwa na wawakilishi wa Balozi za Marekani, Canada, Uingereza na Norway.
   
 2. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #2
  May 28, 2012
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  MAWAZO YA UBORESHAJI WA MUUNDO NA UTENDAJI WA 'MUUNGANO' WETU KWA MAWAZO YA MASHINANI NDIO NJIA SAHIHI TOFAUTI NA HAPO HAKIVUNJWI KITU HAPA!!

  Ladies and Gentlemen, do read this out very clearly both in public and in silence:

  Muungano is here to stay, the only options we have is to find ways to improve the administrative structures and operational efficiency and effectiveness for it to continue benefiting us the most.

  Narudia hapa; Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni KUBORESHWA KWA MISINGI YA MAWAZO HURU YA WANANCHI WA KAWAIDA MASHINANI na kamwe wazo la kulivunja halina nafasi.
   
 3. F

  FJM JF-Expert Member

  #3
  May 28, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145

  Hivi Tanzania hatuwezi kufanya kazi bila kusimamiwa na watu wa nje? Wawikilishi wa hizo nchi wanafanya nini kwenye mkutano wa waziri wa nchi na wadau wa ndani? Au tuamini kwamba serikali imelazimishwa kuchukuwa hatua na mataifa ya nje? Hebu tufanye mambo kama taifa huru.
   
 4. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #4
  May 28, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Nchimbi naona naye anakwepa kiini cha tatizo; ni kushindwa kwa serikali yake na yeye mwenyewe kusimama kuutetea Muungano!!! It IS THAT SIMPLE!
   
 5. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #5
  May 28, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 549
  Trophy Points: 280
  Kwa nini mmetumia picha inayomuonyesha akicheka katikati ya msiba na hofu (torror) kubwa namna hii nchini? au kwa sababu mnajua hakuna jipya anapeleka huko??
   
 6. Wingu

  Wingu JF-Expert Member

  #6
  May 28, 2012
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 4,326
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Sasa hao mabalozi wahizo nchi wanafuata nini hapo hawa ndo wazushi wenyewe.
   
 7. myhem

  myhem JF-Expert Member

  #7
  May 28, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 932
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  nadhani Jusa anatakiwa awe mshtakiwa namba moja kabisa maana ndiye mwanzilishi wa yote yanayokea huko zenji.
   
 8. Kakke

  Kakke JF-Expert Member

  #8
  May 28, 2012
  Joined: Dec 4, 2010
  Messages: 1,797
  Likes Received: 389
  Trophy Points: 180
  Huu ndio ubakuzi unaokuja wa kidini na kutokujuwa wajibu wake Mh Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi, kwa kuhukumu watu wa dini fulani bila ushahidi kumnukuu maneno haya(hatutakubali, tutaendelea kuviziana hata nje ya misikiti tutawakamata" Alisisitiza Waziri Nchi) huyu ni mtini na si Waziri.
  kutokujuwa nyeye ni kioote na dini zote, vipi leo siku mbili tu tokea matokeo upata ushahidi kuwa lolofanya hivyo vitendo vya hujuma ni waislamu haliyakuwa hujapokea ripoti za uchunguzi na ushahidi kuwa ni wao au kulikuwa na watu wenye agenda fulani ama za kisiasa au nyingine katika uchunguzi.

  Hapa ndipo Jeshi la Polisi na viongozi wake kufeli kwa kuto kushunguwa kwanza na badae kupurushuka kuleta zana zisizo na ushahidi,OK TUMEKUSKIA ASKOFU Emmanuel Nchimbi.
   
 9. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #9
  May 28, 2012
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Wewe Ndugu usikejeli ziara ya Waziri wa Mambo ya Ndani kule Visiwani Zanzibar kwenda kujionea matukio ya hatari kiasi hiki nchini mwetu,

  hivyo nakushauri kwamba usilete mambo ya hiyana na kiayawani kwa mambo ambayo ni 'too sensitive' kama haya yanayoendelea visiwani zanzibar hivi sasa.

  If you have nothing more meaningful and nationally constructive to say; don't say it here!!!!


   
 10. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #10
  May 28, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,798
  Likes Received: 3,884
  Trophy Points: 280
  wasiwavizie nje ya misikiti! waingie hata ndani kuwaibua huko na kuwaburuza mahakamani hawawezi kujificha misikitini huku wanachoma makanisa!!
   
 11. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #11
  May 28, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,798
  Likes Received: 3,884
  Trophy Points: 280
  kuwepo au kutokuwepo muungano hakujustify in anyway kuchoma kanisa na kufanya fujo zote hizo
   
 12. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #12
  May 28, 2012
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Wazee wetu Mliotukuka kwa heshima za hiari kwenu,

  Mzee Sinde Warioba, Salim Ahmed Salim, Joseph Butiku, Mzee Ndesamburo, Kingunge Ngombale Mwiru, Dr Slaa, Mzee Mtei, Prof Shivji, Getrude Mongella, Bob Makani na wengine wengi wenye hadhi yenu;
  KUNA TATIZO TANZANIA VISIWANI tena kubwa ajabu kuliko hako ka-pua kalikojitokeza kwenye vurugu za hapo jana.

  Amkeni sasa hivi kulishughulikia KIMOJA au muendelee kusubiri kuona taifa letu likimezwa kwa kutumbukia kwenye shimo kuuubwa ajabu iloko pale Zanzibar kwa kipindi kirefu hivi sasa.
   
 13. Pharaoh

  Pharaoh JF-Expert Member

  #13
  May 28, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 843
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Habari hizo za Ugaidi Zanzibar zishaenea kote Duniani kwa Web na kote wanajua
   
 14. Pharaoh

  Pharaoh JF-Expert Member

  #14
  May 28, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 843
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Jeshi la Polisi Zanzibar limo kwenye uhalifu kwa namna fulani, hapo kikaoni wanakonyezana tu
   
 15. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #15
  May 28, 2012
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Haya sasa ...!!!!!!!!!!!!!!!!!!

   
 16. B

  Bobuk JF-Expert Member

  #16
  May 28, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 5,876
  Likes Received: 481
  Trophy Points: 180
  Kwanini uwavizie Msikitini wahalifu? Nenda uwachomoe huko huko MISIKITI. Msikiti sio VICHAKA vya kuficha wahalifu, unless kama kamusi yangu imenidanganya maana ya neno MSIKITI ni sehemu ya kuabudia waislamu. SIO Sehemu ya kuficha Wahalifu, I stand to be corrected.
   
 17. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #17
  May 28, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,197
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Sio kuingia huko Misikitini tuu hata ikiwezekana wanapata na kichapo wakiwa humo ndani
   
 18. s

  sweke34 JF-Expert Member

  #18
  May 28, 2012
  Joined: Sep 28, 2010
  Messages: 2,533
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  sentence ya mwisho imenifurahisha sana...unaweza kuwa huru wakati bado ni tegemezi?
   
 19. M

  Mkekuu JF-Expert Member

  #19
  May 28, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 1,239
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Kama mwezi na nusu umepita toka jeshi la police liingie kanisani kuvunja ibada kwa kile kilichoitwa kufuata wahalifu pale dar,sasa vp wahalifu wakubwa wenyekutishia amani ya nchi wasubiriwe nje ya misikiti.HII SI SAWA KABISA KAMA NI WAHALIFU WAFUATWE,misikiti ni mahali pa ibada si pango la wahuni,NCHIMBI KACHAMKA SN,AU NA YEYE BWABWA?.
   
 20. U

  Unstoppable JF-Expert Member

  #20
  May 28, 2012
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 1,049
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Inawezekana serikali imelazimishwa kuchukua hatua; inawezekana pia Muungano una support ya hayo mataifa (Marekani, Canada, Norway & co) wakati kikundi cha Uamsho kina-support kutoka Arab countries (kama tetesi hizo ni kweli). That being said; Wanaotaka Muungano na wasioutaka wote watakuwa wana-back up ya mataifa makubwa... mh you can see now where this is heading. Hili swala linaweza kuwa ni complicated kuliko tunavyodhani. Hivi ni kwanini serikali inashindwa kuweka hoja wazi kwanini Muungani ni muhimu uwepo?
   
Loading...