Waziri wa Kazi na Ajira anza na hili la kikokotoo kwa wastaafu

Mnasihi

JF-Expert Member
Oct 9, 2013
7,657
6,909
Ikikupendeza Mh. Ndalichako tafadhali sana hebu kairejeshe sheria iliyoanzisha kikokotoo kwa wastaafu bungeni ili ifutiliwe mbali kwani ipo kinyume na haki za binadamu na ni kinyume cha katiba ya jamhuri ya Tanzania.

Jenga legacy kwenye wizara hii kwa kuifuta sheria hiyo kandamizi kwa wastaafu kama uliyoitendea haki wizara ya elimu.

Uzuri mmoja na faida kwako ni kuwa na naibu waziri katambi ambaye ni mwanasheria atakusaidia kukushauri juu ya ubatili wa sheria ya kikokotoo kwa wastaafu ili uharakishe kuipeleka bungeni kuifuta!

Nakutakia ufutaji mwema wa hiyo sheria.
 
... kwenye hilo huyo profesa hana msaada wowote; sahau! Hao jamaa ni arrogant sana usitegemee watasikiliza vilio vya tabaka la wavuja jasho as long as wao wana ma-package makubwa makubwa mtajua wenyewe huko.
Yes! Wao wanakula kwa urefu wa kwamba zao. Usitegemee akubali kamba yake ikatike kwa kutetea maslahi ya wastaafu.
 
Watu wachomwe moto tu...kuna mijitu mikatili zaidi ya Shetani

Tusitegemee jipyaa...
 
Ikikupendeza Mh. Ndalichako tafadhali sana hebu kairejeshe sheria iliyoanzisha kikokotoo kwa wastaafu bungeni ili ifutiliwe mbali kwani ipo kinyume na haki za binadamu na ni kinyume cha katiba ya jamhuri ya Tanzania...
Naungana na wewe kwa kusema hivi:

Prof, Joyce Ndalichako mimi binafsi nina imani na wewe.

Utendaji kazi wako kuanzia ulipokuwa baraza la mitihani ni wa kutukuka.

Nimefurahi kusikia umepelekwa wizara hii,naamini utaitendea haki.

wasalaam.
 
Ikikupendeza Mh. Ndalichako tafadhali sana hebu kairejeshe sheria iliyoanzisha kikokotoo kwa wastaafu bungeni ili ifutiliwe mbali kwani ipo kinyume na haki za binadamu na ni kinyume cha katiba ya jamhuri ya Tanzania...
Wanasheria waajiriwa serikalini huwa hawazingatii matakwa ya sheria bali wanazingatia matakwa ya bosi wao.
 
Yes! Wao wanakula kwa urefu wa kwamba zao. Usitegemee akubali kamba yake ikatike kwa kutetea maslahi ya wastaafu.
Nchi hii imelaaniwa kupitia Wanasiasa.

Mbunge miaka 5 akimaliza/staff Tshs. milioni 300 mafao.

Mtumishi wa Serikali akistaafu miaka 30-40:TShs milioni 80-100 mafao.

Mtumishi wa Shirika la umma akistaafu miaka 30-40: Tshs. Milioni 20-30.

Wote hawa unakuta kiwango cha elimu ni sawa na muda kazini ni sawa!

Double standards za kipuuzi sana!
 
Tuliopitia huo moto wa tanuru tunajus machungu tuliyoyapata. Kwa mtaji huu hata maprofesa wanajitosa huko ili walau wapate maslahi mazuri wanapomaliza kipindi Chao.
 
Back
Top Bottom