Waziri wa JK aanza fitina za urais 2015 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waziri wa JK aanza fitina za urais 2015

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nickname, Dec 16, 2010.

 1. nickname

  nickname JF-Expert Member

  #1
  Dec 16, 2010
  Joined: Dec 20, 2009
  Messages: 516
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 45
  Mwandishi Wetu

  [​IMG]Mkakati wake wa kwanza ni kuivuruga UVCCM
  [​IMG]
  Akifanikiwa ataanza kupanga safu uongozi Wazazi, UWT
  [​IMG]
  Awaita Dar kimya kimya wenyeviti wa mikoa wa UVCCM


  WAZIRI katika Baraza la Mawaziri la sasa ambaye katika Awamu ya Kwanza ya Rais Jakaya Kikwete alikuwa naibu waziri, ameanza kujipanga kuwania urais mwaka 2015, akianza kujenga mtandao ndani ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) na tayari ameanza mpango wa kuwakusanya baadhi ya wenyeviti wa mikoa wa umoja huo ili washinikize mabadiliko ya uongozi yatakayomnufaisha, Raia Mwema limebaini.

  Gazeti hili limethibitishiwa kuwa waziri huyo ameitisha mkutano wa siri wa baadhi ya wenyeviti wa UVCCM wa mikoa watakaokutana Dar es Salaam Desemba 20, wiki ijayo, ili pamoja na mikakati mingine washinikize kupatikana kwa mwenyekiti wa UVCCM waliyemwandaa kutoka Zanzibar.


  Kwa sasa nafasi ya mwenyekiti wa UVCCM inashikiliwa kwa kukaimu na Makamu Mwenyekiti wa umoja huo, Benno Malisa, baada ya aliyekuwa Mwenyekiti, Hamad Yusuf Masauni kuachia ngazi kutokana na kudanganya kuhusu umri wake.

  Kwa mujibu wa habari zilizotufikia waziri huyo ameamua kutumia mbinu za pembeni zilizo kinyume na taratibu za UVCCM na CCM kwa ujumla ili kufanikisha mkakati wake ikielezwa katika kundi lake la harakti za kusaka urais, yeye ni kati ya watarajiwa kama mtarajiwa mkuu atashindwa kusafishika kutokana na jamii kuamini kuwa si mtu wa maadili safi na tayari amehusishwa katika kashfa kubwa za kitaifa ndani ya miaka mitano iliyopita.


  Habari hizo zinabainisha kuwa ili afanikishe mkakati huo ameanza kwa kuvuruga UVCCM. Ameanza katika umoja huo kwa imani kuwa viongozi wa sasa wakuu ambao ni Makamu Mwenyekiti, Beno Malisa, akisaidiwa na Katibu Mkuu, Martin Shigela hawamuungi mkono na hawana dalili za kufanya hivyo.


  Malisa aliingia madarakani Novemba 14, 2008 na baadaye kukaimu uenyekiti uliokuwa chini ya Masauni ambaye alijikuta katika kashfa ya umri iliyounguruma mwaka jana mjini Iringa, akidaiwa kughushi tarehe ya kuzaliwa wakati akiomba nafasi hiyo kwa kutaja alizaliwa Oktoba 3, 1979 wakati ukweli ni kwamba alizaliwa Oktoba 3, 1973.

  Kwa upande wake, Shigela aliteuliwa na Kamati Kuu ya CCM kuwa Katibu Mkuu wa UVCCM Februari 28, mwaka jana. Taarifa zaidi zinabainisha kuwa tayari waziri huyo ili kufanikisha mkakati wake, amewaita kwa siri wenyeviti wa UVCCM wa mikoa yote nchini jijini Dar es Salaam na kupanga kufanya nao kikao Desemba 20.


  Hata hivyo, uchunguzi wa gazeti hili umeshindwa kuthibitisha moja kwa moja juu ya nani atakayekigharamia kikao hicho na kiasi cha fedha kitakacholipwa kwa waalikwa huku uchunguzi zaidi ukibaini kuwa viongozi rasmi wakuu wa UVCCM, Malisa na Shigela wamekataa kuhusishwa na kikao hicho.

