Waziri wa Habari tueleze TCRA inafanya kazi gani ya maana

Hismastersvoice

JF-Expert Member
Jan 26, 2013
18,587
22,185
Hii TCRA kwa watanzania hatuoni kazi yoyote ya maana inayotufanyia wananchi, imeshindwa kuhakikisha usajiri wa laini za simu unatimiza lengo lake. Mimi ni mmoja kati ya wengi tuliosajiri laini za simu na kupewa namba ya uthibitisho, cha ajabu unajikuta laini imefungwa kwa kukosa usajiri!

Zipo laini nyingi tu za matapeli zinatumika bila kikwazo, badala yake tinatupiwa mzigo wa kutakiwa kutoa taarifa tupigiwapo na matapeli! Tunanunua vifurushi vya ving'amuzi cha ajabu ghafla unakuta baadhi ya chaneli zimeondolewa baada ya kuzilipia! Unauziwa muda wa maongezi na bando ya mitandao ya simu, unachoahidiwa sicho utakacho kipata!

Matangazo ya redio ni vurugu tupu huku baadhi ya stesheni huingiliana au kutosikika vizuri na stesheni za TV ndiyo kabisa makelele matupu bila ya mpsngilio!Haya yote na matendo ya utapeli ambayo TCRA ingetakiwa kuyazuia lakini imeyabariki! Waziri wa habari ni waziri ambaye anaishi kwa kupata mshahara kivulini kwani hasikiki kabisa.
 
Waziri inabidi utoe ufafanuzi kuhusu malalamiko ya wananchi wengi kuhusiana na utapeli unsofanywa na makampuni ya simu na ving'amuzi.
 
Back
Top Bottom