Richard

JF-Expert Member
Oct 23, 2006
14,939
20,399
Breaking News: Waziri wa fedha wa Uingereza Kwasi Kwarteng amejiuzulu.

Serikali ya Uingereza chini ya waziri mkuu Liz Truss na waziri wake wa fedha bwana Kwasi Kwateng ipo matatani kwa kushindwa kusimamia uzuri suala la uchumi.

Taarifa mbalimbali zasema serikali hiyo imezidisha kiwango cha ukopaji kutoka benki kuu kupitia amana za serikali lakini kiwango cha riba kimepanda na kutishia uhai wa fedha za wawekezaji na zile za mifuko ya hifadhi.

Serikali nyingi duniani hukopa fedha kupitia amana na huziuza kwenye mifuko binafsi au (hedge funds) na mifuko ya hifadhi(pension funds).

Waziri wa fedha bwana Kwasi Kwarteng ambae amekuwa akihudhuria mkutano wa IMF wa kila mwaka mjini Washington DC, ameitwa nyumbani mara moja na yupo njiani kuelekea London kwa mazungumzo zaidi na waziri mkuu Liz Truss.

Kwa mujibu wa gazeti ta "The Times" la Uingereza, baadhi ya wabunge waandamizi wa chama cha wahafidhina usiku wa jana walifanya kikao cha kuwabadilisha Liz Trus na Kwasi Kwarteng endapo hali ya uchumi itaendela kuzorota ambapo gharama za maisha nchini humo zimepanda zikiwemo gharama za mafuta na gesi kiasi cha kutishia kuwepo na ghasia kipindi cha baridi kitapoanza kushika kasi mwishoni mwa mwezi huu.

Katikati ya mwezi September mara tu baada ya kuingia madarakani serikali ilipeleka bungeni mapendekezo ya bajeti ndogo yalojumuisha pia kuwepo na kupunguza kodi yenye thamani ya pauni 45 bilioni ambayo ingefidiwa na serikali kukopa jambo lilopelekea kuleta mstuko kwenye soko la fedha na benki kuu kuingilia kati kuokoa fedha za mafao.

Mgogoro wa uchumi wa Uingereza umekuwa ukiisumbua serikali ya nchi hiyo kutokana na kushindwa kupitisha mapendekezo ya bajeti ndogo au "mini budget" ambapo serikali ilitaka kupunguza kiwango cha ulipaji kodi kwa matajiri na kuwaacha walipa kodi wa kawaida kulipa kiwango kilekile.

IMF pia ilitoa kauli ya kupinga bajeti hiyo ambayo iliita ni kutishia uchumi himilivu wa dunia jamblo ambalo lilipingwa vikali na viongozi wa nchi hiyo.

Pia uchumi nchi ya Uingereza imekuwa ukielekea kuanguka yaani "recession" ambapo uwezo wa nchi kuzalisha mali (GDP) ukiwa washuka kwa miezi mitatu mfululizo hali hiyo huchukuliwa kuwa ni kuanguka kwa uchumi au uchumi kufanya vibaya.

Mwanguko wa kiuchumi kwa nchi si jambo jema kwani ukuaji wake kusababisha kuongezeka kwa kiwango cha ajira, makampuni kupata faida kwa wingi na pia wawezekaji kufaidika. Pia hali ya uchumi ikiwa nzuri wananchi hulipa kodi na serikali kufaidika na kodi hizo ambapo huzitumia kulipia uendeshaji wake na shughuli za maendeleo.

Lakini kuna wakati serikali pia ukiona uchumi wanona huamua kupunguza kiwango cha ulipaji kodi na hapo ndipo serikali ya Liz Truss ilipoamua kufanya hivyo lakini kwa wale matajiri pekee jambo lilopelekea wananchi kulalamika kwa anawapendelea watu hao ambao wengi ndo wenye biashara.

Vyombo vingi vya habari nchini humo asubuhi hii vimeripoti kurejea ghafla London kwa bwana Kwarteng na ujumbe wake akiwemo gavana wa benki kuu ya Uingereza Andrew Bailey na kuacha mkutano huo vyombo vya fedha za nchi saba tajiri duniani au G7 ukiendelea jijini Washington DC.

Bwana Kwarteng jioni hii anatarajiwa kufanya mazungumzo ya dharura na waziri mkuu Liz Truss kutafuta namna ya kuokoa nafasi zao na kurekebisha sera yao ya uchumi ya upunguzaji viwango vya ulipaji kodi.

sky News
Kwasi Kwarteng has been sacked as chancellor three weeks after his mini-budget unleashed chaos in the economy, Sky News understands.

He was appointed to the role by Liz Truss only 38 days ago.

Mr Kwarteng's downfall was set in motion by the mini-budget on 23 September, in which he announced £45bn in unfunded tax cuts.

The mini-budget pushed the pound to a record low against the dollar, sent the cost of government borrowing and mortgage rates up and led to an intervention by the Bank of England.

Ms Truss and Mr Kwarteng, who have been close friends for years, insisted that the turbulence in the UK economy was part of a global problem exacerbated by the war in Ukraine and post-pandemic recovery.

But last week, after open revolt by Tory MPs and a record surge for Labour in the polls, the prime minister announced the first major reversal of mini-budget policies when she backtracked on scrapping the 45p top rate of income tax.

The second U-turn is expected to come on Friday afternoon, with the government set to raise corporation tax from 19% to 25% next April, despite promising not to do so in the mini-budget.

Vyanzo: Sky news ,The times
 
Updates:

Waziri mkuu wa Uingereza Liz Truss kuongea na waandishi wa habari mchana huu. Bado nafasi ya bwana Kwasi Kwarteng kuendelea kuwa waziri wa fedha inazidi kupungua.

Mkutano huo wa Liz Truss na waandishi unakusudia kuambiwa kuwa serikali imekubali kurekebisha bajeti yake na kuamua kuwatoza kodi kubwa makampuni makubwa yaani "corporation tax".

Hatua hiyo yafuatia kitendo cha bwana Kwarteng kukatiza safari yake ya Washington alikokuwa akihudhuria mkutano wa shirika la fedha duniani IMF na kurejea nchini humo mchana huu kitendo kinoashiria kwamba huenda tayari amejiuzulu.

Tetesi zimedokeza kuwa huenda bwana Saj Javid akateuliwa kushika nafasi hiyo wa uwaziri wa fedha nafasi ambayo aliishika kipindi cha utawala wa Boris Johnson. tetesi zingine zadai kuwa huenda bi Truss na Kwarteng huenda wote wakabadilishwa.

Tuendelee kufuatilia habari hii ya mgogoro wa kiuchumi nchini humo
 
Updates:

Taarifa mbalimbali zinotokea kwenye vyanzo mbalimbali vya habari zadai kuwa waziri wa fedha wa Uingereza bwana Kwasi Kwarteng ametolewa mbuzi wa kafara na amejiuzulu.

Tuendelee kufuatilia habari hizi za kusikitisha kuhusu gundu alo nalo mtu mweusi.
 
Nchi ilishakuwa ovyo kabla hawajaingia madarakani...nilivyoona teuzi zao hao weusi na wahindi wengi ktk cabinet nilihisi ni mbuzi wa kafara tu...leo weusi wapewe wizara nyeti! Ni kwa vile tu mambo siyo mazuri ulaya sa hivi
Ni kweli mambo si mazuri nchini humo uchumi umevurugwa sana na ukweli wafichwa kuwa tatizo ni kupeleka fedha kwenye vita.
 
Hata hapa hamna sehemu yeyote wanaitaja Urusi ila ukweli Vita wanayoifadhili Kijinga jinga kule Ukraine itawaumiza sana....Na bado serikali Nyingi zitaanguka ..Na Msimu wa Baridi kuna janga kubwa zaidi.... Dunia Nzima Inatafuta amani Ila hawa Wanaojiita G7 wanaua watu kwa kumtumia mtu mjing Kule Kyiv anaongea kama debe tupu eti apewe silaha nchi yake imegeuka kuwa Uwanja wa vita...Na hawa wanaomfadhili serikali zao zitaanguka zote....
 
Breaking News: Waziri wa fedha wa Uingereza Kwasi Kwarteng amejiuzulu.

Serikali ya Uingereza chini ya waziri mkuu Liz Truss na waziri wake wa fedha bwana Kwasi Kwateng ipo matatani kwa kushindwa kusimamia uzuri suala la uchumi.

Taarifa mbalimbali zasema serikali hiyo imezidisha kiwango cha ukopaji kutoka benki kuu kupitia amana za serikali lakini kiwango cha riba kimepanda na kutishia uhai wa fedha za wawekezaji na zile za mifuko ya hifadhi.

Serikali nyingi duniani hukopa fedha kupitia amana na huziuza kwenye mifuko binafsi au (hedge funds) na mifuko ya hifadhi(pension funds).

Waziri wa fedha bwana Kwasi Kwarteng ambae amekuwa akihudhuria mkutano wa IMF wa kila mwaka mjini Washington DC, ameitwa nyumbani mara moja na yupo njiani kuelekea London kwa mazungumzo zaidi na waziri mkuu Liz Truss.

Kwa mujibu wa gazeti ta "The Times" la Uingereza, baadhi ya wabunge waandamizi wa chama cha wahafidhina usiku wa jana walifanya kikao cha kuwabadilisha Liz Trus na Kwasi Kwarteng endapo hali ya uchumi itaendela kuzorota ambapo gharama za maisha nchini humo zimepanda zikiwemo gharama za mafuta na gesi kiasi cha kutishia kuwepo na ghasia kipindi cha baridi kitapoanza kushika kasi mwishoni mwa mwezi huu.

