OgwaluMapesa
JF-Expert Member
- May 24, 2008
- 10,942
- 428
Sakata la TBC Kuonyesha muziki wa Taarab na Vodacom miss Tanzania kufanyika wakat Taifa likiwa limegubikwa na Janga / Msiba mkubwa wa kitaifa limechukua sura mpya baada ya waziri wa habari na michezo emanuel Nchimbi kutakiwa ajiuzulu mara moja .''vodacom na waziri Nchimbi ubinadamu ni zero ni bora kushuudia walimbwende na mikogo ya kuhingia kuliko kuonyesha utu . Visingizio vya kupata hasara suala la Michezo kutokuwa miongoni mwa masuala ya muhungano'' ni matusi na Dharau kwa watanzania
Mpaka saa moja jioni kituo cha Televisheni cha Taifa (TBC) Kilikuwa kinaonyesha watu wakicheza muziki wa Congo ,wanawake wakikatika viuno na hata ngoma za kienyeji.Si dharau kwa watanzania tu bali ni tusi kwa Rais Kikwete na Makamu wa Rais Dr Bilal.Makamu wa Rais na Rais wamejitahidi sana wameonyesha uongozi wa Dhabiti katika juhudi za uhokoaji .Ikumbukwe Rais Kikwete alifuta ziara yake huko canada ziara iliyokuwa imeandaliwa muda mrefu na kwa Gharama kubwa ,Lakini Rais aliona ni vema kufuta ziara kuliko kuwa nje ya Nchi na kutangaza siku 3 za maomboleza
Waziri Nchimbi kushindwa kusimamia na kutekeleza maelekezo ya Rais ya 3 ya maombolezo ni dharau na matusi kwa Watanzania Wote na kwa mabosi wake Rais Kikwete na Makamu wa Rais.Kwa mantiki hizo zote kwa busara za kawaida tena pasipo shuruti waziri Nchimbi ajiuzulu mara moja