Waziri wa Mambo ya Ndani, Charles Kitwanga atenguliwa Uwaziri baada ya kuingia Bungeni akiwa amelewa

Ni daktari au mkemia gani amethibitisha bila kutia shaka yakwamba Kitwanga alikuwa amelewa?
Wewe unapolewa na kurudi home ukiyumba barabarani, na wanao kukushangaa na majirani kujiuliza maswali huwa umepimwa na mkemia?
 
Habari nilioipata usiku huu ni kua rais magufuli ametengua uwaziri wa charles kitwanga kwa madai aliingia bungeni na kujibu maswali huku akiwa amelewa
Mliokua bungeni mtuambie ni swali gani aliulizwa akajibu huku kumbe alikua amelewa mpaka rais akatengua cheo chake cha uwaziri

Source bay breaking news usiku huu radio one
 
Habari za hivi punde zinasema Rais Magufuli amemfuta kazi Waziri wa Mambo ya Ndani, Charles Kitwanga.

Sababu kubwa ni kuwa Waziri Kitwanga kaingia bungeni akiwa amelewa na akaenda jibu swali akiwa amelewa..!

Source: Tbc1 Habari

======
Taarifa ya Ikulu:

======
Ofisi ya Waziri Mkuu:

20 Mei, 2016

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

WAZIRI MKUU AFAFANUA KUHUSU KUTENGULIWA KWA UTEUZI WA WAZIRI KITWANGA

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema uamuzi wa Rais Dk. John Pombe Magufuli kutengua uteuzi wa Waziri wa Mambo ya Ndani, Bw. Charles Kitwanga umefuata kanuni za utumishi wa umma ambao unakataza mtumishi kulewa akiwa kazini.

“Zipo sheria za utumishi ambazo mtumishi hatakiwi kunywa pombe na wala hapaswi kulewa akiwa kazini… mtumishi anapaswa kuwa na akili timamu inayokuwezesha kufanya kazi za Serikali,” alisema.

Ametoa ufafanuzi leo usiku (Ijumaa, Mei 20, 2016) wakati akijibu swali la mwandishi wa TBC1 aliyetaka kujua kama taarifa zilizoenea kuhusu kutenguliwa kwa Waziri huyo ni za kweli.

“Ni kweli Mheshimiwa Rais, Dk. John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa Waziri wa Mambo ya Ndani, Mheshimiwa Charles Kitwanga kuanzia leo tarehe 20 Mei, 2016 baada ya kuonekana amelewa wakati wa kazi. Na hili lilibainika pale alipokuwa akijibu maswali ya wizara yake leo asubuhi,” alisema Waziri Mkuu.

Waziri Mkuu amesema kuna swali aliloulizwa ambalo hakulijibu vizuri na kwamba swali hilo litapaswa kurudiwa kuulizwa baada ya wabunge kuomba muongozo wa swali hilo.

IMETOLEWA NA:

OFISI YA WAZIRI MKUU,

S. L. P. 980,

DODOMA.

IJUMAA, MEI 20, 2016

CCM Wanataka tusijadili swala la Lugumi na badala yake tumjadili Kitwanga.
Wakati EPA imepamba moto, tukaletewa Babu Wa Loliondo.

Escrow ikiwa kwenye pick, mfalme akaibuka na tezi dume.

Lugumi sasa, imemuibua Kitwanga.
Hii ni ajenda ya CCM kutuepusha kutoka kwenye mada kuu
Jamani, turudini mada kuu. Ile kamati ya kina Lusinde INAENDELEAJE na kazi yake? Siku 30 za kazi zinakaribia kwwisha. Sijui wataona mashine zimefungwa sehemu zote 104?
 
tayari ndio uchunguzi umeharibika, unadhani kitwanga atawasaidiaje sasa na nyumbani kwake hamna hata waraka mmoja Wa lugumi?
 
======
Taarifa ya Ikulu:

======
Ofisi ya Waziri Mkuu:

20 Mei, 2016

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

WAZIRI MKUU AFAFANUA KUHUSU KUTENGULIWA KWA UTEUZI WA WAZIRI KITWANGA

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema uamuzi wa Rais Dk. John Pombe Magufuli kutengua uteuzi wa Waziri wa Mambo ya Ndani, Bw. Charles Kitwanga umefuata kanuni za utumishi wa umma ambao unakataza mtumishi kulewa akiwa kazini.