Katikati ya mwezi September mara tu baada ya kuingia madarakani serikali ilipeleka bungeni mapendekezo ya bajeti ndogo yalojumuisha pia kuwepo na kupunguza kodi yenye thamani ya pauni 45 bilioni ambayo ingefidiwa na serikali kukopa jambo lilopelekea kuleta mstuko kwenye soko la fedha na benki kuu kuingilia kati kuokoa fedha za mafao.

Mgogoro wa uchumi wa Uingereza umekuwa ukiisumbua serikali ya nchi hiyo kutokana na kushindwa kupitisha mapendekezo ya bajeti ndogo au "mini budget" ambapo serikali ilitaka kupunguza kiwango cha ulipaji kodi kwa matajiri na kuwaacha walipa kodi wa kawaida kulipa kiwango kilekile.

IMF pia ilitoa kauli ya kupinga bajeti hiyo ambayo iliita ni kutishia uchumi himilivu wa dunia jamblo ambalo lilipingwa vikali na viongozi wa nchi hiyo.

Pia uchumi nchi ya Uingereza imekuwa ukielekea kuanguka yaani "recession" ambapo uwezo wa nchi kuzalisha mali (GDP) ukiwa washuka kwa miezi mitatu mfululizo hali hiyo huchukuliwa kuwa ni kuanguka kwa uchumi au uchumi kufanya vibaya.

Mwanguko wa kiuchumi kwa nchi si jambo jema kwani ukuaji wake kusababisha kuongezeka kwa kiwango cha ajira, makampuni kupata faida kwa wingi na pia wawezekaji kufaidika. Pia hali ya uchumi ikiwa nzuri wananchi hulipa kodi na serikali kufaidika na kodi hizo ambapo huzitumia kulipia uendeshaji wake na shughuli za maendeleo.

Lakini kuna wakati serikali pia ukiona uchumi wanona huamua kupunguza kiwango cha ulipaji kodi na hapo ndipo serikali ya Liz Truss ilipoamua kufanya hivyo lakini kwa wale matajiri pekee jambo lilopelekea wananchi kulalamika kwa anawapendelea watu hao ambao wengi ndo wenye biashara.

Vyombo vingi vya habari nchini humo asubuhi hii vimeripoti kurejea ghafla London kwa bwana Kwarteng na ujumbe wake akiwemo gavana wa benki kuu ya Uingereza Andrew Bailey na kuacha mkutano huo vyombo vya fedha za nchi saba tajiri duniani au G7 ukiendelea jijini Washington DC.

Bwana Kwarteng jioni hii anatarajiwa kufanya mazungumzo ya dharura na waziri mkuu Liz Truss kutafuta namna ya kuokoa nafasi zao na kurekebisha sera yao ya uchumi ya upunguzaji viwango vya ulipaji kodi.
Haitakuwa jambo la kushangaza hiyo ni Mwamba effects a.k.a Motherland effect au Russia effect🤸🤸🏼‍♀️🤸🏃🚶
 
Kiini cha matatizo ya UK na nchi za Ulaya ni kule kukosekana kwa "Cheap energy"

Model ya uchumi wa Ulaya ni "cheap inputs".

Viwanda vinashindwa ku produce kwa sababu ya gharama za uzalishaji kuwa juu.
Na bado wanajifanya magaidi kumkomoa Mrusi,sasa Mrusi ameona isiwe tabu,gesi yake asiipitishe kwa jirani anaye kuhujumu,baadala yake iende Uturuki ili ielekee ulaya.
 
Hata hapa hamna sehemu yeyote wanaitaja Urusi ila ukweli Vita wanayoifadhili Kijinga jinga kule Ukraine itawaumiza sana....Na bado serikali Nyingi zitaanguka ..Na Msimu wa Baridi kuna janga kubwa zaidi.... Dunia Nzima Inatafuta amani Ila hawa Wanaojiita G7 wanaua watu kwa kumtumia mtu mjing Kule Kyiv anaongea kama debe tupu eti apewe silaha nchi yake imegeuka kuwa Uwanja wa vita...Na hawa wanaomfadhili serikali zao zitaanguka zote....
Na bado wanajifanya magaidi kumkomoa Mrusi,sasa Mrusi ameona isiwe tabu,gesi yake asiipitishe kwa jirani anaye kuhujumu,baadala yake iende Uturuki ili ielekee ulaya.

Hata hapa hamna sehemu yeyote wanaitaja Urusi ila ukweli Vita wanayoifadhili Kijinga jinga kule Ukraine itawaumiza sana....Na bado serikali Nyingi zitaanguka ..Na Msimu wa Baridi kuna janga kubwa zaidi.... Dunia Nzima Inatafuta amani Ila hawa Wanaojiita G7 wanaua watu kwa kumtumia mtu mjing Kule Kyiv anaongea kama debe tupu eti apewe silaha nchi yake imegeuka kuwa Uwanja wa vita...Na hawa wanaomfadhili serikali zao zitaanguka zote....
Nilijua vibwengo mtaleta hoja za ushabiki nikawaida yetu watz ndio maana mwiguru anatudharau sana
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom