Patriot
JF-Expert Member
- Feb 11, 2008
- 5,703
- 4,697
Leo itakuwa ni siku ya pili mji wa Morogoro ukiwa mkavu, bila maji. Maji yamekauka ghafla. Taarifa za walioko mamlaka ya maji safi na taka, MORUWASA, zinasema mkurugenzi hana uwezo wa kuongoza mamlaka hii. Tatizo la sasa kumbe maji yamefungwa kwa makusudi ili kuepuka kipindupindu kinachoweza toke kutokana na matumizi ya maji ambayo hayawekewi dawa.
Baada ya mkurugenzi kushindwa kupanga utaratibu wa kuagiza dawa za kusafisha maji, ametoa amri maji yafungwe kwa siku tatu kwa kisingizio cha matengenezo, huku akisubiri dawa zifike. Yaweza kuwa ni njia ya tahadhari lakini lazima tutegemee hatari zaidi kipindi hiki ambacho huenda watu watalazimika kutumia maji machafu zaidi.
Ndugu Waziri, Mkurugenzi huyu ni jipu. hataweza kutusaidia ktk mji huu kwa spidi hii ya mkuu wa nchi.