Waziri wa Kilimo asema Kenya imekiuka makubaliano ya EAC kuzuia mahindi ya Tanzania

kwani hadi useme direkti?
Mbona nimekwishajieleza vizuri tu kwa kirefu hapa hapa mkuu ki2c, kuhusu uamini wangu juu ya swala hili?

Kwa nini usinisome, halafu ndipo uhitimishe, kuliko kunishutumu tu bila kusoma nilyoandika?

Nisome, kama hukubaliani nami baada ya kunisoma, basi, tutajadili zaidi kama utapenda kufanya hivyo.
 
Ni bora umeishia na hiyo Mhhh!

Kikwete ni Mswahili, 'typical'.

Hawezi kuwa amesahau 'COW' alipokuwa nayasema hayo aliyoyasema ya "kiongozi mpuuzi...."

Je, na huko kwingine akitokea kiongozi "mpuuzi" je?, bado atakuwa anaendelea kushikilia huo "ushirikiano"?
 
Sasa mbona yule msemaji wa serikali anasema hana taarifa ya hiyo mambo. Mbona mnatuchanganya bana
 
Kwenye makubakiano ya EAC mlitakiwa kusaini mkataba kwamba bidhaa za chakula hazitakuwa na sumu kuvu...hamkufanya lolote!!

Sasa msitafute mchawi!! Zigo lenu hilo...Mahindi kuleni
wenyewe !!
 
Makubaliano hayakuwa kuuziana mahindi yenye sumu

Hao TBS wenyewe corrupt wametulisha vingi havifai
 
Sisi tulipovichoma moto vifaranga toka Kenya hatukukiuka makubaliano ya EAC? Tukumbuke vile vilikuwa viumbe hai.
 
Mkuki mchungu kwa nguruwe, vipi ile Sukari kutoka Zanzibar inapokataliwa kuingia Bara inakuwa hamujakiuka Makubaliano ya EAC? Au Zanzbar sio mwanachama ni Koloni tu la tanganyika?
 
Hivi mbona Hawa mawaziri, mkuu wa mkoa na msemaji wa serikali wanapishana Sana kwa kauli zao? Msemaji wa serikali kasema ati zuio lile la kikaratasi kile sio halisi kwani mipaka mingine shehena za mahindi zinaendelea kuingizwa nchini Kenya na bado kasisitiza kuwa Kuna mawasiliano ya kidiplomasia yameanzishwa! Kama kaidharau Ile barua ya katazo na kuiita kikaratasi haoni kuwa hayo mazungumzo yatapuuzwa kwa upande wa Kenya?

Nchi imekosa collective leadership kwa baadhi ya wizara na idara kuongozwa na watu wasioujua wajibu wa nafasi wanazozitumikia! Badala ya kupima mahindi kwenye maabara za kimataifa ili kujiridhisha wanabaki kufanya mipasho as if wapo kwenye ukumbi wa kitchen party! Aibu naona Mimi!
 
Mbona watu wengine mnashabikia upumbavu, mwaka 2004 wakenya 317 walilazwa hospitalini na 125 walifariki kutokana na kula mahindi yenye aflatoxin na hayo mahindi yalikuwa yamezalishwa na kuhifadhiwa na wakulima hao hao huko Kenya. Milipuko ya aflatoxin nchini kenya inatokea almost kila mwaka, mwaka 1981 kati ya wakenya 20 waliolazwa hospitali 12 walikufa kutokana na kula mahindi yenye viwango vya juu vya aflatoxin.

Waziri anaposema viwango vya aflatoxin vipo juu sana kwenye mazao ya kenya yupo sahihi kwa sababu mara zote mahindi yanayoleta milipuko ni yale yaliyozalishwa na kuhifadhiwa na wakulima wenyewe huko kenya. Wote tunajua ardhi yenye rutuba na maeneo yenye mvua nyingi huko kenya yanamilikiwa na mabwanyenye wachache wakiwemo wafanyabiashara na wanasiasa.

Kwa hiyo ardhi kame na isiyo na rutuba ndo inamilikiwa na hohe hahe na kwa sababu hawapewi mbinu bora za kilimo kuhusu aina ya mazao yanayostahimili ukame wanajikuta wanalazimisha kulima mahindi. Unapolima mahindi kwenye ardhi isiyo na rutuba na mvua zisizotabirika unatengeneza bomu la aflatoxin kwa sababu hayo mahindi hayataweza kuhimili kupambana na fangasi wanaozalisha aflatoxin kwenye mazao. Mnapoleta pumba zenu za kupinga kila kitu basi angalau muwe mko informed angalau kidogo na hilo jambo linalojadiliwa, shiiit!
 
Je Tanzania yakosa ushawishi ktk mikakati ya kidiplomasia eneo / kanda hii ya Afrika?

Je kama nchi sasa tutembee huku mabega yetu yakiwa yameteremka chini badala ya kutanua kifua mbele ktk masuala ya ushawishi kikanda na kimataifa ?

4 Mar 2019
Waziri wa Mambo ya Nje ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof Palamagamba Kabudi amewataka Watanzania kuwa wazalendo na nchi yao na kusema Tanzania hivi sasa sio nchi ya kusemwa na kudhihakiwa



..............................................................................


Tanzania tuna zaidi ya mabalozi 30 wanaotuwakilisha kimataifa, lakini balozi namba 1 na namba 2 ni nani?

Balozi namba 1
Mh. Magufuli na balozi namba 2 Prof. Palamagamba Kabudi hapa panaonesha kukosekana au kupungua nguvu ya ushawishi katika eneo hili la Geopolitics la EAC, maana haiwezekani mabalozi wetu hawa namba 1 na namba 2 juzi walishiriki kikao cha 21 cha Wakuu wa Nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki halafu siku chache zijazo jambo kubwa kama hili linajitokeza bila kufuata Taratibu na protocol za Jumuiya hii.

..............................................................................

N.B

Kumbukumbu toka kwa taarifa ya Msemaji Mkuu wa serikali 27 February 2021


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akishiriki mkutano wa 21 wa kawaida wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki unaofanyika leo tarehe 27 Februari, 2021 kwa njia ya mtandao.

Chanzo: Msemaji Mkuu wa Serikali

1614425639816.png
 
Back
Top Bottom