Waziri wa Maji, Mbinu hizi za ulaji chini ya Wizara yako unazijua?

kifupi kirefu

JF-Expert Member
Oct 29, 2018
539
3,507
Kama Kuna zoezi gumu na linaweza kuitia hasara serikali nikushindwa kusimamia suala la taasisi zinazosimamia maji nchini. Taasisi hizi zihujumu huduma ya maji kwa njia zifuatazo;

1. Ukiomba kuunganishiwa maji upati msaada huo au utaambiwa subiri mradi utakuja ufike kwako, lakini ukizungumza na mtendaji ndani ya ofisi kila kitu unafanikisha. Wananchi waliojichanga kuunganishiwa maji ni wengi wengi wengi. Hii Ni rushwa iliyohalalishwa na mameneja wa maji.

2. Ukitaka kuunganishiwa maji lazima vifaa ukanunue duka wanalotaka wewe vinginevyo utaambiwa vifaa ni feki au havifai. Hapa Kuna percentage. Niombe mtangaze maduka mliyoingia ubia nayo.

3. Wapo mafundi wanaochimba na kufunga mabomba ya maji, Hawa wamefanya huu ni mradi. Wanafunga bomba Leo kesho unasikia limepasuka, unawahita wanakupigia gharama kwa kisingizio ukifuata utaratibu wa ofisi hautohudumiwa. Na kweli ukiripoti ofisini kwamba bomba limepasuka unakaa wiki kadhaa bila huduma. Waziri toa marufuku kwa wananchi kuchangishana kuwahita mafundi wa maji na wakibainika wachukuliwe hatua, wananchi wakikosa mwanya wakutoa rushwa watasimamia vyema maji katika eneo lao na watawawajibisha mameneja wa maji.

4. Kuna namba za huduma kwa mteja, ukipiga kwamba bomba limepasuka maji yanamwagika baraabarani wanakuambia wanashughulikia. Ukikata simu unapokea ujumbe taarifa yako imefanyiwa kazi...whaaat.

5. Kutokana na hujuma za watendaji na ufungaji mabomba usioridhisha, maji mengi yanapotea njiani na hivyo kuisababishia hasara serikali. Niombe ushirikiane na Waziri wa serikali za mitaa, jukumu lakuakikisha hakuna maji yanamwagika kwa bomba kupasuka liwe chini ya mwenyekiti wa kijiji au mtaa na afisa mtendaji wa kijiji au kata. Endapo itabainika maji yamezagaa barabarani mtendaji wa mtaa au Kijiji husika awajibishwe pale itakapobainika ajaripoti kwa meneja wa maji, na ikibainika ameripoti ila meneja amezembea basi meneja awajibishwe. Watendaji wa vijiji na kata wawasilishe taarifa za mwezi kwa Mkurugenzi na kwako utabaini ukubwa wa tatizo kwa kipindi kifupi.

5. Kubambika bili kunakofanywa na wasoma mita, ipo tabia yakusogeza mita mbele hasa pale unapokorofishana na mtendaji wa idara ya maji. Lakini pia ukikataa kutoa kitu kidogo wanapohitaji. Imezuka tabia familia inapelekewa bili ya units 120 au 130 kwa mwezi unajiuliza haya maji yametumikaje nyumba yafamilia moja. Jibu la wasoma mita ni njoo ujionee mwenyewe. Ila ukimpooza kidogo anaandika mita mtakazokubaliana. Chukueni bili za wateja wenu mwone variation ya mwezi na mwezi

6. Wauza maji. Yapo maeneo maji yanakatwa ili watu wauze maji kwa magari au mapipa.

Haya ni machache ila nimalizie kusema tatizo la wenye maji kuiingizia hasara serikali linaweza kuwa serious kuliko hata upungufu wa maji yenyewe. Maji yanamwagika mitaani hakuna marekebisho. Tutapata wapi maji yakuwaunganisha wasio nayo?
 
Ujenzi wa Miradi ya Maji ni MITAJI kwa MAMENEJA WA RUWASA.

Baada ya miaka miwili MAMENEJA WA RUWASA watakuwa ni MATAJIRI KUPINDUKIA.
 
Hili jambo ni miongoni mwa masuala ya kutazamwa kwa karibu sana, Nilishangaa Waziri wa maji amefika Morogoro anaishia kuongea na watendaji wake anaacha kuitisha mkutano wa hadhara na wananchi wamuambie madudu wanayofanya watu wake kwa raia

Moruwasa Morogoro wanauza sana mabomba ya miradi kwa kisingizio kuwa serikali haijatoa fedha na vifaa kwaajili ya kulazia mabomba kwenye maeneo ya makazi.

Nikuambie jambo moja Waziri, nenda katazame kwenye records, utaona kuwa kuna watu waliomba maji tangu 2019 lakini mpaka leo hawajaunganishiwa, lakini hapohapo utakuta kuna watu wameomba maji mwezi March 2021 nadni ya siku mbili wameunganishiwa maji, swali ni kwamba hawa wanaosubiri tangu 2019 wameikosea nini serikali, huko nyuma kisingizio ilikuwa mita, mita zimekuja wamepewa watu wa karibuni wale wa zamani wameachwa.
 
Back
Top Bottom