Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi: Nyama ya punda inauzwa nje ya nchi zaidi kuliko ile ya ng'ombe

Kuwazalisha kwa wingi ni wazo zuri na ndo linalotakiwa kwa sasa lakini ikumbukwe kuwa kuzaliana kwa punda kunachukua muda mrefu sana hivyo ni vyema kuangalia namna nyingine ili wasijepotea kama walivyopotea wanyama wengine
Sawa. Punda hubeba mimba kwa miezi 12, wakati ngombe ni miezi 9. Kitaalamu, punda anaweza kuzaa mara 3 katika miaka 4. Haipishani mbali na ngombe wetu wa kienyeji wanaotunzwa vizuri. Chakula cha punda ni nafuu mara 5 au 6,ya kile cha ngombe! na haharibu mazingira kwa vile hula mabaki ya miti,masalia ya mazao nk yasiyo na thamani. Hula kidogo (1.4% ya uzito wake tofauti na ngombe 3.0%). Maji hunywa kidogo sana,ni mvumilivu.
Bei kwa kilo uzito akiwa hai ni kubwa kuliko ya ng'ombe!
Kwa ujumla, hii ni fursa ya uwekezaji.
 
Back
Top Bottom