“Zipo sheria za utumishi ambazo mtumishi hatakiwi kunywa pombe na wala hapaswi kulewa akiwa kazini… mtumishi anapaswa kuwa na akili timamu inayokuwezesha kufanya kazi za Serikali,” alisema.

IMETOLEWA NA:

OFISI YA WAZIRI MKUU,

S. L. P. 980,

DODOMA.

IJUMAA, MEI 20, 2016
Baada ya Mhe. Charles Kitwanga kuliambia Bunge jana kuwa hakuwahi kuingia Bungeni akiwa amelewa, nafanya mapitio kidogo ya taarifa hizi.

Mtu kuonekana amelewa na kuwa kweli umelewa ni vitu viwili tofauti. Japo ni kweli Waziri Kitwanga alionekana kama amelewa, kwa nini rais alichukua maamuzi ya haraka ya kumtumbua, bila kumpima kuthibitisha amelewa pombe?.

Mamlaka ya rais kuteua na kutimua is at presidents pleasures, rais anaweza kukuteua for a reason or no reason at all, the same applies kwenye ku fire, anaweza kukutengua wakati wowote, with reasons or no reason at all, na bado rais akawa right na uamuzi huo haupaswi kuhojiwa na mamlaka nyingine yoyote hata Kitwanga mwenyewe, lakini kwa nini taarifa ya Ikulu ilisema ametenguliwa kwa ulevi bila kupimwa na kuthibitisha ni ulevi wa pombe?!

Taarifa ya Ikulu si ingeweza kueleza tuu rais ametengua uteuzi wa Kitwanga na kuishia hapo bila kumuiabisha kwa kueleza sababu?. Wangapi wanatumbuliwa bila sababu kuandikwa?.

Taarifa ya Waziri Mkuu imefafanua vizuri, Mtumishi wa umma hapaswi kunywa pombe, au kuonekana amelewa pombe akiwa kazini. Japo ni kweli Charles Kitwanga alionekana kama amelewa, what if ni kuonekana tuu, but in reality hakuwa amelewa, na hata kama ni kweli alikuwa amelewa, what if sio pombe bali ni dawa ya kifua, uchovu, (fatigue), ukosefu wa usingizi iliompa uchovu wa exhaustion, au sababu nyingine yoyote?.

Kama ni kweli Kitwanga hakulewa, lakini ametenguliwa kwa kuaibishwa kwa ulevi, na yeye kwa nini siku zote amekaa kimya na ndio kuja kuibuka leo?!

All and all, kama ameonewa, karma itamfidia, na walio muonea nao wana shares zao.

Pole sana Charles Kitwanga.

P
 
Nimekusoma Bwana Paskali,lakini nilivyokuelewa ni kama vile kuna kitu unakijuwa ambacho sisi hatukijui kwenye hili swala la ulevi la Mh.Lakini kumbukumbu nilizonazo (sijui kama ni sahihi)
kuna Mh mmoja alimuomba asiingie bungeni siku hiyo kwa kuwa alikuwa amelewa lakini akakataa.All in All,lets keep our fingers crossed na tumuombe Mwenyezimungu atujaalie upendo,amani na riziki halali.
 
Bro nchi yetu inaongozwa kwa double standard Wala usishangae
 
Nimekusoma Bwana Paskali,lakini nilivyokuelewa ni kama vile kuna kitu unakijuwa ambacho sisi hatukijui kwenye hili swala la ulevi la Mh.Lakini kumbukumbu nilizonazo (sijui kama ni sahihi)
kuna Mh mmoja alimuomba asiingie bungeni siku hiyo kwa kuwa alikuwa amelewa lakini akakataa.All in All,lets keep our fingers crossed na tumuombe Mwenyezimungu atujaalie upendo,amani na riziki halali.
Hakuna chochote cha ziada nikijuacho, bali kuonekana amelewa ni tofauti na kuwa umelewa. Kitwanga alionekana kama amelewa na akatumbuliwa kwa ulevi na alinyamaza kimya.

Leo anapoibuka na kusema hajawahi kuingia Bungeni akiwa amelewa, ni kama kuonyeshea ameonewa fulani, ila pia kuonyeshea Mkuu wake ni muonevu fulani. Ukionewa na mkubwa, unapaswa kuoneka na kujinyamazia tuu tena usilalamike popote.

Mimi mwenyewe yameisha nikuta mengi ya kunyanyaswa na wakubwa, inakubidi tuu unyanyasike na kujikalia kimya.
P
 
Back
Top Bottom