Waziri wa Kilimo asema Kenya imekiuka makubaliano ya EAC kuzuia mahindi ya Tanzania

Kwani wale vifaranga walikuwa na kosa gani masikini hadi kustahili ile adhabu ambayo kimsingi utolewa na mwenyezi Mungu?
 
Hii serikali mbona inasarakasi sana,Shigella anasema mahindi hayajazuiwa,mara hakuna taarifa yoyote rasmi kutoka kenya yakuzuia mahindi,leo waziri kaja na lake.

Endeleeni kubisha!
Wakenya wanasema kuwa watanzania tunajikoroga wenyewe
 
.........Pamoja na hayo Waziri amekiri kuwa ni kweli tatizo la sumu kuvu lipo kwenye baadhi ya mazao ya Tanzania lakini tatizo hilo ni kubwa zaidi kwa mazao ya Kenya. Kiwango kilichopo kwa mazao ya Tanzania ni kidogo ambacho sio hatari kwa afya.
Dah....huu mstari umebeba ujumbe mzito 🤭
 
East Africa Community
Haitakaa Isimame Kamwe Kwa Aina Hii Ya Figisu Kila Uchao, Acha Tu Tuone
Hii ni hatari kwa maendeleo ya EAC.

Ukingalia kwa jicho la tatu, kauli ya waziri Mkenda...maana yake anakusudia kulipiza kisasi kwa kupiga marufuku nidhaa/mazao kutoka Kenya alizosema zina sumu kuvu zaidi ya mahindi yetu.

Aina hii ya misuguano haina maslahi yoyote kwa wananchi wa kawaida.
 
Hizi ni kauli za mfamaji tu ;bora huyu kidogo amegusia sumukuvu ,ishu ni kenya ameshatuharibia soko la mahindi akikupiga ngumi ya kushoto wewe mtandike ya kulia alafu aliomuuma zaidi atatafuta jibu
 
Usiumize kichwa mkuu Watu washamjulia huyu Mr President huwa anapenda misifa isiyo na ukwel usishangae kina watu wakaandamana kwenda ubaloz wa kenya kushinikiza wakenya wanunue mahind yetu yenye sumu iili tuwaue. Vizur

Nchi ya maigizo Sana hii mkuu wa mkoa na wilaya n wakubwa kushinda mawazir mifano mnayo mingi tu Kama makonda na. Nape leo shigela na mkenda
Ha ha ha ha
 
Mkuu umeeleza vyema lakini chanzo cha michango isiyo na tija ukiisoma vyema chanzo ni watawala wetu ndani ya siku 3 kila mmoja anabwabwaja yake abbasi anasema hana taalifa shigela kauza mia saba na waziri analeta hoja ya kuwa kenya mahindi yao ndio yanatatizo zaidi,sasa je waziri ni muda muafaka kusema mahindi ya kenya ndio yanashida zaidi?

Jibu kwangu ni hapana & waziri angekuja na majibu kuwa mahindi yatauzwa kenya au la kama hayauzwi wamejipangaje kukabiliana na hali iliyopo ya kudoda mahindi baada ya kenya kugoma?maana hapa tunaitaji shot plan & long plani sasa ukisoma alichosema waziri hakitoi mwanga wa ufumbuzi wa tatizo kwa sasa
 
Waziri wa Kilimo, Prof. Adolf Mkenda amesema hatua ya Kenya kukataa mahindi ya kutoka Tanzania ni kinyume cha utaratibu wa makubaliano ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ya kibiashara.

Utaratibu wa kibiashara uliopo ni kuwa Kenya walitakiwa kupima kama mahindi yana madhara na walipaswa kuwasiliana na Shirika la Viwango la Tanzania (TBS) ili nao wapime kujiridhisha.

Serikali imeanza kuchukua hatua dhidi ya tatizo la mahindi kuzuiwa, aidha Sekretariet ya Jumuiya ya Afrika Mashariki imeingilia kati suala hilo.

Pamoja na hayo Waziri amekiri kuwa ni kweli tatizo la sumu kuvu lipo kwenye baadhi ya mazao ya Tanzania lakini tatizo hilo ni kubwa zaidi kwa mazao ya Kenya. Kiwango kilichopo kwa mazao ya Tanzania ni kidogo ambacho sio hatari kwa afya.


Pia soma


View attachment 1721006
Kwani wakenya kununua mahindi ya tanzania ni lazima ?
 
Hivi na sisi tunalishwa sumu kutoka kenya!,mbona hatujaambiwa!?tena bidhaa zao sina sumu kuliko zetu!?
 
Nani mkweli , RC wa Tanga aliyesema mahindi hayajazuiwa au Waziri wa Kilimo ?
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom