Waziri wa kilimo mh. Chiza utaweza?

peace2007

JF-Expert Member
Oct 9, 2007
213
195
Ninafuatilia Kipindi cha Bunge cha maswali na majibu asubuhi hii hapo TBC 1 na nimemsikia WAZIRI Chiza wa Kilimo, Chakula na Ushirika akisema ule mswada mpya ya Ushirika uliopitishwa na Bunge miezi miwili iliyopita Rais ameshautia saini na kuwa Sheria.

Sheria hii pamoja na mambo mengine inaipa Mamlaka husika (CAG) kukagua mahesabu ya vyama vya Ushirika na pale itakapothibitika kuna ubadhirufu, kuwachukulia hatua za kisheria kwa wahusika ikiwemo KUFILISI mali zao.

Kuna tetesi ya kuwa Sheria hii itakuwa mwiba sana kwa wale waliotafuna pesa za vyama vya Ushirika na kabla ya kupitishwa na Bunge na kusainiwa na Rais, walifanya kila njia usipitishwe na jambo mojawapo ni kuhakikisha Waziri Chiza anang'olewa kwenye huo uwaziri na ilikaa mezani kwa Rais zaidi ya miezi miwili kabla ya kusainiwa.

SWALI LANGU, Mh. Chiza na Wizara yako na Serikali kwa ujumla utaweza kutekeleza kwa vitendo yaliyopo kwenye Sheria hiyo??? Kweli watu wabadhirifu watakamatwa na kufilisiwa?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom