Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi: Nyama ya punda inauzwa nje ya nchi zaidi kuliko ile ya ng'ombe

Kididimo

JF-Expert Member
Sep 20, 2016
4,017
3,655
Katika hotuba ya Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi leo 19/05/2017 bungeni kuhusu bajeti ya 2017/2018,amesema, "Hadi kufikia Machi 2017 jumla ya tani 3,162.65 za nyama ziliuzwa nje ya nchi katika nchi za Dubai, Iraq na Vietnam ikijumuisha tani 711.82 za nyama ya mbuzi, tani 439.03 za nyama ya ng’ombe, tani 222.74 za nyama ya kondoo na tani 1,789.06 za nyama ya punda".

Kwa maoni yangu,hii ni fursa kwa wafugaji kuona punda sio tena mnyama kwa kazi tuu,bali anaweza kuingiza pato (fedha za kigeni) kwa kuuza nyama yake.

Hivyo, uwepo mkakati wa ,maksudi kuongeza na siyo kusitisha uuzaji wa nyama hiyo, kama alivyoshauri Waziri mwenye dhamana ya Mifugo. Inakadiriwa, Tanzania ina punda takriban 500,000 tu wanaopatikana katika mikoa mbalimbali.

Nini maoni yako?
 
Ukicheka na wale vinyau wenye macho madogo watakwambia hata kinyesi cha binadamu kinaliwa kwao na kuanzisha usindikaji wa kinyesi ati kipelekwe Iraq, China n.k wakati kinazungushwa na kuuzwa hapa hapa. Kiukweli punda tunawala sisi wenyewe hapa hapa hata hawapelekwi nje. Dodoma si sehemu salama kula nyama ya ng'ombe kama wewe si mnyiramba.
 
Ukicheka na wale vinyau wenye macho madogo watakwambia hata kinyesi cha binadamu kinaliwa kwao na kuanzisha isindikaji wa kinyesi ati kipelekwe Iraq, China n.k wakati kinazungushwa na kuuzwa hapa hapa. Kiukweli punda tunawala sisi wenyewe hapa hapa hata hawapelekwi nje. Dodoma si sehemu salama kula nyama ya ng'ombe kama wewe si mnyiramba.
Kuna madhara yoyote ya kimwili kwa kula nyama ya punda? Pia sina uhakika kuwa wanauzwa hapahapa nchini. Kama kuna ushahidi ni vyema tujiridhishe.
 
Kama tu nguruwe hawana madhara ila kwa upande huu si mila na utamaduni kula punda kama wale tu wasiokula nguruwe.
Ushahidi wa nini wakati unaambiwa inaingiza foreign currency kwa national au unataka ugo and water zis government is not of sport sport Even though u tell the truth
 
Ukicheka na wale vinyau wenye macho madogo watakwambia hata kinyesi cha binadamu kinaliwa kwao na kuanzisha usindikaji wa kinyesi ati kipelekwe Iraq, China n.k wakati kinazungushwa na kuuzwa hapa hapa. Kiukweli punda tunawala sisi wenyewe hapa hapa hata hawapelekwi nje. Dodoma si sehemu salama kula nyama ya ng'ombe kama wewe si mnyiramba.
Teheteheee Wanyiramba wanakula punda?
 
....
....Nyama nyamaaa. .nyamaaa ya konokono...nyamaaa ...ya Mbwaaaa nyamaaa ..yapundamilia .......ya punda..babikiuuu
 
Toka jadi wanakula punda/nzowe hawa watani zangu. Mbali na punda wanagonga panya pia-mama yangu ni mnyiramba ila mimi nimekula panya tu wa kukaanga watamu aiseee
Inawezekana ndo maana idadi yao inazidi kupungua! Basi kuzuia nyama yake isiuzwe nje,kunaweza kusiwe na tija kubwa. Hivyo,inawezekana, tija ni kuongeza ufugaji na uzalishaji wake.
 
Watatoweka kwa kasi ya ajabu sana. Wachina wanamaliza punda kati ya kati tutazinduka wameisha kama tembo na ndipo tutakapojua tumepoteza lakini inakuwa too late. Leo hii ukisimama mpakani mwa Dodoma na Singinda hususani kati ya Manyoni na Bahi kuja kiwandani Dodoma utaona makundi ya mamia kwa mamia y a punda wakiswagwa kuja Dom kwa ajili ya kuchinjwa kwa siku itakuwa takriban punda 600-1000 wanapoteza uhai kama si kuwa katika eneo la machinjio tayari kwa kuchinjwa
 
Hoja yangu ni namna ya kuitumia hiyo fursa! Kama ng'ombe wako 28 M, na punda ni 0.5M,huku soka la nje la hao ngombe ni robo ya lile la punda,basi tuzalishe punda zaidi! Tuweke mkakati kwa kuanzisha mashamba ya kuzalisha punda kama yale ya kuzalisha ngombe ili tupate forex zaidi!
 
Jirani zetu Kenya,mwaka 2012 walipitisha sheria ya kutambua rasmi nyama ya punda kuwa haina madhara kwa mlaji,na ni nyama halali. Soko lake limeongezeka,kuna kiwanda kikubwa Nakuru,kinachinja hadi punda 600 kwa siku! Sehemu kubwa ya nyama yake inauzwa nje! Bei ya punda 1 imepanda hadi Ksh 8,000/=. Baadhi ya punda wanaochinjwa Kenya,wanatoka Tanzania.
 
Hoja yangu ni namna ya kuitumia hiyo fursa! Kama ng'ombe wako 28 M, na punda ni 0.5M,huku soka la nje la hao ngombe ni robo ya lile la punda,basi tuzalishe punda zaidi! Tuweke mkakati kwa kuanzisha mashamba ya kuzalisha punda kama yale ya kuzalisha ngombe ili tupate forex zaidi!
Kuwazalisha kwa wingi ni wazo zuri na ndo linalotakiwa kwa sasa lakini ikumbukwe kuwa kuzaliana kwa punda kunachukua muda mrefu sana hivyo ni vyema kuangalia namna nyingine ili wasijepotea kama walivyopotea wanyama wengine
 
Back
Top Bottom