Waziri wa maendeleo ya mifugo, Titus Kamani atinga kijiwe cha kahawa Shinyanga, akata vikombe kadhaa

SULEIMAN ABEID

JF-Expert Member
Feb 26, 2013
390
385
Waziri wa Maendeleo ya Mifugo nchini na Mbunge wa Jimbo la Busega (CCM) mkoani Simiyu, Titus Kamani amelazimika kushiriki katika kijiwe cha Kahawa mjini Shinyanga kilichopo jirani na Ofisi za Chama Cha Mapinduzi (CCM) mjini humo baada ya wananchi kumzuia alipokuwa akitokea Dodoma kushiriki kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC).

Tukio hilo lilitokea Jumatatu ya Mei 25, 2015 saa mbili asubuhi baada ya wananchi kuliona gari la waziri likiwa limeegeshwa jirani na Soko Kuu mjini Shinyanga likipeperusha bendera ya serikali huku likiwa na namba zinazoonesha ni gari la Waziri wa Maendeleo ya Mifugo, ambapo wananchi hao walimtuma mmoja wao amfuate amuombe aende katika kijiwe hicho ili aweze kusalimiana nao

Waziri Kamani bila kinyongo aliteremka katika gari lake na kuelekea katika kijiwe hicho cha Kahawa kitendo ambacho kiliwafurahisha wananchi waliokuwa wamekaa kijiweni hapo, ambapo baada ya kufika alikabidhiwa kikombe cha kahawa na kuanza kuinywa bila ajizi na mmoja wa wananchi aliyekuwa akimfahamu alimtambulisha rasmi kwa wananchi wenzake kwamba, huyo bwana ni waziri wa maendeleo ya mifugo.

Utambulisho huo uliongeza furaha ya wana kijiwe hicho cha kahawa hali iliyosababisha wapita njia wengine kuamua kusogolea eneo hilo na kujumuika pamoja na waziri katika kunywa kinywaji hicho cha kahawa wakionesha kufurahishwa na kitendo cha waziri kukubali wito wa wananchi.

Kwa upande wake mmiliki wa kijiwe hicho, Bakari Rashidi, ambaye pia ni mwenyekiti wa mtaa wa Ibinzamata Manispaa ya Shinyanga, aliwaeleza wateja wake kwamba kitendo kilichooneshwa na waziri Kamani kinatokana na CCM kuwa na hazina kubwa ya viongozi wanaowajali wananchi, ambapo alisema pamoja na kwamba ni waziri, lakini hakuwanyanyapaa wananchi hao pale walipomuomba asalimiane nao.

"CCM bwana tuna hazina kubwa ya viongozi, ni viongozi wa watu, ninyi wenyewe mmejionea leo hii, nani alikuwa anamfahamu waziri huyu, lakini bila kujali hadhi yake ya uwaziri amekubali kukaa na sisi hapa na tumekunywa naye pamoja kahawa, CCM ni chama dume bwana, kina viongozi wanaowajali wananchi, mwingine asingekubali kukaa kwenye benchi hizi na kunywa kahawa pamoja na sisi huku tukibadilishana naye mawazo," alieleza Bakari.

Kwa upande wake waziri Kamani aliwashukuru wananchi hao kwa kitendo chao cha kumwita kwa lengo la kusalamiana na kufahamiana ambapo pia alimtambulisha mwenyekiti wa CCM wa wilaya ya Maswa, Mheshimiwa Peter Bunyongoli na kwamba yeye mwenyewe mbali ya nafasi ya uwaziri na ubunge alionao pia ni mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Simiyu. :sad:
 
Attachments

  • Kamani 2.jpg
    Kamani 2.jpg
    113.3 KB · Views: 1,957
Angeshiriki kwenye utatuzi wa matatizo ya wafugani ningeona amefanya cha maana otherwise ushiriki huu wa kunywa gahawa ni unafiki na unakubalika pekee na wananchi wasiojitambua.
 
Hukuna rangi ambayo hata acha kuiona, wana Busega wameshaamua
 
duu, hii nayo imekuwa habari? inaonyesha jinsi gani watawala walivyojitenga na wananchi, ndo maana wakifanya tukio kama hilo watataka litangazwe na vyombo vyote vya habari.
 
