Waziri wa Maji, Umepambwa sasa Jipambe Mwenyewe

JF Member

JF-Expert Member
Dec 14, 2014
7,389
9,664
Aweso wewe ni kijana, Unao uwezo kabisa wa kufanya mambo makubwa na kuwa mtu mhimu sana katika hii nchi.

Nimeona Mama amekupamba na ukapambika, kiufupi tunaelewa kazi yako hasa ukiwa na msimamizi mzuri yaani waziri mkuu, rais na makamu wa rais.

Maji ni kero kubwa sana kwa wana nchi. Kwa taarifa yako tu na ninazani unajua: Kipindi cha JPM wana nchi walipata matumaini ya kupata maji kwa haraka na Wakandarasi walikuwa wanafanya kazi hata bila kulipwa ili muradi tu miradi ikamilike kwa mda na wana nchi wapata huduma. Sasa hivi kazi inafanyika lakini taratibu sana wananchi wamekosa Imani na serikali.

Mifano Michache tu ni miradi ya maji ya Ubungo/Kibamba/Goba/Msakuzi/Msumi/Mkabe/Mbopo. Hii miradi ilikuwa kasi sana kabla ya Machi 2021. Mabomba mengine hadi sasa yako saiti. Matenki yaliyokuwa yanajengwa sasa yamesimama na watu wa maeneo hayo hawana maji. Wengi wanakunywa maji kwenye vijito/mitaro na wenye uwezo wananunua kwenye magari.
 
Back
Top Bottom