Waziri wa Madini aagiza kukamatwa kwa msimamizi kiwanda cha kuchenjua madini, Ntolah Gold Elusion! Asimamisha kazi Watumishi ofisi ya madini Chunya

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Waziri wa Madini, Mhe. Dotto Biteko ameagiza kukamatwa msimamizi wa kiwanda wa kuchenjua dhahabu wa Ntolah Gold Elusion mkoani Mbeya baada ya kubaini utoroshaji wa dhahabu iliyochenjuliwa na kuamuru Jeshi la Polisi kufunga na kulinda kiwanda hicho
====
Waziri wa Madini, Doto Biteko leo Aprili mosi, 2019 amesimamisha uzalishaji wa dhahabu katika mtambo wa Ntolah Gold Elusion uliopo Chunya jijini Mbeya kwa kushindwa kutoa taarifa za uchenjuaji wa dhahabu kwenye mtambo huo.

Biteko amefanya ziara ya siku moja wilayani Chunya mkoani Mbeya kwa ajili kukagua shughuli za uchimbaji madini.

Baada ya kutembelea kwenye mtambo wa Ntolah, Waziri Biteko aligundua upotevu wa dhahabu gramu 30 bila taarifa sahihi kutoka kwa wahusika wa mtambo na wataalamu wa madini wilayani hapo.

"Mimi nina taarifa za mtambo huu kuzalisha dhahabu gramu 30 ninazo na uchenjuaji huo ulifanyika Machi 23, mwaka huu lakini cha ajabu zaidi wataalamu wangu hawana taarifa zozote juu ya uchenjuaji wa dhahabu hizi.”

“Naona kama hapa nachezewa, wataalamu nipeni taarifa sahihi, kamati ya ulinzi ya wilaya na mkoa nitawapa maelezo ili dhahabu isitoke kwenye mtambo huu." amesema Biteko.

Mbali na kusimamisha uchenjuaji dhahabu mtamboni hapo pia ameagiza kukamatwa msimamizi wa kituo hicho aliyefahamika jina moja la Mussa.

“Watalamu wa madini nipeni taarifa za uchenjuaji kwenye kituo hiki kabla sijaondoka zisingekuwa taratibu za utumishi ningewaweka ndani wote, haiwezekani dhahabu zipotee wakati nyie mpo, lakini ngoja niangalie taarifa mtakazonilitea nitatoa uamuzi,” amesema Biteko.

UPDATE:
Waziri wa Madini, Mhe. Dotto Biteko ameagiza kusimamishwa kazi wafanyakazi wote wa Ofisi ya Madini wilayani Chunya mkoani Mbeya kwa tuhuma za kushirikiana na wachenjuaji wa Madini kuiba na kutorosha dhahabu
 
Waziri wa Madini, Mhe. Dotto Biteko ameagiza kukamatwa msimamizi wa kiwanda wa kuchenjua dhahabu wa Ntolah Gold Elusion mkoani Mbeya baada ya kubaini utoroshaji wa dhahabu iliyochenjuliwa na kuamuru Jeshi la Polisi kufunga na kulinda kiwanda hicho

Sent using Jamii Forums mobile app
Kama mnaweka kodi kubwa bila kujali gharama zao za uzalishaji mtapata tabu sana.na mtawafungia wangapi?mwisho was siku hakuna mwekezaji atakuja haya matamko yenu bila kutumia njia sahihi bado hayatanufaisha nchi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
hivi Nimesoma sawasawa gram 30?

Sidhani kama ni gram 30. Tatizo ni kwamba waandishi wetu wa habari ni “reporters” kiasi kwamba hawatoi nafasi ya kushughulisha akili zao japo kuuliza maswali ya ufafanuzi (follow up questions).

Nakataa kuamini kwamba siku nzima mgodi unachenchua 30g. ...Pia nakataa kuaminishwa kwamba Mh. Biteko anaweza kuwa na roho ngumu kiasi hivyo kuwasimamisha watendaji wote wa idara kwa sababu ya discrepancy ya 30g.

Tafadhali vyombo vya habari hasa waandishi acheni kuchonganisha Viongozi na wananchi.
 
aisee gramu 30? hizo sasa ni bange, huyo doto 'per diem' yake ya hiyo safari ya Chunya tu ni kubwa kuliko thamani hizo gram 30 za dhahabu!
labda kama ni kilogramu 30.
 
hata cheni ya dhahabu inazidi gramm 30,lakini pia kama ni kilo 30 ni nyingi sana,Tatizo waandishi wetu wa habari sio makini kabisa

Nimeweka jedwali la bei ya leo sokoni
Tanzania Gold Price per Gram
Tanzania

Tanzania Gold Price | 24-hour gold rate live
Gold Rate in TZS
Tanzanian shilling
BidAskChange
Gold price per gram
Gold Price per gram in TZS96,046.2696,367.49-37.36
Gold Rate last update: Two Minutes Ago
(1 April 2019 14:46 UTC)
gold rate Tanzania
Gold Rates Tanzania
Gold Price per Gram [TZS]
in Tanzanian shilling
HighLowChange
Gold Rate per Gram 24k96,367.4996,768.7696,131.53-37.36
Gold Rate per Gram 22k88,465.3588,833.7288,248.75-34.30
Gold Rate per Gram 21k84,321.5584,672.6784,115.09-32.69
Gold Rate per Gram 18k72,275.6172,576.5772,098.65-28.02
Gold Rate per Gram 14k56,374.9856,609.7356,236.95-21.86
Gold Rate per Gram 10k40,185.2440,352.5740,086.85-15.58
Gold Rate per Gram 6k24,091.8724,192.1924,032.88-9.34
 
L
Kama mnaweka kodi kubwa bila kujali gharama zao za uzalishaji mtapata tabu sana.na mtawafungia wangapi?mwisho was siku hakuna mwekezaji atakuja haya matamko yenu bila kutumia njia sahihi bado hayatanufaisha nchi

Sent using Jamii Forums mobile app
Tunahitaji wawejezaji wajweli na sio wezi,hata nchi zinazotupatia misaada ieleweke wazi kuwa misaada hiyo inatokana na kodi za walipa kodi wa nchi husika.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom