Waziri wa Maji, Jumaa Aweso: Wachawi kikwazo maji kufika vijijini

UCHAWI UPO TANZANIA TENA WA KUTISHA.

KUNA VIJIJI HAVITAKI MAENDELEO KABISA.

KUNA JAMAA YANGU MIAKA HIYO YA NYUMA ALIMALIZA DIPLOMA YA UALIMU AKAPANGIWA KIJIJI FULANI NA SERIKALI.
MOTO ALIOKUTANA NAO HUKO ALIACHA KAZI AKAAMUA KUJA MJINI KUFUNDISHA PRIVATE SCHOOL.

UCHAWI UPO TENA NI WAKISHAMBA KURUDISHA NYUMA MAENDELEO.

ULIZA WAALIMU NA MANESI WALIOPANGIWA VIJIJINI HUKO, KUNA WENGINE WANACHAPWA VIBOKO USIKU KUCHA.

Sent from my Infinix Zero 3 using JamiiForums mobile app
 
Nilifika kijijini Kilindi huko ndani ndani wakati napata chakula nilikutana na mtendaji/ km sijakose anacheo cheo huko ofisini. Analalamika kila akijenga mashimo ya choo kinatitia.Akawa kadata anawaza jinsi atakavyowakilisha baheti yake tena ya mashimo.
Mimi nikamtonya safari hii waite wazee tuu wa kijiji waambie unataka kuanza ujenzi wa mashimo ya choo.Tena utaanza kwa dua /sala kabisa. Alinipigia simu kafanikiwa na maisha yanaenda
Hahaha

Ova
 
UCHAWI UPO TANZANIA TENA WA KUTISHA.

KUNA VIJIJI HAVITAKI MAENDELEO KABISA.

KUNA JAMAA YANGU MIAKA HIYO YA NYUMA ALIMALIZA DIPLOMA YA UALIMU AKAPANGIWA KIJIJI FULANI NA SERIKALI.
MOTO ALIOKUTANA NAO HUKO ALIACHA KAZI AKAAMUA KUJA MJINI KUFUNDISHA PRIVATE SCHOOL.

UCHAWI UPO TENA NI WAKISHAMBA KURUDISHA NYUMA MAENDELEO.

ULIZA WAALIMU NA MANESI WALIOPANGIWA VIJIJINI HUKO, KUNA WENGINE WANACHAPWA VIBOKO USIKU KUCHA.

Sent from my Infinix Zero 3 using JamiiForums mobile app
Hahahaha

Ova
 
Hello JF

Hii habari imenichekesha sana
----
Waziri wa Maji, Jumaa_Aweso ameeleza kupitia alipokuwa katika ziara ya kukagua miradi ya maji Vijijini moja ya kituko alichokutana nacho kwenye kijiji kimoja alipomuuliza mkandarasi sababu ya maji kutokuwepo kwenye kijiji hicho licha ya kujengwa tank kubwa la maji.

"Unakwenda Vijijini unakuta 'tank' kubwa lakini hakuna maji, unauliza kwa mkandarasi kwanini hakuna maji anakwambia Mh. Naomba nikunong'oneze namwambia hapana! Waeleze wananchi kwanini maji hakuna anasema hajawahi kuona wananchi wachawi kama Vijijini anasema mabomba Usiku yanapaa kama ndege, namuuliza rubani wake yupo wapi? Kwahiyo wahandisi wa namna ile hawawezi kufanya kazi na wizara"

Hao ni wahandisi madaktari nao hivyo hivyo na sera zao za nyungu. Siku tukikuta marubani wa hayo mabomba ni msukuma na yule mwenziwe wala tusishangae.

Hiiiiii bagosha!
 
Kuna barabara ya vikawe kibaha.wachawi wa vikawe hawataki iwekwe Rami.
Barabara inayounganisha wilaya na wilaya mpaka leo HAINA rami
 
Nina bro wangu alipata tenda ya kuchimba visima ilikuwa songea kijiji sikumbuki waliua sana mashine akapiga bonge la hasara baadae ndio akaumwa sikio akawaita wazee wa kijiji kikapikwa chakula na pombe wakaaanywa baada ya hpo wazee wakagawana visima kisima fulani kitalindwa na fulani kisima fulani kitalindwa na fulani sio kulinda na mtutu wanajua wenyewe listi ilikuwa inapangwa na mbabe wao mzee mmoja mbaya sana anaitwa roketi na akachimba mkwara ole wao kazi isiende mbona wiki tu watu wakaanza kutumia maji
Duh,wapi huko?
 
Kumbe huenda Ndiyo sababu kule Handeni maji hakuna tangu uhuru?

Mto ruvu upo karibu sana korogwe iko pale karibu sana lakini mpaka leo maji ni shida kubwa.

Vyanzo vya maji vingi lakini maji ni shida kubwa kuliko maelezo.
 
Haya mambo ukisimuliwa unaweza usiamini kabisa..juzi nimeshuhudia caterpillar la kuchonga barabara huko chunya limekwama eti
 
Huyu waziri kwasababu yeye katokea Pangani kwenye maendeleo duni na Imani za kichawi anataka nchi nzima wawe na akili na mawazo kama yake.
Tuna safari ndefu kama taifa.!!
 
📍 Chalinze

"Nilienda Mwakitoryo,Shinyanga, mradi wa Bil 1.4 lakini hautoi maji,ukimuuliza Mhandishi anasema Mhe Waziri sijawahi kuona wananchi wachawi kama kijiji hiki,usiku mabomba yanapaa kama ndege. Nikamuuliza kama yanapaa rubani wake yuko wapi?,"-Waziri wa Maji Jumaa Aweso
IMG_20220322_220159_165.jpg
 
22 Reactions
Reply
Back
Top Bottom