Waziri wa Katiba na Sheria: Mahakimu wenye elimu ya astashahada na stashahada kufutwa kazi

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,899
Waziri wa Katiba na Sheria Mh.Dkt Harrison Mwakyembe amesema serikali itawafuta kazi Mahakimu wote wa mahakama za mwanzo wenye elimu ya cheti na diploma ya sheria.

“Tunahitaji mahakimu wenye uwezo wa sheria ambao wamehitimu shahada ya kwanza, hivyo serikali inaandaa utaratibu wa kuwafuta kazi mahakimu wote wenye elimu ya cheti na diploma”

Katika kikao kijacho cha Bunge, Serikali inakusudia kupeleka bungeni na kusoma kwa mara ya kwanza Muswada wa Sheria ya msaada wa Kisheria (The Legal Aid Bill), ambao pamoja na mambo mengine utaruhusu watu wasio na taaluma ya sheria lakini wenye uzoefu na masuala ya kisheria (Paralegals) kutoa msaada wa kisheria, kwa mujibu wa kifungu cha Kifungu 10(1)d(ii) na (iii).

Maana yake ni kwamba ikiwa muswada huu utapita na kuwa sheria, it means wale watu wasio na taaluma ya sheria lakini wanajishughulisha kwa namna moja au nyingine na mambo ya kisheria (mnawaita Bush Lawyers) watatambulika rasmi na watapewa fursa ya kutoa msaada wa kisheria katika baadhi ya masuala ya kijamii.

Nini maoni yako??
 
Waziri wa Katiba na Sheria Mh.Dkt Harrison Mwakyembe amesema serikali itawafuta kazi mahakimu wote wa mahakama za mwanzo wenye elimu ya cheti na diploma ya sheria.
“Tunahitaji mahakimu wenye uwezo wa sheria ambao wamehitimu shahada ya kwanza, hivyo serikali inaandaa utaratibu wa kuwafuta kazi mahakimu wote wenye elimu ya cheti na diploma”
HEHEHE.....hatari sana
 
Waziri wa Katiba na Sheria Mh.Dkt Harrison Mwakyembe amesema serikali itawafuta kazi Mahakimu wote wa mahakama za mwanzo wenye elimu ya cheti na diploma ya sheria.

“Tunahitaji mahakimu wenye uwezo wa sheria ambao wamehitimu shahada ya kwanza, hivyo serikali inaandaa utaratibu wa kuwafuta kazi mahakimu wote wenye elimu ya cheti na diploma”
Mwakyembe sio mtu wa mchezomchezo
 
Mimi nitamuona mwanaume kama atawatimu JWTZ na polisi wenye vyeti feki ....

Bila hivyo nitaamini ni moto Wa mabuwa tu....

kuangaika na wafanyakazi wenye elimu ya chini ni kuwaonea tu........

Akumbuke pia yeye alitokea kwenye Diploma.......
 
Picha tafadhali!
IMG-20161020-WA0003.jpg
 
Back
Top Bottom