Waziri wa Maji, Jumaa Aweso: Wachawi kikwazo maji kufika vijijini

Hello JF

Hii habari imenichekesha sana
----
Waziri wa Maji, Jumaa_Aweso ameeleza kupitia alipokuwa katika ziara ya kukagua miradi ya maji Vijijini moja ya kituko alichokutana nacho kwenye kijiji kimoja alipomuuliza mkandarasi sababu ya maji kutokuwepo kwenye kijiji hicho licha ya kujengwa tank kubwa la maji.

"Unakwenda Vijijini unakuta 'tank' kubwa lakini hakuna maji, unauliza kwa mkandarasi kwanini hakuna maji anakwambia Mh. Naomba nikunong'oneze namwambia hapana! Waeleze wananchi kwanini maji hakuna anasema hajawahi kuona wananchi wachawi kama Vijijini anasema mabomba Usiku yanapaa kama ndege, namuuliza rubani wake yupo wapi? Kwahiyo wahandisi wa namna ile hawawezi kufanya kazi na wizara"
Miaka 60 baada ya uhuru
 
Ni kweli kabisa ndugu Waziri unachosema wala si uongo.

Kwa sehemu fulani wachawi wanakwamisha
Maendeleo sana.

Wachawi hawapatani na
Maji wala Nuru Yani umeme!
 
22 Reactions
Reply
Back
Top Bottom