Waziri wa maji / TANESCO ikikata umeme nansio maji yanakuja baada ya miezi, kwanini?

mfungwa

JF-Expert Member
May 23, 2015
1,291
341
Kipindi Makamu wa Rais na baadae Waziri mkuu akija kufungua mradi wa maji hapa Nansio Ukerewe pamoja na Kata za Mukituntu, Namagondo, na Igalla alisema Idara ya maji hakikisheni maji yanatoka ili wananchi wafaidike kwani wamezungukwa na maji. Hii sentensi inakuwa inavunjika kabisa wala kutokuwa na maana hapa wilayani ukerewe.

Kwani TANESCO wakikata umeme kutokana na kutolipa bili kwa idara hii ya maji basi imekuwa desturi maji yanatoka baada ya miezi kuanzia mitano nakuendelea. sasa wewe waziri wa maji kazi yako ninini kwa hawa watendaji wako wanaopaswa kulipia umeme kabla Tanesco hawajakata umeme wakidai bili yao.
 
Mkuu kumbe upo nansio..af mvua ikichimba mkwara tu kidogo(achana na kunyesha) umeme nao unasepa..mara utasikia nguzo zmeanguka sijui Namagubo, mara cjui wap hahahaaaa
 
Si ni mpaka walipe bill ya umeme ndiyo mitambo ipate kusukuma maji...

Kama hawajalipa ina maana hakuna maji...


Cc: mahondaw
 
Back
Top Bottom