beth
JF-Expert Member
- Aug 19, 2012
- 3,877
- 6,326
Waziri wa Madini, Mhe. Dotto Biteko ameagiza kukamatwa msimamizi wa kiwanda wa kuchenjua dhahabu wa Ntolah Gold Elusion mkoani Mbeya baada ya kubaini utoroshaji wa dhahabu iliyochenjuliwa na kuamuru Jeshi la Polisi kufunga na kulinda kiwanda hicho
====
Waziri wa Madini, Doto Biteko leo Aprili mosi, 2019 amesimamisha uzalishaji wa dhahabu katika mtambo wa Ntolah Gold Elusion uliopo Chunya jijini Mbeya kwa kushindwa kutoa taarifa za uchenjuaji wa dhahabu kwenye mtambo huo.
Biteko amefanya ziara ya siku moja wilayani Chunya mkoani Mbeya kwa ajili kukagua shughuli za uchimbaji madini.
Baada ya kutembelea kwenye mtambo wa Ntolah, Waziri Biteko aligundua upotevu wa dhahabu gramu 30 bila taarifa sahihi kutoka kwa wahusika wa mtambo na wataalamu wa madini wilayani hapo.
"Mimi nina taarifa za mtambo huu kuzalisha dhahabu gramu 30 ninazo na uchenjuaji huo ulifanyika Machi 23, mwaka huu lakini cha ajabu zaidi wataalamu wangu hawana taarifa zozote juu ya uchenjuaji wa dhahabu hizi.”
“Naona kama hapa nachezewa, wataalamu nipeni taarifa sahihi, kamati ya ulinzi ya wilaya na mkoa nitawapa maelezo ili dhahabu isitoke kwenye mtambo huu." amesema Biteko.
Mbali na kusimamisha uchenjuaji dhahabu mtamboni hapo pia ameagiza kukamatwa msimamizi wa kituo hicho aliyefahamika jina moja la Mussa.
“Watalamu wa madini nipeni taarifa za uchenjuaji kwenye kituo hiki kabla sijaondoka zisingekuwa taratibu za utumishi ningewaweka ndani wote, haiwezekani dhahabu zipotee wakati nyie mpo, lakini ngoja niangalie taarifa mtakazonilitea nitatoa uamuzi,” amesema Biteko.
UPDATE:
Waziri wa Madini, Mhe. Dotto Biteko ameagiza kusimamishwa kazi wafanyakazi wote wa Ofisi ya Madini wilayani Chunya mkoani Mbeya kwa tuhuma za kushirikiana na wachenjuaji wa Madini kuiba na kutorosha dhahabu