Kama yeye ni Waziri na wananchi wa Mkoa wake Shinyanga/Simiyu hawamjui, yani bado wanamshangaa hadi leo, inatosha sana kuonesha kwa jinsi gani walivyo mbali na wananchi. Wanatafuta pa kutokea siku hizi za mwisho, poor CCM! Na huyo mwenyekiti wa mtaa bado anaamini mpaka leo kuwa huyo mtu kuja na kuwapumbaza hapo kijiweni ndio kuwa karibu nao. Ama kweli mtaji wa CCM ni ujinga wa watu kama hawa (Mwenyekiti wa Ibinzamata) na wenzake waliokuwapo kijiweni siku hiyo
 
Waziri wa Maendeleo ya Mifugo nchini na Mbunge wa Jimbo la Busega (CCM) mkoani Simiyu, Titus Kamani amelazimika kushiriki katika kijiwe cha Kahawa mjini Shinyanga kilichopo jirani na Ofisi za Chama Cha Mapinduzi (CCM) mjini humo baada ya wananchi kumzuia alipokuwa akitokea Dodoma kushiriki kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC).

Tukio hilo lilitokea Jumatatu ya Mei 25, 2015 saa mbili asubuhi baada ya wananchi kuliona gari la waziri likiwa limeegeshwa jirani na Soko Kuu mjini Shinyanga likipeperusha bendera ya serikali huku likiwa na namba zinazoonesha ni gari la Waziri wa Maendeleo ya Mifugo, ambapo wananchi hao walimtuma mmoja wao amfuate amuombe aende katika kijiwe hicho ili aweze kusalimiana nao

Waziri Kamani bila kinyongo aliteremka katika gari lake na kuelekea katika kijiwe hicho cha Kahawa kitendo ambacho kiliwafurahisha wananchi waliokuwa wamekaa kijiweni hapo, ambapo baada ya kufika alikabidhiwa kikombe cha kahawa na kuanza kuinywa bila ajizi na mmoja wa wananchi aliyekuwa akimfahamu alimtambulisha rasmi kwa wananchi wenzake kwamba, huyo bwana ni waziri wa maendeleo ya mifugo.

Utambulisho huo uliongeza furaha ya wana kijiwe hicho cha kahawa hali iliyosababisha wapita njia wengine kuamua kusogolea eneo hilo na kujumuika pamoja na waziri katika kunywa kinywaji hicho cha kahawa wakionesha kufurahishwa na kitendo cha waziri kukubali wito wa wananchi.

Kwa upande wake mmiliki wa kijiwe hicho, Bakari Rashidi, ambaye pia ni mwenyekiti wa mtaa wa Ibinzamata Manispaa ya Shinyanga, aliwaeleza wateja wake kwamba kitendo kilichooneshwa na waziri Kamani kinatokana na CCM kuwa na hazina kubwa ya viongozi wanaowajali wananchi, ambapo alisema pamoja na kwamba ni waziri, lakini hakuwanyanyapaa wananchi hao pale walipomuomba asalimiane nao.

"CCM bwana tuna hazina kubwa ya viongozi, ni viongozi wa watu, ninyi wenyewe mmejionea leo hii, nani alikuwa anamfahamu waziri huyu, lakini bila kujali hadhi yake ya uwaziri amekubali kukaa na sisi hapa na tumekunywa naye pamoja kahawa, CCM ni chama dume bwana, kina viongozi wanaowajali wananchi, mwingine asingekubali kukaa kwenye benchi hizi na kunywa kahawa pamoja na sisi huku tukibadilishana naye mawazo," alieleza Bakari.

Kwa upande wake waziri Kamani aliwashukuru wananchi hao kwa kitendo chao cha kumwita kwa lengo la kusalamiana na kufahamiana ambapo pia alimtambulisha mwenyekiti wa CCM wa wilaya ya Maswa, Mheshimiwa Peter Bunyongoli na kwamba yeye mwenyewe mbali ya nafasi ya uwaziri na ubunge alionao pia ni mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Simiyu. :sad:

Umeamua kumpigia kampeni? Bila shaka siyo bure ni lazima ina malipo. Hongera
 
Hongera sana Dr Titus cheers.....wasiokujua watasema mengi but kaza butiiiiii

mwaka wa Jinamizi la kutisha kwa wanasiasa...mpaka ifike October 25 wapo watakaowaamkia watoto wadogo.
 
Alafu akapiga picha kwa simu yake na akaja kuanzisha post hapa jf
Hongera muheshimiwa waziri hii bahati ya kukutana na wananchi huwa ni wakati wa kampeni tu!!
 
asiyejitambua pekee ndo anaweza kuungana naww mtoa mada kufurahia hicho kitendo.
 
Back
Top Bottom