Waziri wa JK ahenyeshwa na Mratibu wa Kata

Mwana Mpotevu

Platinum Member
Sep 7, 2011
3,295
2,500
Hapa ndipo unapoona watendaji wa chini wanapokuwa na dharau kwa uongozi wa serikali ya JK

Naibu waziri wa JK atunishiwa msuli na Mratibu wa Kata

Atunishiwa msuli na Mratibu Elimu Kata
*Ni baada ya kumzuia kugombea uongozi CCM

NAIBU Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI-Elimu), Kassim Majaliwa, ameonja machungu ya uongozi, baada ya kutunishiwa msuli na Mratibu wa Elimu wa Kata ya Mvumi Mission, Charles Ulanga, kutokana na kuzuiwa kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa CCM wa kata hiyo.

Lakini pamoja na Waziri Majaliwa kutoa kauli hiyo, Mratibu huyo amesema atagombea nafasi hiyo, kwa sababu ni haki yake ya kikatiba.

Akitoa ufafanuzi kuhusiana na uamuzi wake, Waziri Majaliwa alisema kitendo cha mratibu kugombea nafasi hiyo ni kukiuka sheria.

Licha ya kauli hiyo, mratibu huyo amechukua fomu kwa mara nyingine kwa ajili ya kutetea nafasi yake hiyo ya uenyekiti.

Waziri Majaliwa, alisema nafasi ya Uratibu Elimu Kata, ni kazi ya kila siku ambayo haipaswi kuambatana na shughuli za kisiasa.

“Kitendo cha Mratibu Elimu Kata kugombea nafasi katika Chama Cha Mapinduzi (CCM), ni kwenda kinyume na kanuni za utumishi.

“Haiwezekani akaweza kutenda haki kwa watu anaowaongoza na wala hatotenda haki kwa mwajiri wake, kwa kuwa katika harakati za kisiasa ni lazima ataacha nafasi moja na kutumikia zaidi nafasi nyingine,” alisema Majaliwa.

Alisema Mkurugenzi wa Halmashauri, ana wajibu wa kutoa majibu ya mratibu kuhusu mratibu huyo kutumikia nafasi katika chama, wakati ni muajiriwa wa halmashauri.

Malalamiko ya kugombea kwa Ulanga katika nafasi hiyo, yalikuja baada ya baadhi ya walimu anaowaongoza kuandika barua kwa Katibu wa CCM Wilaya ya Chamwino, kupinga jina lake, kupitishwa kwa madai kuwa kiongozi wao huyo hawatendei haki.

Pamoja na mambo mengine, barua hiyo ilimtaka mratibu huyo kuchagua nafasi moja, kwani kutaka nafasi zote zinapunguza ufanisi wake wa kazi.

Kwa upande wake mgombea huyo, alisema anayo haki ya kugombea na ana haki pia ya kuchaguliwa kwa ajili ya kuwaongoza, huku akitolea mfano wa Rais kwamba licha ya majukumu mengi, lakini bado ni mwenyekiti wa CCM.

“Haya ni majungu tu yanayotengenezwa dhidi yangu na mimi nitaendelea kugombea na wanachama ndio wenye haki ya kumchagua mtu au kutokumchagua, lakini suala la kazi haliwezi kunizuia kuendelea na harakati zangu za kisiasa,” alisema.

SERIKALI YA JK, KAZI IPO
 
ni dalili pia ya kupotea kwa heshima ya watendaji wadogo kwa mabosi wao wateule wa JK
 
Hajakosea JK ni rais na Mwenyekiti wa Chama tawala. Kama yeye "anaweza", huya mratibu atashindwaje kwenye kata?
 
Wote si ni magamba kwanini wasikae wakajadili pamoja wakatoka fresh au wametofauttiana gamba nyoka na mwingine kenge?
 
Namfahamu Mr Ulanga,huwezi mtenganisha na siasa,iko damuni.Hata pale Kigwe alikuwa akifanya siasa na uratibu at a time.Lakini kama asemavyo ni haki yake kikatiba
 
Namfahamu Mr Ulanga,huwezi mtenganisha na siasa,iko damuni.Hata pale Kigwe alikuwa akifanya siasa na uratibu at a time.Lakini kama asemavyo ni haki yake kikatiba

lakini kubishana live na waziri kunataka moyo sana
 
ni haki yake kikatiba,tatizo la wateule wa jk wanapokea maagizo ya ridhiwan ya nani agombee sababu dogo anapanga safu kwa ajili ya urais 2015 kwa maelekezo ya dingi kulida mali zao za wizi watakapokuwa nje ya ofisi...mafisadi wakubwa
 
Namfahamu Mr Ulanga,huwezi mtenganisha na siasa,iko damuni.Hata pale Kigwe alikuwa akifanya siasa na uratibu at a time.Lakini kama asemavyo ni haki yake kikatiba

ni haki yake kikatiba lakini pia aelewe kwamba kama mtumishi wa umma haruhusiwa kugombea nafasi ya kisiasa,akabakia ni mtumishi wa umma! Achague kati ya uongozi wa kisiasa ama wa umma. Waziri yupo sahihi!
 
Kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na miongozo mbalimbali kwenye Utumishi wa Umma ikiwa ni pamoja na Standing Orders for Public Service ya mwaka 2009 Mtumishi wa Umma haruhusiwi kushika nafasi yoyote ya Kisiasa ama kwa kuchaguliwa kuteuliwa lakini anaruhusiwa kushiriki shughuli za vyama vya siasa ikiwa ni pamoja na mikutano. Kwa mara ya kwanza nampongeza Majaliwa kwa kusimamia ukweli hasa kwa kuwa hiyo nafasi ya Kata haina athari yoyote kwa Majaliwa. Wana JF tujifunze kusoma sheria za nchi badala ya kushabikia vitu ambavyo ukweli uko wazi. Hii ndio iliyomtoa Prof Baregu pale Mlimani na wengi humu tulilalamika kwamba ameonewa, sasa huyu ni Mwana CCM tumpongeze Waziri na Tumwambie aendelee kuwaondoa wana CCM wote waliopo kwenye Utumishi wa Umma na wana madaraka kwenye Chama. Wote tunakumbuka kwamba alipoteuliwa kugombea Uenyekiti wa UVCCM Masauni Hamad Masauni alilazimika kuacha kazi Wizara ya nishati na madini na hata yule Kashindye wa Chadema Igunga aliacha kazi tyake ya Afisa Elimu (W). Huyo Mratibu kama mnampenda mwambienni atapaoteza kazi na maslahi yake kijinga kazi ya kujifanya kushinda na sheria
 
ni haki yake kikatiba lakini pia aelewe kwamba kama mtumishi wa umma haruhusiwa kugombea nafasi ya kisiasa,akabakia ni mtumishi wa umma! Achague kati ya uongozi wa kisiasa ama wa umma. Waziri yupo sahihi!
Nimetafuta kitufe cha Like sijaiona, bais ngoja niseme "Gerrard says senkyu for zis yuziful post". Ndivyo utaratibu ulivyo
 
ni haki yake kikatiba,tatizo la wateule wa jk wanapokea maagizo ya ridhiwan ya nani agombee sababu dogo anapanga safu kwa ajili ya urais 2015 kwa maelekezo ya dingi kulida mali zao za wizi watakapokuwa nje ya ofisi...mafisadi wakubwa

hahahahaha punguza hasira
 
ni haki yake kikatiba lakini pia aelewe kwamba kama mtumishi wa umma haruhusiwa kugombea nafasi ya kisiasa,akabakia ni mtumishi wa umma! Achague kati ya uongozi wa kisiasa ama wa umma. Waziri yupo sahihi!

That's what I was thinking before. Lakini if that being he case, how comes mtendaji wa chini kimajukumu anapata nguvu za kubishana na waziri wake kuhusu jambo lililo wazi na kuonyesha kama waziri kasalimu amri? ni sababu yuko CCM? ni sababu ya udhaifu wa watendaji kutokujua taratibu? au ni tatizo la mfumo mzima kuparaganyika?
 
Back
Top Bottom