Waziri wa Habari alifanya hivi, ili Mobutu aonekane Mungu mtu

DIDAS TUMAINI

Senior Member
Nov 11, 2014
144
500
WATEULIWA WANA MENGI MOYONI.

Aliyekuwa WAZIRI wa Habari katika utawala wa Dikteta Mobutu, Mh. Sakombi Inongo siku moja alipewa saa chache abuni kitu ambacho kitamtukuza Rais wake na kumfanya watoto wanaokua kumuona ni MUNGU. Baada ya kutulia ofisini kwake,alikuja na ubunifu wa kipande cha video ambacho kinaonyesha picha ya Rais Mobutu akichomoza katika mawingu. Watoto katika Taifa la Congo waliishi wakijua Rais Mobutu ni MUNGU. Kipande kile cha video kilichezwa kabla ya kurushwa kipindi chochote kwenye luninga.

Waziri huyo ndiyo alihakikisha wasanii wa muziki na makundi mengine wanatunga nyimbo za kumsifia na kumtukuza Rais Dikteta Mobutu muda wote.
......................................................
Cha kumsikitisha WAZIRI huyo ni kwamba Rais wake huyo alikuja kutembea kimapenzi na mkewe. Tangu mkewe anatongozwa alikuwa anajua ila waziri huyo hakuwahi kufumbua mdomo kukalipia au kukemea jambo hilo kwa hofu ya kupoteza maisha yake. Katika mahojiano maalumu waziri huyo anakili wazi kuwa Rais Mobutu alikuwa akipenda sana kuchukua wake wa wateule wake.
.......................................................
 
darcity

JF-Expert Member
Jul 20, 2009
6,124
2,000
Nahofia Bashite,Kibudi,Kairiku ( balozi) huenda wakawa mfanano wa Waziri wa habari wa Mobutu
 
Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
172,932
2,000
Katika mahojiano maalumu waziri huyo anakili wazi kuwa Rais Mobutu alikuwa akipenda sana kuchukua wake wa wateule wake. hapa ndio penye msingi wa mada
WATEULIWA WANA MENGI MOYONI.

Aliyekuwa WAZIRI wa Habari katika utawala wa Dikteta Mobutu, Mh. Sakombi Inongo siku moja alipewa saa chache abuni kitu ambacho kitamtukuza Rais wake na kumfanya watoto wanaokua kumuona ni MUNGU. Baada ya kutulia ofisini kwake,alikuja na ubunifu wa kipande cha video ambacho kinaonyesha picha ya Rais Mobutu akichomoza katika mawingu. Watoto katika Taifa la Congo waliishi wakijua Rais Mobutu ni MUNGU. Kipande kile cha video kilichezwa kabla ya kurushwa kipindi chochote kwenye luninga.

Waziri huyo ndiyo alihakikisha wasanii wa muziki na makundi mengine wanatunga nyimbo za kumsifia na kumtukuza Rais Dikteta Mobutu muda wote.
......................................................
Cha kumsikitisha WAZIRI huyo ni kwamba Rais wake huyo alikuja kutembea kimapenzi na mkewe. Tangu mkewe anatongozwa alikuwa anajua ila waziri huyo hakuwahi kufumbua mdomo kukalipia au kukemea jambo hilo kwa hofu ya kupoteza maisha yake. Katika mahojiano maalumu waziri huyo anakili wazi kuwa Rais Mobutu alikuwa akipenda sana kuchukua wake wa wateule wake.
.......................................................

Jr
 
Daisy Llilies

JF-Expert Member
Apr 19, 2019
1,022
2,000
Kuna aliyezaa na mke wa balozi huko nchi ya Kufukirika. Balozi ameufyata akifungua mdomo tu ile hospitali itapata bill ya tax isiyolipika.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom