Kididimo
JF-Expert Member
- Sep 20, 2016
- 4,005
- 3,641
Katika hotuba ya Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi leo 19/05/2017 bungeni kuhusu bajeti ya 2017/2018,amesema, "Hadi kufikia Machi 2017 jumla ya tani 3,162.65 za nyama ziliuzwa nje ya nchi katika nchi za Dubai, Iraq na Vietnam ikijumuisha tani 711.82 za nyama ya mbuzi, tani 439.03 za nyama ya ng’ombe, tani 222.74 za nyama ya kondoo na tani 1,789.06 za nyama ya punda".
Kwa maoni yangu,hii ni fursa kwa wafugaji kuona punda sio tena mnyama kwa kazi tuu,bali anaweza kuingiza pato (fedha za kigeni) kwa kuuza nyama yake.
Hivyo, uwepo mkakati wa ,maksudi kuongeza na siyo kusitisha uuzaji wa nyama hiyo, kama alivyoshauri Waziri mwenye dhamana ya Mifugo. Inakadiriwa, Tanzania ina punda takriban 500,000 tu wanaopatikana katika mikoa mbalimbali.
Nini maoni yako?