Waziri wa Mambo ya Ndani, aamuru kukamatwa kwa Mchungaji wa Kanisa la Pentecostal Power Ministry

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,397
EEBRefKXsAI6YRt.jpg


EEBRsoOWwAEm1NQ.jpg
> Taarifa zilizotufikia zinaeleza kuwa Waziri Kangi Lugola amefika katika kanisa hilo na kuamuru kukamatwa kwa Mchungaji wake, Nabii Eliya Mahela

> Mchungaji huyo anatuhumiwa kwa kuendesha Kanisa bila kusajiliwa na kuwapigia kelele kwa Wananchi wanaomzunguka.

EEBRz5CXYAEOozk.jpg
 
Hizo ni Operation zimamoto tu hamna lolote hapo wanaopigia kelele watu wengine wako wengi sana ila hawachukuliwi hatua yoyote sema huyo mchungaji hana koneksheni tu pengine anatumika kama bangusilo..



















Mungu Ibariki Tanzania
Mungu Ibariki Chakwale
Mungu Ibariki Gairo
Mungu Ibariki Morogoro
 
Ni hatua nzuri, na akina Mashimo nao waswekwe ndani Kwa wizi wa njia danganyifu
 
> Taarifa zilizotufikia zinaeleza kuwa Waziri Kangi Lugola amefika katika kanisa hilo na kuamuru kukamatwa kwa Mchungaji wake, Nabii Eliya Mahela

> Mchungaji huyo anatuhumiwa kwa kuendesha Kanisa bila kusajiliwa na kuwapigia kelele kwa Wananchi wanaomzunguka.

Endelea kutatua kero za wananchi mzee Lugola kweli upo makini.

Kama mmeshawaona mpaka na hao wapiga makelele safi sana. tupo pamoja na SERIKALI ktk hilo pia.

Huwezi kufanya kazi kwa juhudi na ubunifu ikiwa usiku hukulala!! Jamaa wanafungulia spika ambazo wao wanalenga kupeleka sauti mbaaaalii ili kuvuta wateja bila kujali nyumba jirani kuna kitoto kichanga kimezaliwa jana kinatakiwa kilale !!

Wakinunua uwanja jirani yako you are finished !!! Anza mapemaaa kutafuta mteja uuze hiyo nyumba hautaishi tena kwa raha!!!

Kamata wote hao mzee Lugola
 
Nani? - Mchungaji
Nini? - Kukamatwa
Lini? - Haijulikani
Wapi? - Haijulikani
Kwanini? - Kupiga kelele/kuendesha kanisa bila kibali
Vipi? - Agizo la Waziri kwa Jeshi la Polisi
 
Back
Top Bottom