Waziri wa kilimo amsimamisha Mkurugenzi Mkuu wa bodi ya sukari

real G

JF-Expert Member
Feb 7, 2013
5,227
5,287
Waziri wa kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba amemuagiza Katibu mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Methew Mtigumwe kumsimamisha kazi mara moja Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Sukari Tanzania Ndg Henry J. Semwanza kuanzia leo Novemba 9, 2017.

Kwa agizo hilo lililotolewa na Waziri wa Kilimo Dkt Tizeba, Mkurugenzi huyo atatakiwa kurejea kwa mwajiri wake ambaye ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo kwa ajili ya kupangiwa kazi nyingine.

Simwanza anasimamishwa kazi kutokana na mwenendo wake wa utendaji akiwa Msimamizi Mkuu wa Bodi ya Sukari kutoridhisha.

Simwanza amehudumu katika nafasi hiyo akiwa Mkurugenzi wa Bodi ya Sukari tangu mwaka 2011.


Chanzo: Muungwana Blog
 
Maana sukari ilikutwa sh 5000, si mchezo. Kwa hiyo huyo jamaa aliyetumbuliwa anakula mshahara kama kawaida au sio?
 
New medicine for luxy servants is now available in every pharmacy closer to you
 
Kama ni yule Kingunge aliyejimilikisha Ubungo bus stand basi mtafute tu mkanywe naye chai wakati mkihangaika na hali yenu.
Huyu Kingunge unayemsema hapa ni mdogo wake wa "aliyegawa nyumba za serikali"
 
Sizonje na majaliwa ndio wametibua swala la sukari kwa kuleta ujuaji na wakakimbilia kuanzisha kiwanda cha magereza Vipi tena msala anapewa mnyonge wakati kiwanda hata uzalishaji haujaanza
 
Mara asimamishwe kazi Mara arejeshwe kwa Muajiri wake wa awali apangiwe kazi nyingine,
 
Bodi ya sukari inafanya kazi gani? Bodi ya chumvi je, maharage, mchele
 
Ninaimani msimu huu wa Magu hata wakina sie tunaoitwa wanyonge twaweza kupata wadhifa mkubwa serikalini maana sio kwa kutumbua tumbua huku
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom