Boniphace Kichonge
JF-Expert Member
- Jul 31, 2017
- 1,606
- 1,956
Waziri wa Madini Angellah Kairuki amesaini Kanuni za Sheria Mpya ya Madini ambapo Wakala wa Jiolojia Nchini (GST) amepewa nguvu ya kisheria ya kuingia katika ardhi yoyote kufanya utafiti wa kina wa madini.
Mwaka jana Bunge lilipitisha Sheria mbili za madini ambazo zinalenga kuleta mabadiliko makubwa katika Sekta ya Madini.
Hata hivyo kanuni za sheria hizo zilikuwa bado hazijasainiwa na Waziri wa Madini hadi Januari mwaka huu jambo ambalo lilimkera Rais John Magufuli na kutoa agizo zikamilike ndani siku tano.
Akizungumza leo Januari 28 Naibu Waziri wa Madini Dotto Biteko amesema kuwa kanuni hizo zimesainiwa Januari 9 mwaka huu ikiwa ni siku moja baada ya Rais John Magufuli kuagiza kukamilishwa kwa mchakato wa kanuni hizo ndani ya siku tano.Biteko alikuwa akizungumza mbele ya Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini ambayo ilitembelea ofisi za GST mjini Dodoma.
“Kuna watu wanasema sheria hii mpya itafukuza wawekezaji na hakuna wawekezaji wapya watakaokuja lakini nataka kuwaambia kuwa kuna wageni wengi wanakuja kutaka kuwekeza katika migodi mikubwa,” amesema.
Amesema wastani katika kila wiki wamekuwa wakipokea wawekezaji kati ya 10 na 20 ambao wanaonyesha nia ya kuwekeza nchini katika sekta hiyo kwa hiyo sheria sio kikwazo kwao.
Alisema kujitokeza kwa wingi kwa wawekezaji kunatokana na sheria hiyo kuweka uwazi katika taratibu na kanuni za kuwekeza.
Biteko amesema lengo la wizara yake ni kuongeza uchangiaji wa sekta ya madini katika pato la taifa kutoka asilimia 4.8 ya mwaka jana hadi kufikia asilimia 10 kama Mpango wa Maendeleo wa miaka mitano unavyosema.
Chanzo: MCL