Waziri wa Kilimo asema Kenya imekiuka makubaliano ya EAC kuzuia mahindi ya Tanzania

Nyumisi

JF-Expert Member
Nov 10, 2010
7,129
2,000
Kwani wakenya kununua mahindi ya tanzania ni lazima ?
Siyo lazima, ndo maana serikali inabidi ije na plan ya namna ya kuzuia moja kwa moja mahindi kupelekwa kenya tusije kuwaua kwa sumu kuvu.

Badala yake tutafute masoko mbadala na kutumia mahindi ya ziada kuzalisha vyakula vya mifugo, yaani in the long run kusiwe na mahindi yanayopelekwa Kenya kutoka Tanzania na vivyo hivyo kusiwe na bidhaa yoyote itakayokuja Tanzania kutoka kenya. Yaani mbwai mbwai.
 

Gama

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
12,467
2,000
tatizo la sumu kuvu lipo kwenye baadhi ya mazao ya Tanzania lakini tatizo hilo ni kubwa zaidi kwa mazao ya Kenya. Kiwango kilichopo kwa mazao ya Tanzania
Huu ndio ukweli, ni vema serikali ya TANZANIA ingekaa kimya juu ya hili kwasababu licha ya uzalishaji mdogo wa nafaka uliopo kenya lakini mqzingira ya kenya yanazalisha more aflatoxin kuliko Tz because mazao haya hukaukia shambani na maeneo mengi ya kenya ni more humid kuliko mazingira similar ya Tanzania yanayozalisha mahindi. Kimsingi nadhani kenya wanatafuta namna ya kupata grains kwa bei nafuu zaidi kwakuwa wafanyabiashara wa TANZANIA+UGANDA wanapopeleka nafaka kenya huambiwa kuwa zina high levels za mycotoxins lakini hununuliwa na kuuzwa kwenye prime markets, ni hujuma za kitoto
 

Bila bila

JF-Expert Member
Dec 20, 2016
14,069
2,000
Yaani mtu kakataa kula mboga yako sababu umeweka pilipili, halafu kujitetea unamwambia mbona mboga anayoandaa yeye huwa ina pilipili zaidi ya hii yengu? What a Bogus Minister?
 

Nyumisi

JF-Expert Member
Nov 10, 2010
7,129
2,000
Huna akili, nyinyi ndo mlikimbia umande halafu unataka kulazimisha kujua kila kitu, ukijibiwa unaleta matusi. Haya mambo hayahitaji hasira, ni kwenda shule tu baaasi.
 

Ncha Kali

JF-Expert Member
Sep 19, 2019
9,760
2,000
Maana hiyo kama wamekuta sumu kwenye mazao yetu wanatakiwa kuendelea kuwaruhusu wananchi wao wale sumu hadi TBS itakajiridhisha? Je kama wakiruhusu wananchi wao kuyatumia halafu TBS wakakuta yana sumu, serikali iko tayari kubeba huo msalaba? Profesa mzima unatoa utetezi kama mtoto aliyishia darasa la pili.
Nina mtoto darasa la pili, hawezi kuwa mpuuzi kama huyu Profesa uchwara. Make radhi tafadhali.
 

Valuhwanoswela

JF-Expert Member
Jun 27, 2019
1,223
2,000
Ule ulikuwa ujinga na unyama wa hali ya juu maana vifaranga havikuwa na kosa lolote vingerudishwa vilikotoka, kama mahindi yana kuvu kwa nini alaumiwe mnunuzi na siyo muuzaji? Mkuki kwa nguruwe kwa Binadamu mchungu eh?
 

NewOrder

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
1,708
2,000
Umeona eh! Sijui Tanzania tumeingiza mahindi kutoka Kenya ili aweze kutoa data?? Yaani viongozi wetu hata coordinated response hawawezi!! Tatizo kuwa Kenya zaidi hakuondoi tatizo letu, ashughulike na yetu.
 

