Waziri wa Katiba na Sheria Mwigulu Nchemba awajibu TLS kuhusu Rais Samia Suluhu kuteua Baraza jipya la Mawaziri

Sasa Mwigulu mbona kama anahofu na nafasi yake? Magufuli ameshakufa ni lazima serikali mpya iendelee. Sijaona point yake hapa
 
Mwigulu Nchemba ! Upo? Natamani sana utumbuliwe moja kwa moja awamu hii! Sasa sijui kama MAMA yetu atapata huo ujasiri!

Wengine ni PM, yule mwenzako wa afya, Kabudi, Bashungwa (huyu hata kupiga dana dana sijui kama anaweza! Halafu eti ni Waziri wa michezo!), Kibabu George Mkuchika, Doto James, Ole Sabaya, na wengineo wengi!! Nyinyi mlikubuhu kwa unafiki, kujikomba komba na pia kumpotosha Mzee enzi za uhai wake.
Maderu hana nafasi tena ya kuendelea kuwepo kwenye uwaziri
 
Kama kuna watu wanatakiwa kutemwa kwenye Baraza la Mawaziri basi ni huyu Mwigulu Nchemba, jitu lenye roho mbaya kuwahi kutokea
 
Katiba inasema ndani ya saa 24 mpaka 48 Rais awe ameapishwa, na hili limefanyika kwa mujibu ya katiba. Tayari nchi ina Rais (amiri jeshi mkuu)

Ni upumbavu uliopitiliza kuanza kujadili teuzi zingine wakati Rais na nchi iko kwenye`maombolezo na mwili haujazikwa bado.

Subira huvuta heri
 
Nimesoma andiko la TLS, kwa heshima zote kwa chombo chetu hiki kilichopewa mamlaka kisheria, Nimeshtuka sana, I wish to say,

Kwanza KATIBA HAIJAVUNJWA KWA MHE RAIS SAMIA SULUHU kuapa, na wala hakuna Mkanganyiko wowote wa Kikatiba, kwa yeye kutoteua PM na Baraza jipya. Mmekaa wote kweli mkaona hivyo.

Kwa mujibu wa Katiba Ibara ya 42(5) kuna watu wa aina mbili wanaweza kuwa Rais. Moja, Rais Mteule ambaye anatokana na Ibara ya 42(1). Mbili, Mtu anayeshika kiti cha Rais ambaye anatokana na ibara ya 37(5) na 50(2)(d) ambaye ni Makamu wa Rais. Kwa Mazingira haya, Makamu wa Rais, baada ya kifo cha Rais, anakuwa Kaimu Rais baadae ndio ameapa na kuwa RAIS wa Nchi. Rais Mteule anapatikana kutokana na uchaguzi. Hivyo basi ibara ya 57(2)(f) ya Katiba haitumiki katika mazingira haya. Kwa mjibu wa Sheria, Mhe Rais alitakiwa kutoa taarifa hii kwenye Baraza la Mawaziri baada ya kuapa na alifanya hivyo, maana yake Baraza lipo.

Hata hivyo kwa tamaduni za Kiafrika, kitanzania na Misingi ya UTU, SIONI KAMA NI JAMBO JEMA SANA KUANZA KUJADILI MGAWANYO WA MADARAKA TUNGALI HATA HATUJAMZIKA ALIYEKUWA KIONGOZI WETU. HUU SIO MSIBA MDOGO, JAMBO HILI ZITO LIKO MIKONONI MWA RAIS WETU MAMA SAMIA SULUHU, HALAFU SISI TUANZE KUMPATIA MAMBO YA MARA TEUA PM, MARA VUNJA BARAZA, KATIBA INAELEKEZA RAIS KUAPA NA NAMNA YA KUMPATA MAKAMU WA RAIS.

KWA MJIBU WA KATIBA RAIS ANARUHUSIWA KUVUNJA BARAZA MUDA WOWOTE NA KUPANGA ATAKAVYO HATA SIO KWA MAZINGIRA KUAPA KWAKE,

KWANINI HATUIONI HEKIMA YAKE YA KUSHUGHULIKIA MSIBA KUMSITIRI KWANZA ALIYEKUWA KIONGOZI WETU? TUNAANZA NA MAZISHI AU MIRATHI? 😭😭😭😭

Pia soma > TLS: Kwa Mujibu wa Katiba, sasa Tanzania haina baraza la Mawaziri, Rais Samia atakiwa kuteua Waziri Mkuu ndani ya siku 14
Mtu anajigonga jamani. Waziri Miami ati maana unalinda biashara za watu ati.
 
Dah! Mwigulu kama anajua tupo kwenye msiba mzito ametoa wapi nguvu ya kuandika haya? Hapa ninachokiona ni namna ya kujipigia debe ili asiachwe kwenye baraza lijalo. Hakuna chochote cha msingi alichokiongea. TLS wametoa mwanga kuhusu issue nzima ya kikatiba kuhusu hali iliyopo, sasa hapa Mwigulu hata haieleweki anaongea nini.
Nadhani kea Sasa issue ya msiba ndo ya msingi haya mengi ni baada ya kumzika kwanza Mzee wetu.Haraka ya nn pia wakati mwingine wanasheria wanakuwa wababaishaji na hujifanya wanajua sana.sheria ni nn tusubiri mengine yaishe kwanza.
 
Huyu mama Samia asipoiga udikteta wa jiwe kwa hizi siku mbili tatu watampasua kichwa kwa maushari na makelele kitoka kila kona,hawa TLS walikuwaga wapi kipindi kile Jiwe linaikanyaga Katiba na kufanya neno lake kuwa sheria
Leo hii ndio wamekuwa vimbele mbele kweli...
 
Back
Top Bottom