Waziri wa Mambo ya Ndani, Charles Kitwanga atenguliwa Uwaziri baada ya kuingia Bungeni akiwa amelewa

poa umesikika bavicha na pumba zako
kwa kuwa alimnadi kwa sifa kedekede ko asimtengue hata anapoharibu maadili ya kazi,unatuambia hata marais walopita walikuwa wanashtua una uhakika?? weka ushahid af ukumbuke hii awamu sio kama ile sawa???
yan wabongo pasua kichwa asingemchukulia hatua mngebwabwaja leo kamchukulia hatua mnaropoka hovyo...
 
Pole kwa yaliyokukuta kaka, mambo hayo yanaweza mtokea mtu yeyote. Hukuzaliwa uwe waziri na ulikuwa waziri kwa uweza na mapenzi ya mungu kupitia jk na jpm.
Nakuomba sana kipindi hiki utulize mawazo na wala usiingie malumbano na mheshimiwa. iga mfano wa ombeni sefue baada ya kutenguliwa alishukuru kupewa imani hiyo na mheshimiwa ambayo kimsingi hakulazimishwa na mtu kumpa ila kwa matakwa yake.
Japo kwa muda mfupi watu wenye busara wanasubiri kusikia sauti yako ukimshukuru raisi wa jamhuri kwa imani aliyokuwa amekupa na muahidi ushirikiano katika njia nyingine atakazoona zinafaa. ukifanya hivo historia itakukumbuka na utakuwa umeacha legacy mpaka kwa vitukuu.
interest za taifa ni kubwa kuliko interest za mtu binafsi.
pamoja daima tujenge taifa letu.
 
Kipindi hiki lazima kutakuwa na watu wanamjaza upepo..nimesikia kuna madiwani huko misungwi wanataka uthibitisho wa kisayansi kuwa alikuwa amelewa...that is not a smart/strategic move! Its not prudent! ingawa wahenga walisema "silence isn't always golden"....lakini ni ukweli pia kuwa "silence can never be misquoted"...Akae kimya, akianza kuongea kila mtu atanukuu kivyake.....
 
Pole kwa yaliyokukuta kaka, mambo hayo yanaweza mtokea mtu yeyote. Hukuzaliwa uwe waziri na ulikuwa waziri kwa uweza na mapenzi ya mungu kupitia jk na jpm.
Nakuomba sana kipindi hiki utulize mawazo na wala usiingie malumbano na mheshimiwa. iga mfano wa ombeni sefue baada ya kutenguliwa alishukuru kupewa imani hiyo na mheshimiwa ambayo kimsingi hakulazimishwa na mtu kumpa ila kwa matakwa yake.
Japo kwa muda mfupi watu wenye busara wanasubiri kusikia sauti yako ukimshukuru raisi wa jamhuri kwa imani aliyokuwa amekupa na muahidi ushirikiano katika njia nyingine atakazoona zinafaa. ukifanya hivo historia itakukumbuka na utakuwa umeacha legacy mpaka kwa vitukuu.
interest za taifa ni kubwa kuliko interest za mtu binafsi.
pamoja daima tujenge taifa letu.
Yaani walevi mna lugha ya kufarijiana hadi raha eti "pamoja tujenge taifa letu
 
poa umesikika bavicha na pumba zako
kwa kuwa alimnadi kwa sifa kedekede ko asimtengue hata anapoharibu maadili ya kazi,unatuambia hata marais walopita walikuwa wanashtua una uhakika?? weka ushahid af ukumbuke hii awamu sio kama ile sawa???
yan wabongo pasua kichwa asingemchukulia hatua mngebwabwaja leo kamchukulia hatua mnaropoka hovyo...
Natujua Kuna Mmoja Wewe na Mimi Tunamhshimu, Alikuwa anakunywa Kidogo Na Wewe au Mimi hatuwezi Kumhukumu kwani hajawahi/hawajawahi kujidhalilisha. Na pia hakufanya dhambi! Ushahidi gani, Kwani Kuna dhambi gani/ au uhaini gani walifanya? Kweli hata Ukikaaa Ukifikiri kwa uhaki Unasawishika ati Wabunge, Marais, Mawaziri hawanyi?

Angalia mfano hapa Obama akiwa amelewa, Sikiliza Mtiririko wa sauti yake na jinsi anavyoomchachafya Jamaa bila Kutumia Lugha ya Diplomasia ambayo ni Hulka yake.

Msikilize Mzee Kinyatta Akiongea Kwa hasira sana, Akimtukana Odinga Jaramogi. Lakini watu walionjua Mzee Kenyatta alikuwa sii mtu wa Maneno mengi sana Kama hajaonja Glass moja!

NA WALE WABUNGE WALA RUSHWA SAKATA LIMEISHIA WAPI??BUNGE LINASIFA NDEFU RUSHWA.LEVI..LOH
 
Ni bora usijibu chochote ukae kimya maana unavosema unamjua halafu unachangia madudu inashangaza maana inaonekana ni jinsi gani ulivo sawa na jina lako mavipunda..
Hivi mnafundishwaga kuwadanganya watanzania sio eeh.. Maana kama wewe ni mtu makini huwezi kukoment hoja dhaifu na za kizandikizandiki kama unavofanya.

Kaa chini ujipange upya..
Nasisitiza namjua Kitwanga kuliko unavyofikiria na wala sichangii kizandiki..fuata maelekezo niliyokupa afu ndio urudi hapa
 
Hilo fizi la mdomo limelegea Kwa sababu ya kukaa glass Kwa mda mwingi , Pombe imemponza kisa alilewa akamsema vibaya Magufuli kapelekewa taarifa .
NILIOGOPA KUANDIKA HILII SASA WEWE NDIE UNAJUA UKWELI WAHUYU BWEGE ULEVI ILITUMIKA TU CHAMBO ALIMCHAMBA HON
 
Kwenye Bar wamejazana wengi tena wengine majumbani mwao familia zinashindia maharage tu, lakini wanajenga Heshima Bar , huko bar ndipo kwenye kila Aina za majungu , Uzinzi na mambo yote ya ajabu , Nchi za Uarabuni zimepiga hatua Kwa kasi kutokana na kutokumbatia Ulevi, hata ulaya na China na America hawafagilii ulevi Kwa Watumishi hata Kwa sekta binafsi.
NAHISI HATA SPIKA N JIPU

JANA NASOMA MPEKUZIHURU.COM NAONAA ANASEMA SIO ULEVI HADI WAVUTA SIGARA KUBWA BANGI NA ...MADAWA YA KULEVYA ....HEE KUMBE ANAWAJUA AMEFICHA MBAYA ANASEMA HASA WA MCHANA WENGI WANAKUJA WAMELEWA NA WENGI WANAGONGA KONYAGI
 
Habari za hivi punde zinasema Rais Magufuli amemfuta kazi Waziri wa Mambo ya Ndani, Charles Kitwanga.

Sababu kubwa ni kuwa Waziri Kitwanga kaingia bungeni akiwa amelewa na akaenda jibu swali akiwa amelewa..!

Source: Tbc1 Habari

======
Taarifa ya Ikulu:

======
Ofisi ya Waziri Mkuu:

20 Mei, 2016

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

WAZIRI MKUU AFAFANUA KUHUSU KUTENGULIWA KWA UTEUZI WA WAZIRI KITWANGA

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema uamuzi wa Rais Dk. John Pombe Magufuli kutengua uteuzi wa Waziri wa Mambo ya Ndani, Bw. Charles Kitwanga umefuata kanuni za utumishi wa umma ambao unakataza mtumishi kulewa akiwa kazini.

“Zipo sheria za utumishi ambazo mtumishi hatakiwi kunywa pombe na wala hapaswi kulewa akiwa kazini… mtumishi anapaswa kuwa na akili timamu inayokuwezesha kufanya kazi za Serikali,” alisema.

Ametoa ufafanuzi leo usiku (Ijumaa, Mei 20, 2016) wakati akijibu swali la mwandishi wa TBC1 aliyetaka kujua kama taarifa zilizoenea kuhusu kutenguliwa kwa Waziri huyo ni za kweli.

“Ni kweli Mheshimiwa Rais, Dk. John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa Waziri wa Mambo ya Ndani, Mheshimiwa Charles Kitwanga kuanzia leo tarehe 20 Mei, 2016 baada ya kuonekana amelewa wakati wa kazi. Na hili lilibainika pale alipokuwa akijibu maswali ya wizara yake leo asubuhi,” alisema Waziri Mkuu.

Waziri Mkuu amesema kuna swali aliloulizwa ambalo hakulijibu vizuri na kwamba swali hilo litapaswa kurudiwa kuulizwa baada ya wabunge kuomba muongozo wa swali hilo.

IMETOLEWA NA:

OFISI YA WAZIRI MKUU,

S. L. P. 980,

DODOMA.

IJUMAA, MEI 20, 2016
Leo ni siku ya nne sasa tangu mheshimiwa charles kitwanga atenguliwe uteuzi wake kama waziri wa mambo ya ndani ya nchi kutokana na fedheha kubwa ya kuingia bungeni akiwa amelewa, ila ninavyojua viongozi wa kitanzania walivyo hata habari ya kuwaomba radhi watanzania walipa kodi pamoja na wapiga kura wa jimboni kwake hana!!!!!
 
1. Wakati Mheshimiwa Charles Kitwanga anajibu Swali la Magdalena Sakaya mlikuwepo Bungeni?
2. Mlitambulishwa kama Wageni wa Waziri wa Mambo ya Ndani, Charles Kitwanga kama ilivyo kawaida kwa kiongozi wa Bunge kuwatambulisha wageni wa Waheshimiwa Wabunge?
3. Picha mlizopiga na mheshimiwa Kitwanga nje ya Ukumbi wa Bunge zipo? alikuwa sawasawa? Tuwekeeni hapa.
3 Kwa mujibu wenu, hii video imehaririwa, mnayo video ambayo inamuonesha Mh. Kitwanga akijibu swali la Mh. Sakaya kwa ufasaha?
4. Kwenye video hii, Wabunge walikuwa wakimcheka Kitwanga jinsi alivyokuwa akijibu maswali akiwa amelewa. Vicheko hivyo vya Wabunge navyo vimehaririwa?
 
Mkuu, wala usihangaike sana na hao jamaa. Wamechanganyikiwa. Wanamuona Mheshimiwa Rais hana akili mpaka kutamka dhahiri kwamba Kitwanga alikuwa amelewa.
 
1. Wakati Mheshimiwa Charles Kitwanga anajibu Swali la Magdalena Sakaya mlikuwepo Bungeni?
2. Mlitambulishwa kama Wageni wa Waziri wa Mambo ya Ndani, Charles Kitwanga kama ilivyo kawaida kwa kiongozi wa Bunge kuwatambulisha wageni wa Waheshimiwa Wabunge?
3. Picha mlizopiga na mheshimiwa Kitwanga nje ya Ukumbi wa Bunge zipo? alikuwa sawasawa? Tuwekeeni hapa.
3 Kwa mujibu wenu, hii video imehaririwa, mnayo video ambayo inamuonesha Mh. Kitwanga akijibu swali la Mh. Sakaya kwa ufasaha?
4. Kwenye video hii, Wabunge walikuwa wakimcheka Kitwanga jinsi alivyokuwa akijibu maswali akiwa amelewa. Vicheko hivyo vya Wabunge navyo vimehaririwa?

Naona mod kaona mada utumbo ndo mana kaiunganisha
Ila mod hawana huruma na mawazo ya mtu hawa jamaa
 
Back
Top Bottom