Waziri wa Mambo ya Ndani aagiza Rage achunguzwe; DPP anafanya nini?

Zak Malang

JF-Expert Member
Dec 30, 2008
5,404
226
Leo gazeti la Mwananchi leo limeandika kuwa Waziri wa Ndani Shamsi vuai Nahodha kawaagiza polisi kumhoji Mbunge wa Tabora Mjini, Aden Rage kuhusiana na tuikio lake la kubeba bastola kiunoni Igunga wakati akihutubia mkutano wa CCM wa kampeni.

Jee hili si thibitisho tosha la kile kinachodaiwa kila mara, hasa na Chadema, kwamba Polisi hupata maagizi kuhusiana na kazi zao kutoka kwa wanasiasa, hasa katika shughuli za kisiasa kama vile kampeni?

Jamani, kuna ushahidi mwingine zaidi ya agizo hili la waziri kwa polisi? Kwani polisi si wako kibao Igunga, hawakuliona hili tukio. Jee ingekuwa ni Tundu Lissu ndiye alibeba silaha katika mkutano wa Chadema, saa hizi si angekuwa tayari lupango?
 
Mwita Maranya

JF-Expert Member
Jul 1, 2008
10,565
7,947

Sio kwamba polisi wanafanya kazi kwa maelekezo ya wanasiasa bali wanafanya kazi kwa maelekezo ya wanasiasa wa ccm.

Na hapa shamsi vuai nahodha anajaribu kusaidia kukifanyia kampeni chama chake kwakuwa rage ni mwana ccm mwenzake hawezi kushtakiwa hata kama atapatikana na makosa.
 
Ndoano

Senior Member
Aug 9, 2011
192
31
Kama anaimiliki hio bunduki kihalali kuna kosa gani?tusichanganye siasa na sheria
 
Mvaa Tai

JF-Expert Member
Aug 11, 2009
6,159
4,435
Leo gazeti la Mwananchi leo limeandika kuwa Waziri wa Ndani Shamsi vuai Nahodha kawaagiza polisi kumhoji Mbunge wa Tabora Mjini, Aden Rage kuhusiana na tuikio lake la kubeba bastola kiunoni Igunga wakati akihutubia mkutano wa CCM wa kampeni.

Jee hili si thibitisho tosha la kile kinachodaiwa kila mara, hasa na Chadema, kwamba Polisi hupata maagizi kuhusiana na kazi zao kutoka kwa wanasiasa, hasa katika shughuli za kisiasa kama vile kampeni?

Jamani, kuna ushahidi mwingine zaidi ya agizo hili la waziri kwa polisi? Kwani polisi si wako kibao Igunga, hawakuliona hili tukio. Jee ingekuwa ni Tundu Lissu ndiye alibeba silaha katika mkutano wa Chadema, saa hizi si angekuwa tayari lupango?
Unazungumzia lupango huwenda angeuawa kwa kisingizio kwamba alijaribu kupambana na Polisi. Mimi sina imani na Polisi nchi hii naona naiona polisi kama ni KITENGO fulani ndani ya CCM
 
sweetlady

JF-Expert Member
Dec 24, 2010
16,947
8,355
Kama anaimiliki hio bunduki kihalali kuna kosa gani?tusichanganye siasa na sheria
Kwa hiyo kila anayemiliki bastola kihalali apite ameining'iniza hadharani? Ili iweje? Hivi una habari kuwa asilimia kubwa ya watz kwa sasa wanamiliki bastola kihalal? Wanaoficha sio wajinga. Wajinga ni hao akina Rage wanaodhani kuwa bastola ni kitu cha kutisha watu. Hata hivyo afanyie huo upuuzi wake huko huko Igunga! Shame on him!
 
mkolosai

JF-Expert Member
Jun 14, 2011
1,578
1,099
Sweetlady big up, si wote wanataka kuning'iniza vibastola viunoni mwao kwat ajili ya sifa. Jambo jingine unakuwa target kwa majambawazi. Tutamsikia rage kapigwa roba ili wachukue hyo silaha.
 
Kipre tchetche

JF-Expert Member
Dec 13, 2010
238
40
Waziri wa mambo ya ndani anaagiza
sasa hivi kwani inteljensia ya polisi
ilikuwa wapi hawakumwona akipanda?
 
ntamaholo

JF-Expert Member
Aug 30, 2011
12,785
6,614
Leo gazeti la Mwananchi leo limeandika kuwa Waziri wa Ndani Shamsi vuai Nahodha kawaagiza polisi kumhoji Mbunge wa Tabora Mjini, Aden Rage kuhusiana na tuikio lake la kubeba bastola kiunoni Igunga wakati akihutubia mkutano wa CCM wa kampeni.

Jee hili si thibitisho tosha la kile kinachodaiwa kila mara, hasa na Chadema, kwamba Polisi hupata maagizi kuhusiana na kazi zao kutoka kwa wanasiasa, hasa katika shughuli za kisiasa kama vile kampeni?

Jamani, kuna ushahidi mwingine zaidi ya agizo hili la waziri kwa polisi? Kwani polisi si wako kibao Igunga, hawakuliona hili tukio. Jee ingekuwa ni Tundu Lissu ndiye alibeba silaha katika mkutano wa Chadema, saa hizi si angekuwa tayari lupango?

inawezekana kabisa, lakini hata huyo waziri kajitutumua baada ya wanaharakati kukemea. kimsingi si utaratibu kuonesha siraha yako hata kama unaimiliki kihalali, kwani kufanya hivyo ni sawa na kutishia
 
kapotolo

JF-Expert Member
Sep 19, 2010
3,727
2,212
Rage anasema alipanda nayo kwa kuwa mwenyekiti wa chadema igunga alimtishia maisha.
So Rage alipanda nayo ili kuitumia, na kwa nini asitoe taarifa polisi kama alitishiwa maisha. CCM karibu wataingia msituni.
 
Mwita Maranya

JF-Expert Member
Jul 1, 2008
10,565
7,947
Bongo bana yaani hata hili linahitaji waziri wa mambo ya ndani ku-intervene!!!!!!!!!!

Nadhani JD zao zinawataka kusubiri maelekezo ya waziri ama kiongozi wa ccm inapotokea kwamba aliyetenda kosa ni mwana ccm.

Sitoshangaa kusikia polisi wakitoa statement kwamba upelelezi unaendelea ama hakuna ushahidi wa kutosha wa kuwafanya wafungue kesi dhidi ya rage.
 
sweetlady

JF-Expert Member
Dec 24, 2010
16,947
8,355
Rage anasema alipanda nayo kwa kuwa mwenyekiti wa chadema igunga alimtishia maisha.
So Rage alipanda nayo ili kuitumia, na kwa nini asitoe taarifa polisi kama alitishiwa maisha. CCM karibu wataingia msituni.
Majibu mepesi hayana maana! Hapo kwenye huo mkutano alikuwa anamhutubia mwenyekit wa chadema? Mwongo mkubwa! Hivi ukitishiwa maisha unaanza kutembea na bastola hadharani au unaenda kuripoti panapohusika? Ccm wanatapatapa tuuuu kila kukicha, hawana jipya.
 
dhahabuinang'aa

Senior Member
Aug 10, 2011
134
28
Mi binafsi nina mtazamo tofauti labda kwa mtu aliyekaribu nae atujuze ameimiliki lini huyu ni LIMBUKENI
nahisi hana mda mrefu toka ameimiliki kwahiyo anataka watu wajue kuwa na yeye ana cha MOTO
na pia anamini ccm kuwa ni wana hati miliki ya NCHI wanajidanganya hawa punguani pumbavu zao.

MASABURI
 
Mag3

Platinum Member
May 31, 2008
12,742
22,090
Kama anaimiliki hio bunduki kihalali kuna kosa gani?tusichanganye siasa na sheria

Jamani hivi watu wengine mnaokotwa wapi ? Sasa we Ndoano, vipi wanaomiliki mapanga, mikuki, sime na silaha zingine za jadi je, umeambiwa kwamba hawayamiliki kihalali ? Maadili ya Uchaguzi ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi kifungu namba 2.2(c) kinasema...
Mtu yeyote haruhusiwi kuwa na/au kubeba silaha ya aina yoyote ikiwa ni pamoja na silaha za jadi au zana yoyote inayoweza kumdhuru mtu katika mkutano wa kampeni au mkusanyiko wowote wa kisiasa.
Sasa mpaka hapo tayari huyu exconvict Aden Rage amefanya kosa na haikuwepo na haja ya Waziri kuingilia kati hali polisi walikuwapo. Ni kwamba hili genge la majambazi linalojulikana kama CCM, liko juu ya sheria na hata wakifanya uhuni gani hakuna wa kuwachukulia hatua. Na hiyo ni sababu mojawapo kwa nini wanang'ang'ania madaraka, wanajua wakiachia watawajibishwa kwa uhuni waliowafanyia Watanzania kwa miaka nenda rudi. Hivyo hivyo mdokozi Aden Rage alivyoweza kuingia mjengoni na ndivyo hawa woote mafisadi wameweza kuyakwaa madaraka kuanzia na Kikwete mwenyewe.
 
Ninaweza

JF-Expert Member
Dec 14, 2010
11,481
6,036
Jaman rage kupanda jukwaani na bastola haikuwa bahati mbaya, nakataaaaaaa kabisa, hii kitu ilipangwa. Tunaoishi igunga kuna vituko vingi sana ccm wanapeleka action movies huko vijijini wakiwaambia watu kuwa endapo watachagua cdm nchi itaingia vitan kama hizo muvi za akina vandame zinvyo onesha.OVA!
 
Rejao

JF-Expert Member
May 4, 2010
9,232
4,045

Na kauli mbinu ya CDM ya kutaka kuingia msituni unaiongelea vp?
Wananchi wa Igunga wana uelewa wa kutosha wa mambo! Usitake kuwaona washamba kihivyo.
 
Izack Mwanahapa

JF-Expert Member
Apr 21, 2011
497
235
Shamsi Vuai Nahodha anaonekana ni mtendaji mzuri na mtu mwenye upeo ndio maana ameagiza alichokiagiza, lakini tusishangae atakapokatishwa tamaa kama alivyokatishwa tamaa na aliyekuwa katibu wa sisim bw. makamba alipotoa tamko la kutaka muafaka kati ya sisim na CDM katika mgogoro wa Arusha.
 
Rejao

JF-Expert Member
May 4, 2010
9,232
4,045
Kwenye hiyo interview masaburi kama wewe usingepita walah tena!..
Mimi siitwi masaburi..Masaburi ni Meya wa Jiji la DSM! Mimi naitwa rejao!
Hivi mbona wewe mtoto unalazimishia sana kuingia kwenye siasa? Kule MMU ndio kunakufaa zaidi.
 
10 Reactions
Reply
Top Bottom