Waziri wa Kilimo, Prof. Adolf Mkenda unaiyumbisha KNCU

Fred Mwakitundu

JF-Expert Member
Dec 31, 2018
227
383
Waziri wa Kilimo Profesa Adolf Mkenda amesababisha kuahirishwa mara mbili mkutano Mkuu wa Mwaka wa Chama Kikuu cha Ushirika mkoani Kilimanjaro(KNCU) kwa sababu zake binafsi mkutano uliopangwa kufanyika jana ukasogezwa mpaka leo lakini mkutano huo umefutwa tena leo na kusogezwa mpaka Jumatatu kisa Mkenda amebanwa na majukumu' yake.

Kimsingi Profesa Mkenda si mjumbe wa mkutano Mkuu wa KNCU na pili hata akiwepo kwenye huo mkutano atatambulika kama mwalikwa na si mgeni rasmi hoja kwamba ana jambo lake anataka atumie mkutano huo kufikisha ujumbe wake haina mashiko kwa sababu mkutano huo siyo wake na wajumbe wa mkutano mkuu ambao ndiyo wenye ushirika wao na kama ana jambo lake angeandaa mkutano wake mwenyewe wa kuzungumza na wanaushirika.

Anachokifanya Profesa Mkenda ni kutaka kuturudisha enzi za ujima ambako vyama vya ushirika viliendeshwa kwa kufuata maagizo ya wanasiasa chini ya mfumo wa chama kimoja na ndiyo maana wenye ushirika wao walikosa sauti ya kuusemea ushirika na ndiyo chanzo cha kuyumba kwa ushirika ambako wanasiasa walichangia kuua ushirika.

Lakini yote kwa yote hii inachangiwa na KNCU kuwa na Bodi dhaifu isiyokuwa na maamuzi pamoja na menejimenti ya KNCU chini ya Meneja wake bwana Massawe ambao wameshindwa kuitendea haki sheria ya ushirika iliyowaondoa wanasiasa kujihusisha na masuala ya ushirika kama ambavyo Prefesa Mkenda anajaribu kufanya jambo ambalo ni hatari kwa mstakabali wa ushirika.

Mkutano Mkuu wa KNCU ni muhimu kuliko Profesa Mkenda,ni mkutano unaotoa taswira ya KNCU kwani ni mkutano wa kusoma Taarifa ya fedha kwa mwaka wa fedha taarifa ambayo profesa Mkenda hana nafasi ya hata kuijadili na kutoa mapendekezo kwa sababu si mjumbe wa MKutano Mkuu bali ni mgeni mwalikwa tu,kwa hiyo kitendo cha kuupeleka mbele mkutano huo ni matumizi mabaya ya madaraka.

Wakati umefika kwa wanasiasa kuacha kuingilia masuala ya ushirika vinginevyo ushirika utakufa lakini ni muhimu kwa wanaushirika kuchagua bodi imara ambazo hazitayumbishwa na wanasiasa kama ambavyo Bodi ya KNCU chini ya mwenyekiti wake Cosmas Mushi inavyoyumbishwa na kusindwa kutoa maamuzi jambo ambalo linawaumiza wajumbe wa mkutano mkuu.

Kazi kwenu wanaushirika,mkikubali kuyumbishwa na wanasiasa jiandaeni kushuhudia anguko la ushirika

Laki
 
Back
Top Bottom