Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Balozi Augustine Mahiga akana Tanzania kujitoa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,790
4,425
Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Augustine Mahiga amekanusha taarifa za Serikali kujitoa katika Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu (AfCHPR)

Akifafanua zaidi kuhusu dai hilo, Dkt. Mahiga anasema serikali haijajitoa katika Mahakama hiyo isipokuwa imeiandikia barua Mahakama hiyo kuondoa itifaki ambayo inapingana na sheria ya Tanzania.

Anaongeza kuwa, endapo marekebisho hayo ya itifaki yasipofanyiwa kazi na Mahakama hiyo ndipo Serikali itajiondoa lakini kwa sasa Serikali haijajitoa kama inavyosemekana.

Miongoni mwa shughuli za Mahakama ya Haki za Binadamu na Watu ni kusikiliza kesi zinazofunguliwa na Mashirika yasiyo ya Kiserikali na Watu dhidi ya Serikali.

Aidha, Miongoni mwa kesi za Tanzania zilizowahi kuamuliwa katika Mahakama hiyo ni pamoja na kesi ya Mwanamuziki maarufu aitwaye Nguza Viking maarufu kama Babu Seya na Mwanaye Johnson Nguza maarufu kama Papi Kocha.

Hata hivyo, Dkt. Mahiga hakuweka bayana kipengele chenye utata katika itifaki hiyo na kuwataka waandishi wamuulize Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

1575279761916.png

======
Dar es Salaam. Waziri wa Katiba na Sheria, Balozi Augustine Mahiga amesema Serikali haijajitoa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu (AFCHPR) bali imeiomba kubadilisha itifaki.

Alisema uamuzi wa kujitoa utakuja baada ya ombi la kubadilisha itifaki hiyo yenye utata katika shughuli za kimahakama kushindikana.

Alisema Serikali imeiandikia barua mahakama hiyo yenye makao makuu yake jijini Arusha kuondoa itifaki hiyo ambayo inapingana na sheria ya Tanzania na kusisitiza kuwa kwa sasa haijajitoa bali inasubiri marekebisho hayo.

“Tunachosubiri kwa sasa ni marekebisho hayo ila ikishindikana basi tutajitoa. Kwa sasa bado hatujajitoa kama inavyosemekana,” alisema.

Miongoni mwa shughuli za mahakama hiyo ni kusikiliza kesi zinazofunguliwa na mashirika yasiyo ya kiserikali au wananchi dhidi ya Serikali.

Mpaka sasa nchi tisa kati ya 30 zilizoridhia itifaki hiyo zimesaini kuwapa uhuru huo wananchi wake kudai haki zao mahakamani pindi Serikali inapowatendea kinyume. Zilizosaini Benin, Burkina Faso, Ivory Coast, Gambia, Ghana, Mali, Malawi, Tanzania na Tunisia.

Zilizoridhia ni Algeria, Burundi, Cameroon, Chad, Comoros, Kongo, Gabon, Kenya, Libya, Lesotho, Msumbiji, Mauritania, Mauritius, Nigeria, Niger, Rwanda, Jamuhuri ya Kidemokrasia Sahrawi, Afrika Kusini, Senegal, Togo na Uganda.

Miongoni mwa kesi za Tanzania ambazo zimewahi kuamriwa kwenye mahakama hiyo ni ya mwanamuzi maarufu Nguza Viking maarufu kama Babu Seya na mwanaye Johnson Nguza au Papii Kocha.

Babu Seya na wanaye walihukumiwa kufungwa maisha na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mwaka 2004. Walikata rufaa Mahakama Kuu wakashindwa, Mahakama ya Rufani ikawaachia huru watoto wawili lakini Babu Seya mwenyewe na Papii Kocha wakaendelea kutumikia adhabu hiyo.

Mwaka 2015 walikimbilia katika mahakama hiyo na Machi 23, 2018 ikakubali kukiukwa kwa baadhi ya haki zao hivyo kuamuru waachiwe ingawa walishapata msamaha wa Rais.

Kwenye maelezo yake Dk Mahiga hakueleza kipengele chenye utata katika itifaki hiyo bali alitaka aulizwe Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Chanzo: Mwananchi

Pia Soma:

Siasa zinatuendesha vibaya kwenye hii nchi na tuna watu wenye upeo mdogo!! .. mijitu humu ilikuwa inafurahia na inakejeli Jambo ambalo nimeshindwa kuelewa ni msimamo wa wananchi!,Ni kwamba tumesimama kisiasa kuliko kimaendeleo na ndio maana kila Jambo baya litakaloipata serikali watu wanafurahia!! Taarifa za hovyo zinavumishwa na makandokando mengi.. Kuna mahali hapako sawa.
 
Kipengele muhimu cha mtu binafsi kuishitaki nchi kwenye mahakama ya Afrika kikiondolewa hiyo mahakama itabaki jengo tu la kujikinga na mvua.
 
Siasa zinatuendesha vibaya kwenye hii nchi na tuna watu wenye upeo mdogo!! .. mijitu humu ilikuwa inafurahia na inakejeli Jambo ambalo nimeshindwa kuelewa ni msimamo wa wananchi!,Ni kwamba tumesimama kisiasa kuliko kimaendeleo na ndio maana kila Jambo baya litakaloipata serikali watu wanafurahia!! Taarifa za hovyo zinavumishwa na makandokando mengi.. Kuna mahali hapako sawa.
Tatizo Jiwe
 
Umewahi kishughulisha ubongo wako japo kidogo ilikujua tumefikaje hapo
Siasa zinatuendesha vibaya kwenye hii nchi na tuna watu wenye upeo mdogo!! .. mijitu humu ilikuwa inafurahia na inakejeli Jambo ambalo nimeshindwa kuelewa ni msimamo wa wananchi!,Ni kwamba tumesimama kisiasa kuliko kimaendeleo na ndio maana kila Jambo baya litakaloipata serikali watu wanafurahia!! Taarifa za hovyo zinavumishwa na makandokando mengi.. Kuna mahali hapako sawa.
 
Akifafanua zaidi kuhusu dai hilo, Dkt. Mahiga anasema serikali haijajitoa katika Mahakama hiyo isipokuwa imeiandikia barua Mahakama hiyo kuondoa itifaki ambayo inapingana na sheria ya Tanzania.
Hata hivyo, Dkt. Mahiga hakuweka bayana kipengele chenye utata katika itifaki hiyo na kuwataka waandishi wamuulize Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Kwa nini hataki kutaja kipengele kinachokinzana na Sheria zetu? Kwa vyo vyote vile kitakuwa kinaibana Serikali!
Sasa Mahiga bila kukitaja kipengele hicho cha itifaki ni kipi anakuwa ameongea na kupinga kama layman yeyote mfano wa Lusinde au Musukuma.
Naona mwana diplomasia anathibitisha yale yanayosemwa kwa kutumia diplomasia ya hali ya juu-kutuchanganya-bado ukweli unasimama kuwa serikali ina nia ya na wamesha amua kujitoa huko. Balozi anataka tuwaone kuwa wako makini lakini wanajua hatima ya hili. Sasa yeye atashindwaje kujua hiyo itifaki ni ipi-anajua na anajua wanatupeleka wapi. HAHA UTAWALA BORA ala CCM-BASHIRU UPO na Polepole. Wapi Kabudu mtaalamu wa sheria? Baba unatupeleka sote jalalani?
 
Ukiona hivyo ujue wananchi hawana imani na serikali.
Siasa zinatuendesha vibaya kwenye hii nchi na tuna watu wenye upeo mdogo!! .. mijitu humu ilikuwa inafurahia na inakejeli Jambo ambalo nimeshindwa kuelewa ni msimamo wa wananchi!,Ni kwamba tumesimama kisiasa kuliko kimaendeleo na ndio maana kila Jambo baya litakaloipata serikali watu wanafurahia!! Taarifa za hovyo zinavumishwa na makandokando mengi.. Kuna mahali hapako sawa.
 
Dar es Salaam. Waziri wa Katiba na Sheria, Balozi Augustine Mahiga amesema Serikali haijajitoa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu (AFCHPR) bali imeiomba kubadilisha itifaki.

Alisema uamuzi wa kujitoa utakuja baada ya ombi la kubadilisha itifaki hiyo yenye utata katika shughuli za kimahakama kushindikana. Alisema Serikali imeiandikia barua mahakama hiyo yenye makao makuu yake jijini Arusha kuondoa itifaki hiyo ambayo inapingana na sheria ya Tanzania na kusisitiza kuwa kwa sasa haijajitoa bali inasubiri marekebisho hayo.

“Tunachosubiri kwa sasa ni marekebisho hayo ila ikishindikana basi tutajitoa. Kwa sasa bado hatujajitoa kama inavyosemekana,” alisema.

Miongoni mwa shughuli za mahakama hiyo ni kusikiliza kesi zinazofunguliwa na mashirika yasiyo ya kiserikali au wananchi dhidi ya Serikali. Mpaka sasa nchi tisa kati ya 30 zilizoridhia itifaki hiyo zimesaini kuwapa uhuru huo wananchi wake kudai haki zao mahakamani pindi Serikali inapowatendea kinyume. Zilizosaini Benin, Burkina Faso, Ivory Coast, Gambia, Ghana, Mali, Malawi, Tanzania na Tunisia.

Zilizoridhia ni Algeria, Burundi, Cameroon, Chad, Comoros, Kongo, Gabon, Kenya, Libya, Lesotho, Msumbiji, Mauritania, Mauritius, Nigeria, Niger, Rwanda, Jamuhuri ya Kidemokrasia Sahrawi, Afrika Kusini, Senegal, Togo na Uganda. Miongoni mwa kesi za Tanzania ambazo zimewahi kuamriwa kwenye mahakama hiyo ni ya mwanamuzi maarufu Nguza Viking maarufu kama Babu Seya na mwanaye Johnson Nguza au Papii Kocha. Babu Seya na wanaye walihukumiwa kufungwa maisha na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mwaka 2004. Walikata rufaa Mahakama Kuu wakashindwa, Mahakama ya Rufani ikawaachia huru watoto wawili lakini Babu Seya mwenyewe na Papii Kocha wakaendelea kutumikia adhabu hiyo. Mwaka 2015 walikimbilia katika mahakama hiyo na Machi 23, 2018 ikakubali kukiukwa kwa baadhi ya haki zao hivyo kuamuru waachiwe ingawa walishapata msamaha wa Rais. Kwenye maelezo yake Dk Mahiga hakueleza kipengele chenye utata katika itifaki hiyo bali alitaka aulizwe Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
 
Sasa amekanusha nini hapo..?
Au ndio kama ACT wazalendo wanamuuliza waziri wa afya swali la kusema kama barua ya NHIF ni halisi au feki anaishia kuzunguka mbuyu! Kwanini wajitoe sasa hivi, waliingiaje!?
Kibaya hii mahakama inatuletea heshima kama miongoni mwa waasisi wake na tukifanya hivi inakuwa sio.
 
Back
Top Bottom