Zanzibar-ASP

JF-Expert Member
Nov 28, 2013
7,182
2,000
Na mkuu tunasikia yuko Kenya akitibiwa Covid na shambulizi la moyo.
Sasa sijui tushike lipi, hili la mahindi yenye sumu au mkuu kuumwa Covid?

Safari hii wakenya wametushika vibaya sana.
 

Deceiver

JF-Expert Member
Apr 19, 2018
6,909
2,000
Tulivyochoma vifaranga toka Kenya tulikua sahihi. Tulivyochoma Mara ya pili tulikua sahihi pia.
Tulipopiga mnada ng'ombe toka Kenya kilikua Ni kitendo Cha kiungwana. Kibaya Ni wao kukataa kununua?
 

Deceiver

JF-Expert Member
Apr 19, 2018
6,909
2,000
East Africa Community
Haitakaa Isimame Kamwe Kwa Aina Hii Ya Figisu Kila Uchao, Acha Tu Tuone
Wakenya hawana figisu. Nyie na roho zenu tu.
Tundu Lissu alipotaka kuuawa alienda kuponea NAIROBI HOSP akapona mpaka akagombea urais. Mhh ..... sasa ubaya wa wakenya uko wapi?
 

tweenty4seven

JF-Expert Member
Sep 21, 2013
13,308
2,000
Waziri wa Kilimo, Prof. Adolf Mkenda amesema hatua ya Kenya kukataa mahindi ya kutoka Tanzania ni kinyume cha utaratibu wa makubaliano ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ya kibiashara.

Utaratibu wa kibiashara uliopo ni kuwa Kenya walitakiwa kupima kama mahindi yana madhara na walipaswa kuwasiliana na Shirika la Viwango la Tanzania (TBS) ili nao wapime kujiridhisha.

Serikali imeanza kuchukua hatua dhidi ya tatizo la mahindi kuzuiwa, aidha Sekretariet ya Jumuiya ya Afrika Mashariki imeingilia kati suala hilo.

Pamoja na hayo Waziri amekiri kuwa ni kweli tatizo la sumu kuvu lipo kwenye baadhi ya mazao ya Tanzania lakini tatizo hilo ni kubwa zaidi kwa mazao ya Kenya. Kiwango kilichopo kwa mazao ya Tanzania ni kidogo ambacho sio hatari kwa afya.


Pia soma


View attachment 1721006
Huyo waziri nae ni mzigo kma kabudi,prof mzima anaropoka tu aendelee kufukuza nzige na mateke.
Mahindi ya sasa ni stock ya mavuno yaliyopita sasa kma yamewekewa dawa watu wayanunue tu?awamu hii imejaa maprof wa hovyohovyo hoja hujibiwa kwa hoja sio kelele
 

LESIRIAMU

JF-Expert Member
Feb 12, 2008
7,055
2,000
Ndio mkumbuke mlivyouwa wale vifaranga wao pale Namanga.
Swali rahisi,
Hivi ni lazima Kenya wanunue mahindi toka Tanzania? Maana hata huku mtaani kuna maduka ya Mchagga na Mpemba kila mtu huchagua pa kwenda.
Badala ya Wakenya kulalamika naona sisi wenye chakula ndio tuna lalamika. Kwani tulilima kwa ajili ya Wakenya?
 

MENGELENI KWETU

JF-Expert Member
Oct 23, 2013
9,456
2,000
Swali rahisi,
Hivi ni lazima Kenya wanunue mahindi toka Tanzania? Maana hata huku mtaani kuna maduka ya Mchagga na Mpemba kila mtu huchagua pa kwenda.
Badala ya Wakenya kulalamika naona sisi wenye chakula ndio tuna lalamika. Kwani tulilima kwa ajili ya Wakenya?
Inashangaza sana Mkuu..
Ni kama vile mwanamke kashakwambia hakutaki lakini wee unamng'ang'ania tu.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom