Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,010
- 9,874
Waziri wa Kilimo, Prof. Adolf Mkenda amesema hatua ya Kenya kukataa mahindi ya kutoka Tanzania ni kinyume cha utaratibu wa makubaliano ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ya kibiashara.
Utaratibu wa kibiashara uliopo ni kuwa Kenya walitakiwa kupima kama mahindi yana madhara na walipaswa kuwasiliana na Shirika la Viwango la Tanzania (TBS) ili nao wapime kujiridhisha.
Serikali imeanza kuchukua hatua dhidi ya tatizo la mahindi kuzuiwa, aidha Sekretariet ya Jumuiya ya Afrika Mashariki imeingilia kati suala hilo.
Pamoja na hayo Waziri amekiri kuwa ni kweli tatizo la sumu kuvu lipo kwenye baadhi ya mazao ya Tanzania lakini tatizo hilo ni kubwa zaidi kwa mazao ya Kenya. Kiwango kilichopo kwa mazao ya Tanzania ni kidogo ambacho sio hatari kwa afya.
Pia soma