Waziri wa Maliasili na Utalii Dr. Kigwangalla amsimamisha kazi Mkurugenzi wa Wanyama Pori

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,261
Akizungumza kutokea ndani ya Hifadhi ya Serengeti, ambapo amefanya ziara ya kushtukiza na kuuzunguka mpaka wote wa Mashariki ambapo hifadhi ya Serengeti inapakana na Pori la Tengefu la Loliondo, lenye mgogoro wa muda mrefu, Dr. Kigwangalla ameagiza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Mej. Gen. Gaudence Milanzi, kumsimamisha kazi Mkurugenzi wa wanyamapori Prof. Alexander Songorwa mara moja.

Ametoa sababu kuwa ni Tuhuma za kuhujumu Serikali kwa kutoa taarifa za siri za Serikali kwa vyombo vya habari na kutunga taarifa zenye kulenga kuchochea mgogoro wa Loliondo.

Waziri Kigwangalla amesema kuwa Mkurugenzi huyo amekuwa akifanya kazi kwa maelekezo ya muwekezaji wa Kampuni ya Utalii wa Uwindaji ya OBC, Kampuni hii imekuwa ikihusishwa na kashfa kwa miaka mingi.
----------------

Taarifa zaidi..

Akizungumza kutokea ndani ya Hifadhi ya Serengeti, ambapo amefanya ziara ya kushtukiza na kuuzunguka mpaka wote wa Mashariki ambapo hifadhi ya Serengeti inapakana na Pori Tengefu la Loliondo, lenye mgogoro wa muda mrefu, Dkt. Kigwangalla ameagiza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Maj. Gen. Gaudence Milanzi, kumsimamisha kazi Mkurugenzi wa Wanyama Pori, Prof. Alexander Songorwa mara moja. Ametoa sababu kuwa ni:

1. Tuhuma za kuhujumu Serikali kwa kutoa taarifa za siri za Serikali kwa vyombo vya habari na kutunga taarifa zenye kulenga kuchochea mgogoro wa Loliondo. (Jana usiku zilizunguka taarifa kwamba Dkt. Kigwangalla yupo na msafara wa gari mbili binafsi (private) njiani kwenda Loliondo na kwamba atalala Hotel ya Acacia iliyopo Karatu. Na leo msafara wake umekuwa ukifuatiliwa na watu wasiojulikana ambapo kila hatua aliyofikia ilikuwa ikiripotiwa kwenye mtandao, hali ambayo imetishia usalama wa kiongozi huyo).

2. Waziri Kigwangalla amesema Mkurugenzi huyo amekuwa akifanya kazi kwa maelekezo ya muwekezaji wa Kampuni ya Utalii wa Uwindaji ya OBC (maarufu kama kampuni ya kiwindaji ya wafalme wa Dubai). Kampuni hii imekuwa ikihusishwa na kashfa kwa miaka zaidi ya 26.

3. Aidha Prof. Songorwa amekuwa akihusishwa na kashfa ya kushiriki kugawa vitalu vya uwindaji kinyume cha sheria. Wiki mbili zilizopita Waziri Kigwangalla alisitisha mchakato wa kuhuisha leseni za uwindaji uliofanywa na Prof. Jumanne Maghembe, aliyekuwa waziri wa Maliasili na Utalii kwa tuhuma za rushwa na kukosekana uwazi kwenye mchakato huo. Pia ameelekeza mchakato wa kugawa vitalu sasa ufanywe kwa njia ya mnada.

Pia, ameelekeza TAKUKURU waanze kuchunguza kashfa za rushwa dhidi ya kampuni ya OBC na waanze kwa kumhoji bwana Mollel (Mkurugenzi wa OBC) ambaye amekuwa akijigamba kila kona kuwa alimhonga Maghembe dola 200,000, huyu kijana Kigwangalla dola 100,000 inamtosha! Dkt. Kigwangalla amesisitiza hahongeki na ndiyo maana jitihada za bwana Mollel kumuona zimekwama, na hata alipotumiwa ujumbe kupitia watu wake wa karibu alikataa.

Ili kuimarisha ulinzi wa mpaka wa Mashariki mwa Serengeti, Waziri Kigwangalla amewaondoa Askari wote wa Kituo cha Geti la Kleins kwa kuwa wamekuwa wakitumika na mwekezaji huyo ambaye ana mahusiano ya Karibu na Prof. Songorwa, na alikuwa na mahusiano ya karibu na Prof. Maghembe, Lazaro Nyalandu, balozi Kagasheki na Mawaziri wa Maliasili na Utalii wa zamani.
 
Nisionekane kupinga ila kwa nini hiyo kampuni ina m,atatizo na wananchi siku nyingi lakini haifungwi?? Akumbuke ni kampuni hiyo hiyo ilimtoa Kagasheki. Shauri lake. Wenzake walikaa mbali na hiyo kampuni wakadumu kidogo
 
Nisionekane kupinga ila kwa nini hiyo kampuni ina m,atatizo na wananchi siku nyingi lakini haifungwi?? Akumbuke ni kampuni hiyo hiyo ilimtoa Kagasheki. Shauri lake. Wenzake walikaa mbali na hiyo kampuni wakadumu kidogo
sio kwa kipindi hiki,ilikuwa kipindi tofauti.
 
Taarifa la gazeti la Jamhuri dhidi ya Waziri wa Maliasili imemwondoa huyu Mkurugenzi hongera Waziri Hamisi Kiwangwala. Ni fundisho kwa viongozi wanaonunua magazeti kuficha maovu yao. Niliwahi kuandika humu gazeti la Jamhuri huwa linatumika kuchafua viongozi.
 
Nisionekane kupinga ila kwa nini hiyo kampuni ina m,atatizo na wananchi siku nyingi lakini haifungwi?? Akumbuke ni kampuni hiyo hiyo ilimtoa Kagasheki. Shauri lake. Wenzake walikaa mbali na hiyo kampuni wakadumu kidogo
Ni suala gumu kweli. Mkuu wa wilaya husika pia anaweza kwenda na maji. Unajua kilichopo yule muwekezaji hana tatizo ila tatizo ni wananchi kwani OBC amekuwa ni muwekezaji mwenye matokeo mazuri ila wananchi ndiyo kimeo, ila in short kuna mengi nyuma ya pazia. UDOM kwa sehemu kubwa ni OBC, n.k., na huja mara moja kwa mwaka
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom