Waziri wa Kilimo asema Kenya imekiuka makubaliano ya EAC kuzuia mahindi ya Tanzania

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
3,835
2,000
Waziri wa Kilimo, Prof. Adolf Mkenda amesema hatua ya Kenya kukataa mahindi ya kutoka Tanzania ni kinyume cha utaratibu wa makubaliano ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ya kibiashara.

Utaratibu wa kibiashara uliopo ni kuwa Kenya walitakiwa kupima kama mahindi yana madhara na walipaswa kuwasiliana na Shirika la Viwango la Tanzania (TBS) ili nao wapime kujiridhisha.

Serikali imeanza kuchukua hatua dhidi ya tatizo la mahindi kuzuiwa, aidha Sekretariet ya Jumuiya ya Afrika Mashariki imeingilia kati suala hilo.

Pamoja na hayo Waziri amekiri kuwa ni kweli tatizo la sumu kuvu lipo kwenye baadhi ya mazao ya Tanzania lakini tatizo hilo ni kubwa zaidi kwa mazao ya Kenya. Kiwango kilichopo kwa mazao ya Tanzania ni kidogo ambacho sio hatari kwa afya.


Pia soma
 

bulicheka 4

JF-Expert Member
Mar 22, 2020
916
1,000
Kama Yanga huyu aseme hatujazuiwa ni magari yamezuiw Rc Tanga tumepitisha tani 570 tumuamini nani Yanga walisema Marefa Tff Uchawi sasa kocha na golikipa bado mashabiki kufukuzana
 

ryan riz

JF-Expert Member
Feb 17, 2015
279
500
Hivi Tanzania kuna serikali ngapi hasa huu upande wa Tanganyika? maana kila kiongozi anatoa taarifa anavyojua yeye! Huyu wamezuia, mwingine hawajazuia na magari yanapita kama kawaida, huyu yanasumu, mwingine yanasumu kidogo, yule mwingine wanatuonea wivu hii ni vita ya kiuchumi.

Daaaah nichoka kabsaa sasa sijui magazeti huwa yanaripoti vipi taarifa moja yenye maelezo tofautitofauti?
 

Peramiho yetu

JF-Expert Member
May 25, 2018
2,687
2,000
Hivi Tanzania kuna serikali ngapi hasa huu upande wa Tanganyika? maana kila kiongozi anatoa taarifa anavyojua yeye! huyu wamezuia,mwingine hawajazuia na magari yanapita kama kawaida,huyu yanasumu,mwingine yanasumu kidogo...
Usiumize kichwa mkuu Watu washamjulia huyu Mr President huwa anapenda misifa isiyo na ukwel usishangae kina watu wakaandamana kwenda ubaloz wa kenya kushinikiza wakenya wanunue mahind yetu yenye sumu iili tuwaue. Vizur

Nchi ya maigizo Sana hii mkuu wa mkoa na wilaya n wakubwa kushinda mawazir mifano mnayo mingi tu Kama makonda na. Nape leo shigela na mkenda
 

mkorinto

JF-Expert Member
Jun 11, 2014
24,087
2,000
TUKIWA TUNASUBIRI HATUA ZA UPANDE HUU SASA KWA BIDHAA ZA KENYA.

wacha tuendelee kuchapa kazi.

waziri kashaweka dash hapo kwenye"sumu iliyopo kwenye bidhaa za tz ni chache kulinganisha na ile iliyopo kwenye nafaka za kenya"
 

Wyatt Mathewson

JF-Expert Member
Dec 22, 2017
11,910
2,000
Hahahaa

Eti tatizo ni kubwa "zaidi" kwenye mazao ya Kenya kuliko kwetu..

Huyu professor naona analeta ujinga kwenye mambo serious....wanawake wa Uswahili wanachambana....

Hatujawahi kuona huu upumbavu the previous administrations,never
 

issenye

JF-Expert Member
Feb 2, 2011
3,438
2,000
Utaratibu wa kibiashara uliopo ni kuwa Kenya walitakiwa kupima kama mahindi yana madhara na walipaswa kuwasiliana na Shirika la Viwango la Tanzania (TBS) ili nao wapime kujiridhisha.
Maana hiyo kama wamekuta sumu kwenye mazao yetu wanatakiwa kuendelea kuwaruhusu wananchi wao wale sumu hadi TBS itakajiridhisha? Je kama wakiruhusu wananchi wao kuyatumia halafu TBS wakakuta yana sumu, serikali iko tayari kubeba huo msalaba? Profesa mzima unatoa utetezi kama mtoto aliyishia darasa la pili.
 

Hamatan

JF-Expert Member
Nov 10, 2020
1,909
2,000
Hivi serikali ya JMT ilipochoma wale vifaranga au walipotaifishawale ng'ombe toka Kenya na wamiliki kuwasweka ndani, na kisha kutaifisha ng'ombe wote, walishauriana kwanza na mamlaka za Kenya.

Tusijifanye tunajua sana utaratibu pale tunapoguswa, lakini tukawa wababe a kufanya chochote tutakacho inapowahusu wengine.

Awamu hii ya uongozi imeharibu sana mahusiano. Kubalini, anzeni upya, japo tayari hasara nyingi zimesababishwa na utawala wa awamu ya 5.

Namkumbuka yule Gavana wa Kenya alivyosema wakati akiwarudisha ng'ombe wa kutoka Tanzania waliokamatwa wakiwa ndani ya Kenya (sisi tulikamata ng'ombe 4,000 toka Kenya tukawataifisha. Kenya baada ya wiki 1 ikawakamata ng'ombe 9,000 toka Tanzania, wakawarudishia wafugaji wa Tanzania):

Masai ya Tanzania na masai ya Kenya ni ndugu, haina ugomvi. Yenyewe haina ugomvi. Utawala wa Magufuli ni aibu ya Afrika nzima. Unajifanya kifua mbele, kifua mbele na hiyo umaskini wako, itakufikisha wapi?"
 

Kalamu1

JF-Expert Member
Jul 7, 2018
11,038
2,000
Pamoja na hayo Waziri amekiri kuwa ni kweli tatizo la sumu kuvu lipo kwenye baadhi ya mazao ya Tanzania lakini tatizo hilo ni kubwa zaidi kwa mazao ya Kenya. Kiwango kilichopo kwa mazao ya Tanzania ni kidogo ambacho sio hatari kwa afya.
Sijui kama Prof. Mkenda kayasema haya, na kama kayasema, sijui alikusudia nini hasa! Kwa sababu Kenya kuwa na tatizo hilo hakufanyi bidhaa za Tanzania kuwa bora kama zimeonekana kuwa na sumu hiyo.

Kinachotazamwa hapa ni kiwango gani kilichomo kwenye sampuli iliyopimwa. Kama kiko juu ya kiwango kinachoruhusiwa, haijalishi, maana hata hizo bidhaa za Kenya zenye viwango vilivyo juu ya kiwango kinachokubalika bado zitakuwa hazifai.

Pamoja na yote, bado ninaheshima kubwa juu ya ufahamu na uwezo wa waziri wa maswala kama haya.
 

Kalamu1

JF-Expert Member
Jul 7, 2018
11,038
2,000
Maana hiyo kama wamekuta sumu kwenye mazao yetu wanatakiwa kuendelea kuwaruhusu wananchi wao wale sumu hadi TBS itakajiridhisha? Je kama wakiruhusu wananchi wao kuyatumia halafu TBS wakakuta yana sumu, serikali iko tayari kubeba huo msalaba? Profesa mzima unatoa utetezi kama mtoto aliyishia darasa la pili.
Ngoja nikukumbushe tu.

Unaona usivyokuwa na akili kwa andiko kama hili hapa?
 

Kennedy

JF-Expert Member
Dec 28, 2011
29,492
2,000
East Africa Community
Haitakaa Isimame Kamwe Kwa Aina Hii Ya Figisu Kila Uchao, Acha Tu Tuone
 

Kalamu1

JF-Expert Member
Jul 7, 2018
11,038
2,000
wewe unatakaje,Kenya waruhusu mahindi yenye sumu yaingie nchini mwao wananchi wadhurike au wayazuie wananchi wasidhurike?
Just imagine wewe ni mfanyakazi wa mamlaka ya chakula,si ungeua watu sana kwa sumu?
Ni wapi umenisoma nikisema hayo uliyoandika?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom