Waziri wa Habari na Michezo Emanuel Nchimbi atakiwa kujiuzulu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waziri wa Habari na Michezo Emanuel Nchimbi atakiwa kujiuzulu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by OgwaluMapesa, Sep 12, 2011.

 1. O

  OgwaluMapesa JF-Expert Member

  #1
  Sep 12, 2011
  Joined: May 24, 2008
  Messages: 10,948
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Sakata la TBC Kuonyesha muziki wa Taarab na Vodacom miss Tanzania kufanyika wakat Taifa likiwa limegubikwa na Janga / Msiba mkubwa wa kitaifa limechukua sura mpya baada ya waziri wa habari na michezo emanuel Nchimbi kutakiwa ajiuzulu mara moja .''vodacom na waziri Nchimbi ubinadamu ni zero ni bora kushuudia walimbwende na mikogo ya kuhingia kuliko kuonyesha utu . Visingizio vya kupata hasara suala la Michezo kutokuwa miongoni mwa masuala ya muhungano'' ni matusi na Dharau kwa watanzania

  Mpaka saa moja jioni kituo cha Televisheni cha Taifa (TBC) Kilikuwa kinaonyesha watu wakicheza muziki wa Congo ,wanawake wakikatika viuno na hata ngoma za kienyeji.Si dharau kwa watanzania tu bali ni tusi kwa Rais Kikwete na Makamu wa Rais Dr Bilal.Makamu wa Rais na Rais wamejitahidi sana wameonyesha uongozi wa Dhabiti katika juhudi za uhokoaji .Ikumbukwe Rais Kikwete alifuta ziara yake huko canada ziara iliyokuwa imeandaliwa muda mrefu na kwa Gharama kubwa ,Lakini Rais aliona ni vema kufuta ziara kuliko kuwa nje ya Nchi na kutangaza siku 3 za maomboleza

  Waziri Nchimbi kushindwa kusimamia na kutekeleza maelekezo ya Rais ya 3 ya maombolezo ni dharau na matusi kwa Watanzania Wote na kwa mabosi wake Rais Kikwete na Makamu wa Rais.Kwa mantiki hizo zote kwa busara za kawaida tena pasipo shuruti waziri Nchimbi ajiuzulu mara moja
   
 2. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #2
  Sep 12, 2011
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,816
  Likes Received: 10,106
  Trophy Points: 280
  Sijakuelewa Mpwa, ila shinikizo ni kubwa na uko sahhihi, irekebishe tu kidogo hasa upande wa source,
   
 3. Kwetu Iringa

  Kwetu Iringa JF-Expert Member

  #3
  Sep 12, 2011
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 359
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Mbona TFF haiguswi?? Iliruhusu ligi iendelee!! Lkn bado Nchimbi anahusika hata kwenye ligi
   
 4. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #4
  Sep 12, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Waambie anayetakiwa kujiuzulu ni Waziri mwenyewe dhamana kwenye Wizara ya Usafirishaji na Miundombinu kwa kutokufahamu wamiliki wa meli iliyozama.
   
 5. M

  Mapujds JF-Expert Member

  #5
  Sep 12, 2011
  Joined: May 12, 2011
  Messages: 1,291
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Ajiuzuru
   
 6. O

  OgwaluMapesa JF-Expert Member

  #6
  Sep 12, 2011
  Joined: May 24, 2008
  Messages: 10,948
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Duhu!! Kazi kweli kweli ,mpwa source fuatilia Vipindi vya TBC,2nd Fuatilia Miss Tanzania ilifanyika lini? na Wapi? Hope utakuwa umenielewa
   
 7. K

  Kifulambute JF-Expert Member

  #7
  Sep 12, 2011
  Joined: May 8, 2011
  Messages: 2,506
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Ajiuzuru na kufunguliwa mashtaka si mtanzania yawezekana
   
 8. Rugaijamu

  Rugaijamu JF-Expert Member

  #8
  Sep 12, 2011
  Joined: Jul 10, 2010
  Messages: 2,826
  Likes Received: 553
  Trophy Points: 280
  <br />
  <br />
  Sio hao tu....Mbona wale waliofanya "tamasha la wazi" kuzindua kampeni kule Igunga hawatajwi?
   
 9. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #9
  Sep 12, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
 10. RedDevil

  RedDevil JF-Expert Member

  #10
  Sep 12, 2011
  Joined: Apr 30, 2009
  Messages: 2,287
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  Nadhani tuanze na yule wa Zanzibar waziri mwenye dhamana ya usafirishaji bado hatujasikia kawajibika, "ajiuzuru mara moja" then afuate na huyu wa bara (aka wa muungano). Kiufupi mawaziri wote wenye wizara husika wanatakiwa kujiuzuru kwa hiari na kuonyesha ubinaaaadamu.
   
 11. Radhia Sweety

  Radhia Sweety JF-Expert Member

  #11
  Sep 12, 2011
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 4,448
  Likes Received: 345
  Trophy Points: 180
  Sidhani kama ana sababu ya kuwajibika kwasababu TBC ni chombo huru. Mwenye wajibu wa kuchukuliwa hatua ni Boss wa TBC.
   
 12. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #12
  Sep 12, 2011
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,529
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280

  TBC ni tasisi huri inayosimamiwa na Bodi ya Wakurugenzi hivyo haiwajibiki moja kwa moja kwa Waziri.
   
 13. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #13
  Sep 12, 2011
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,306
  Likes Received: 5,596
  Trophy Points: 280
  Hapo kuna kazi kubwa sana ya kushosheana vidole...sidhani kama itasaidia!ubora wa vyombo unadhibiwa na nani??kwa nini waruhusu meli kama ile imechoka haswa ile meli...pia nani aliruhusu iondoke na mziko mkubwa kama ule??waliupima na kujua idadi ya abiria?tukimaliza huko ndio tuanze vitu vya ziada...sasa mawaziri,tv zetu mitandao etc!
   
 14. NYENJENKURU

  NYENJENKURU JF-Expert Member

  #14
  Sep 12, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 1,008
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Tz kujiuzulu?MMh sijui labda kwa shinikizo la mkuu wa kaya tu basi.
   
 15. M

  Massenberg JF-Expert Member

  #15
  Sep 12, 2011
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 1,173
  Likes Received: 1,061
  Trophy Points: 280
  Mnapopendekeza watu wajiuzulu ni kama hampo Tanzania vile. Hapo sasa hivi kila anayestahili kumwambia mwenzie ajiuzulu na yeye ataambiwa mbona wakati ule ulipofanya jambo fulani hukujiuzulu?
  Tukumbuke kuwa haya mnayoyaona ni utamaduni wa kishenzi ambao umekuzwa na kuendelezwa na mfululizo wa serikali za magamba. Kujiuzulu kwa waziri maana yake ni kwamba uchunguzi wa kweli na wa wazi utafuata na wahusika wote watapatikana, kushitakiwa, kunyang'anywa leseni na kisha kufungwa. Hayo mmeshayaona yakifanyika?
   
 16. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #16
  Sep 12, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  kaka una allergy na Vodacom eeenh! wale ni wadhamini tuuuu kaka.
   
 17. franksarry

  franksarry JF-Expert Member

  #17
  Sep 12, 2011
  Joined: Nov 9, 2009
  Messages: 1,107
  Likes Received: 229
  Trophy Points: 160
  BAADA YA UTAWALA WA MWALIMU, JE UTAMADUNI HUO WA KUJIUZULU UTOKE WAPI...?

  Hapa Tanzania hatuna utamaduni wa kujiuzulu......!
  Itakuwa miugiza ya aina yake, kwa kuwa maamuzi km hayo huwa yaanzia juu, Office ya JK kwa kuwakumbusha Ministers wale ambao Ministries zao zimepata matatizo au kashfa kufanya hivyo,
  so km JK haoni umuhimu wowote.., je unategemea hao Ministers wakale wapi..? Maana ukiangalia umuhimu wao kipindi hiki ni nn la ziada linalofanyika kwa kumpunguzia mtanzania umaskini?
  wameshindwa kuwapa Opportunities za kushiriki kuujenga Uchumi wa Nchi.
   
 18. segwanga

  segwanga JF-Expert Member

  #18
  Sep 12, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 2,790
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Hivi tanzania hii kuna m2 anaweza kujiuzuru.Ngereja kila siku anadanganya lkn yupo 2 anapeta.Wazir wa mambo ya ndani mabom yamelipuka mara 2 kukawepo na wito wa kujiuzuru akasema hakuna sababu ya kujiuzuru
   
 19. s

  smz JF-Expert Member

  #19
  Sep 12, 2011
  Joined: Dec 18, 2010
  Messages: 251
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Jamani,

  Kwa Tz yetu ya sasa tunayoishi, utamaduni wa kujiuzulu kwa hiari haupo kabisa (wa mwisho alikuwa Ali Hasan Mwinyi). Kama ungekuwepo basi Hussein Mwinyi angekuwa waziri wa kwanza kujiuzulu kwa majanga ya mabomu Mbagala na Gongolamboto. Kwa hiyo msitegemee Nchimbi afanye hivyo.
   
 20. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #20
  Sep 12, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Nchimbi aliona kinachoendelea kwenye TBC1 na ana contact za moja kwa moja na uongozi wa juu wa TBC kwa kuwashauri wasitishe maonyesho hayo na badala yake wageukie upande wa msiba ambao hisia za watu ziko. Wote wawili bosi wa TBC na Nchimbi wanabeba lawama.
   
Loading...