Waziri wa Maji, Jumaa Aweso: Wachawi kikwazo maji kufika vijijini

Rebeca 83

JF-Expert Member
Jun 4, 2016
14,840
31,583
Hello JF

Hii habari imenichekesha sana
----
Waziri wa Maji, Jumaa_Aweso ameeleza kupitia alipokuwa katika ziara ya kukagua miradi ya maji Vijijini moja ya kituko alichokutana nacho kwenye kijiji kimoja alipomuuliza mkandarasi sababu ya maji kutokuwepo kwenye kijiji hicho licha ya kujengwa tank kubwa la maji.

"Unakwenda Vijijini unakuta 'tank' kubwa lakini hakuna maji, unauliza kwa mkandarasi kwanini hakuna maji anakwambia Mh. Naomba nikunong'oneze namwambia hapana! Waeleze wananchi kwanini maji hakuna anasema hajawahi kuona wananchi wachawi kama Vijijini anasema mabomba Usiku yanapaa kama ndege, namuuliza rubani wake yupo wapi? Kwahiyo wahandisi wa namna ile hawawezi kufanya kazi na wizara"
 
Huyu Jamaa atakuwa ni Muongo..., Mosi mkandarasi hawezi kutoa majibu ya hivyo, pili angeona kweli hayo asingebaki kufanya kazi hapo angeshaondoka zamani.., na kama kweli kaona apunguze kutumia vilevi

Na hao wananchi angewaambia wampe hio teknolojia aweze kupaisha maji kutoka huko yaliko mpaka majumbani mwa watu..., kwanini tuingia gharama ya mabomba...
 
Kuna mambo yanaweza kuonekana ni masihara lakini kweli...

Kazi za ujenzi vijijini ni ngumu sana...
Nina bro wangu alipata tenda ya kuchimba visima ilikuwa songea kijiji sikumbuki waliua sana mashine akapiga bonge la hasara baadae ndio akaumwa sikio akawaita wazee wa kijiji kikapikwa chakula na pombe wakaaanywa baada ya hpo wazee wakagawana visima kisima fulani kitalindwa na fulani kisima fulani kitalindwa na fulani sio kulinda na mtutu wanajua wenyewe listi ilikuwa inapangwa na mbabe wao mzee mmoja mbaya sana anaitwa roketi na akachimba mkwara ole wao kazi isiende mbona wiki tu watu wakaanza kutumia maji
 
Chai tu hizi.
 
Back
Top Bottom