  Gazeti hili lilizungumza na baadhi ya wenyeviti wa UVCCM wa mikoa ambao pamoja na kuthibitisha kuwapo kwa kikao hicho Dar es Salaam, wameweka bayana kuwa ni kwa ajili ya kutathmini mchakato wa Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani Oktoba 31, mwaka huu. Aidha, baadhi ya wenyeviti hao wamekiri kutaarifiwa kuwapo kwa uchaguzi wa Mwenyekiti wa UVCCM Taifa.

  Hata hivyo, wakati juhudi za kufanikisha mkutano huo zikiendelea kwa siri imebainika kuwa mkutano husika utakuwa kinyume cha kanuni za UVCCM ambazo zinaweka wazi kuwa, wenyeviti wa ngazi zote huchaguliwa na wajumbe wa mkutano mkuu wa ngazi husika na si wenyeviti na kwamba, mikutano yote hiyo huandaliwa na Baraza Kuu la UVCCM kwa kila ngazi husika.


  Hadi tunakwenda mitambani, Katibu Mkuu wa UVCCM, Shigela na Naibu Katibu Mkuu wake Athman Kizigo, hawakupatikana kuzungumzia suala hilo.

  Kwa upande mwingine, mpango huo wa siri umezusha upinzani mkali na tayari baadhi ya maofisa waandamizi wa UVCCM wanasema haiwezekani wenyeviti wa mikoa wafanye kikao cha kitaifa cha kutathmini Uchaguzi Mkuu wakati kazi hiyo ilipaswa kufanywa na Baraza Kuu la Taifa la UVCCM kwa kuzingatia Ibara ya 89(m) ya kanuni ya umoja huo inayotumika sasa.

  "Lakini pia hawawezi kufanya tathmini ya kitaifa, iwe kwa vyeo vyao na hata vinginevyo, wakati bado katika mikoa yao wenyewe hawajakutana kwanza kwa ajili hiyo," kinasema chanzo kimoja cha habari hizi na kuongeza:

  "Kama wanalijua hilo, lazima baraza kuu la kila mkoa lifanye tathmini kwanza, ndipo tathimini hizo zitumwe Makao Makuu ya UVCCM na hatimaye kazi hiyo ifanywe na wajumbe wa Baraza Kuu la Taifa wanaotajwa katika Ibara ya 88(a) hadi (p) ya kanuni zetu, na vikao vyote vinakwenda kwa utaratibu maalumu."

  Watu walioko karibu na waziri huyo kijana wanaeleza kuwa uamuzi wake unalenga si tu kujiwekea mazingira bora ya urais yeye na kundi lake lakini pia unalenga kuwadhibiti Malisa na Shigela.

  "Malisa, kwa waziri huyo anaonekana kuwa kikwazo kinachoweza kumfanya asiwe Rais wa Serikali ya Awamu ya Tano mwaka 2015, ndiyo maana hajashirikishwa," kinasema chanzo kingine.

  Vyanzo vyetu vya habari kutoka kundi la mkakati la waziri huyo vinamtaja mtu aliyeandaliwa kuwa mwenyekiti wa UVCCM ili kulinda maslahi ya waziri huyo kuwa ni Mjumbe wa Baraza Kuu la Taifa la UVCCM kutoka Zanzibar ambaye ametajwa kwa jina moja la Jamal.

  Hata hivyo, uchunguzi zaidi umebaini kwamba Ofisi ya Katibu Mkuu wa UVCCM haifahamu chochote kuhusu uchaguzi huo wa mwenyekiti Taifa, hali inayopambanua kuwa mpango huo mzima ni kinyume cha Ibara ya 89(b) ya Kanuni ya UVCCM.


  Wakati Ofisi ya Katibu Mkuu ikiwa haina taarifa rasmi, baadhi ya Wakuu wa Idara za Makao Makuu ya UVCCM, wakiwamo wabunge wa Viti Maalumu kupitia umoja huo wanatajwa kuwa sehemu ya mpango huo wa siri wakifanya hivyo ili kulipa fadhila. Wabunge hao wa viti maalumu wanatajwa kusaidiwa na waziri huyo ambaye aliwahi kuwa kiongozi mwandamizi wa UVCCM kupata nafasi walizonazo sasa.


  "Baadhi ya wabunge hao walibebwa sana kisiasa na (anatajwa waziri huyo) hadi wakafika hapo walipo sasa, hivyo wanachofanya ni kumrudishia fadhila bila ya kujali kuwa jambo hilo kwa kweli lipo nje ya kanuni zetu," anasema mmoja kati ya wenyeviti wa mikoa bila kutaka jina lake litajwe.

  Hata hivyo, utekelezaji wa mkakati huo wa siri wa kumpachika Jamal kuwa Mwenyekiti wa Taifa wa UVCCM kuchukua nafasi ya Masauni ni wa muda kabla ya kupisha awamu nyingine ya mkakati husika. Inaelezwa kuwa Jamal atadumu kwenye uenyekiti hadi 2013 ili kumpisha mdogo wa waziri huyo ambaye jina la ukoo wake lilianza kusikika kwenye siasa za Tanzania kuanzia kwa baba yake aliyekuwa kada maarufu katika CCM.


  Mdogo wa waziri huyo atapachikwa nafasi hiyo katika wakati ambao atakuwa amehitimu masomo katika moja ya vyuo vikuu mikoa ya Kanda ya Ziwa.


  Tayari inatajwa kuwa Mwenyekiti huyo mtarajiwa wa UVCCM kuanzia mwaka 2013, alikuwa Zanzibar hivi karibuni kwa lengo la kuwahamasisha wenyeviti wa mikoa ya Tanzania Zanzibar kuhudhuria mkutano huo uliopangwa kufanyika siku yoyote kuanzia Jumatatu wiki ijayo.

  Utekelezaji wa mpango huo pia unahusisha uteuzi wa Makatibu wa Mikoa wa UVCCM watakaomtii kwa kila jambo atakaloagiza mwenyekiti huyo mpya kwa maslahi ya waziri husika na kwamba makatibu hao mwaka 2015 watakuwa pia ni Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa wa CCM tayari kupiga kura kuteua mgombea urais wa Tanzania.

  Mbali na kuweka Makatibu wa Mikoa vibaraka, kazi nyingine iliyopangwa na waziri huyo katika Mkutano Mkuu wa Taifa wa UVCCM wa mwaka 2013 ni kuhakikisha mdogo wake anasimikwa uenyekiti wa UVCCM Taifa.

  Wengine watakaochaguliwa kwa ajili hiyo ni mjumbe mmoja wa mkutano mkuu wa Taifa wa CCM kutoka kila mkoa wa Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar ili kukidhi Ibara ya 104(z) ya Katiba ya CCM Toleo la Mwaka 2010.

  Hayo yanatajwa kuwa ni mazingira yanayomhakikishia waziri husika uwingi wa kura katika mkutano mkuu wa CCM wa 2015 utakaoteua mgombea urais kwa tiketi ya CCM.


  Sehemu nyingine ya mkakati au mpango wa waziri huyo baada ya kuvuruga UVCCM ni kujipenyeza na kupanga safu zake katika jumuiya nyingine za CCM ambazo ni Umoja wa Wazazi na Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), sambamba na kupanga safu ya wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa wa CCM kupitia jumuiya hizo tatu zinazotajwa na Ibara ya 128(1)(a) – (c) ya katiba ya chama hicho tawala.

  Malisa na Shigela ambao ndio viongozi wa juu zaidi katika UVCCM kwa sasa, wanaelezwa kuwa na msimamo tofauti na waziri huyo, wakidaiwa kutokuwa tayari kugeuzwa vibaraka na baadhi ya wanasiasa wenye uchu wa urais, ambao tayari wanajipanga ili kusaka ushindi kwa njia zozote zile ziwe halali au haramu.

  Wachambuzi wa masuala ya siasa za ndani ya CCM, wakiwamo baadhi ya wastaafu wanasema endapo siasa chafu zilizopangwa kufanywa na waziri huyo zitafanikiwa, CCM itaingia Uchaguzi Mkuu ujao ikiwa hoi.


  Wanasema wazi kwamba endapo chama hicho kitapitisha jina la waziri huyo, ambaye kwa mujibu wao hafai hata kwa nafasi hiyo aliyonayo, CCM ijiandae kuwa chama cha upinzani baada ya Uchaguzi Mkuu wa 2015.
   
 2. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #2
  Dec 16, 2010
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Emmanuel Nchimbi?
   
 3. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #3
  Dec 16, 2010
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,519
  Likes Received: 1,689
  Trophy Points: 280
  Dakta Emmanuel.......unautaka uprezidaa??? Wewe na EL tofauti yenu ni majina tu
   
 4. HIMO ONE

  HIMO ONE Senior Member

  #4
  Dec 16, 2010
  Joined: Sep 6, 2010
  Messages: 129
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Haituhusu

  Sio issue

  Ruksa
   
 5. nickname

  nickname JF-Expert Member

  #5
  Dec 16, 2010
  Joined: Dec 20, 2009
  Messages: 516
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 45
  Anaweza kuwa Emmanuel Nchimbi,Matayo David Matayo au Ezekiel Maige.Hawa ndio mawaziri wa sasa waliokuwa manaibu waziri serikali iliyopita.Mwenye data azilete
   
 6. HIMO ONE

  HIMO ONE Senior Member

  #6
  Dec 16, 2010
  Joined: Sep 6, 2010
  Messages: 129
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kawaida
   
 7. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #7
  Dec 16, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  fitna za akina malisa na uvccm wote

  wameharibu a very productive ccm wing kwa siasa za majitaka, inasikitisha sana kuona vijana badala ya kufanya kazi au kusoma. wako bize kuangalia nani anatishia mkate wangu..

  too sad
   
 8. S

  Silas A.K JF-Expert Member

  #8
  Dec 16, 2010
  Joined: Apr 23, 2008
  Messages: 807
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  ni huyo huyo uliyemtaja ndiye anayezungumziwa hapo
   
 9. macho_mdiliko

  macho_mdiliko JF-Expert Member

  #9
  Dec 16, 2010
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 6,434
  Likes Received: 2,303
  Trophy Points: 280
  Ndio maana nasema Mkapa alikuwa rais mbovu kuliko wote. Alikaa kama boga mpaka watu hopeless na mindless kama Kikwete wakanunua urais... sasa ona hata na mizoga nayo inaanza kufurukuta...inajiona nayo inaweza kununua urais.....Ati Nchimbi???? Huu ni mzaha mbaya sana kwa Watanzania....
   
 10. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #10
  Dec 16, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Du kweli Tanzania zaidi ya uijuavyo, yaani hata Nchmbi ana ndoto ya uraisi?
   
 11. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #11
  Dec 17, 2010
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Ni Nchimbi kaka ila anashirikiana na kupewa support na kina EL na RA, hapa ni kuweka akiba kama mzee (ELY atashindwa kujisafisha
   
 12. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #12
  Dec 17, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  B Membe
   
 13. Deodat

  Deodat JF-Expert Member

  #13
  Dec 17, 2010
  Joined: Sep 18, 2008
  Messages: 1,279
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  Kile kipande kinachosema huyo jamaa aliwahi kuwa kiongozi mwandamizi wa UVCCM nafikiri kinanifanya niamini kuwa huyo kwenye red hapoi ndio muhusika!
   
 14. Deodat

  Deodat JF-Expert Member

  #14
  Dec 17, 2010
  Joined: Sep 18, 2008
  Messages: 1,279
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  Kama ndio huyu basi urais umegeuka mat*ko, kila mtu anataka kuwa nayo! huyu naye awe rais wetu? cum..on!
   
 15. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #15
  Dec 17, 2010
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Nyamaza kweli Tanzania nyamaza, nyamaza tu usilie!!

  Kuna miaka inakuja ambapo kiongozi wa kueleweka mbele na nyuma ATAPATIKANA KWA NJIA YA SIASA ZA USHINDANI wa kweli kuongoza. Nakuhakikishia wale wote wenye NJAMA KUBWA KUKUCHUNA KAMA BUZI kamwe hawatokua na nafasi tena ya KUJIPANGIA RAIS ZAIDI YA MIAKA kumi kabla ya wakati.

  Tanzania kweli nakuahidi juu ya hili. Kamwe hautokaa UKABAKWA NA MINAJISI kwenye 'chaguzi KARATA TATU'. Hii ndio maana WANAO SOTE tunapigania KATIBA MPYA itakayowazuilia mbali MIFISI YOTE wa nchi hii inayojaribu kukuhodhi na KUKUBAKA bila kupenda kwako.

  Tanzania naomba uamini ninachokuambia hapa hivi sasa, jambo linalowafanya WANA-MNADA WA KUCHUUZA URAIS NCHINI KWA KUTEGEMEA AMA UKUBWA ZAIDI DAU AU UJIRANI WA UNDUGU WA KURITHISHIANA UFALME na kudiriki kusema wazi wazi kwamba hamna haja ya mabadiliko KAMILI isipokua viraka vya hapa na pale ni kutokana na ukweli kwamba sisi wanao TUMEBAINI SIRI ZOTE ZA UBAKAJI wao kwako kila mara bila huruma.

  Tanzania, 2015 chuya na mchele wote watapembuliwa kwa KIPIMO SAWA bila ya UMASHUHURI WA MTU WALA wala fedha zake. Hivyo Mama Mpendwa Tanzania ukisikia WATU KAMA WANYAMA nchi hii huko mbele ya safari basi moja kwa moja ujue kwamba VIJANA wako tutakua tumejitolea kukupigania na KUKUKINGA NA DAMU ZETU sisi wenyewe ili hii mijina ya ajabu ajabu isije IKAKUBAKA TENA mbele ya macho yetu kama ilivyofanyika 2010.
   
 16. m

  moma2k JF-Expert Member

  #16
  Dec 17, 2010
  Joined: Dec 12, 2010
  Messages: 953
  Likes Received: 984
  Trophy Points: 180
  Anaye faa ni Nahodha, siyo mafisadi hawa wa Tanzania bara.
   
 17. afroPianist

  afroPianist Member

  #17
  Dec 17, 2010
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 86
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Naona ndugu zetu wa visiwani nao sasa wameona ni zamu yao, kweli ni haki yao na ingependeza rais angetoka ZBR(kama yupo mwenye sifa kuliko wagombea wote) lakini shida inakuja tu ktk upigaji kura, kwamba mtu kama nahodha hata akipitishwa na CCM, je anakubalika pia na umma wa Tz Bara?

  2005 mlipoteza nafasi adimu kwa ujinga na ubaguzi wa viongozi wenu, kwa kumkataa Salim(probably the best president Tanzania never had),ambaye anakubalika sana hata huku bara. Inabidi mjipange upya na mrekebishe kasoro hizo kabla ya kufikiri tu kuwa ni "zamu yetu".
   
 18. Sinkala

  Sinkala JF-Expert Member

  #18
  Dec 17, 2010
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 1,505
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Azikate zile nywele sasa, zimekuwa ndefu sana!
   
 19. maishapopote

  maishapopote JF Gold Member

  #19
  Dec 17, 2010
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 1,998
  Likes Received: 955
  Trophy Points: 280
  Amina Chifupa
  Ippy malecela
  ...................
  ...................
  mh atupata tu huo uraisi......no one to stop him...
   
 20. B

  Bobby JF-Expert Member

  #20
  Dec 17, 2010
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,682
  Likes Received: 197
  Trophy Points: 160
  Kwani huyo aliyeko madarakani ana tofauti gani na huyo mwenye PhD fake? Hii ndio Tanzania mtu yeyote anaweza kuwa rais awe na uwezo wa kuongoza ama asiwe nao, uwezo si kigezo TZ. What matters doesn't matter in Tanzania and the opposite is also very true. Ingekuwa urais ni issue serious Tanzania jmk asingekuwa magogoni sasa hivi.Let's face it jamani hapa ndipo tulipofika kama nchi period.
   
Loading...